Search This Blog

Saturday, May 14, 2011

KUELEKEA MECHI KALI YA LEO ITAKAYOPIGWA UWANJA WA TAIFA KATI YA TAIFA STARS NA BAFANA BAFANA MAKOCHA WATOA TAMBO ZAO.


Kocha wa timu ya bafana bafana PITSO MOSIMANE akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu mechi yao ya leo dhidi ya TAIFA STARS.
Aidha kocha wa wa bafana bafana PITSO MOSIMAME kikosi chake kitashuka dimbani bila nyota wake 14 wanaocheza soka la kulipwa ulaya huku pia ikiwakosa nyota wake wengine nane wanaochezea klabu za Ajax Cape town,Orlando pirates na Kaizer Chiefs zilizokataa kuwaruhusu kutokana na kukabiliwa na mechi muhimu za ligi kuu ya kwao,kombe la shirikisho na ligi ya klabu bingwa afrika"ukicheza siku ambayo haitambiliwi na FIFA ni tatizo, ila wachezaji nilionao watatumia nafasi hii kunionesha kwamba wanaweza alisema Mosimane. Aliwataka wachezaji wake ambao wako kwenye kikosi cha kwanza na leo watashuka dimbani kuwa ni pamoja na Itumeleng Khune (kipa) Reneilwe Letsholonyane na mfungaji wa bao la kwanza kwenye fainali za kombe la dunia zilizopita Siphiwe Tshabalala ambaye ndiye aliechaguliwa kuwa nahoza wa timu hiyo.Mosimame alisema kuwa wakali anaowakubali zaidi ndani ya kikosi cha stars ni winga Mrisho Ngassa n, Shadrack Nsajigwa na kipa juma kaseja aliowahi kuwaona katika mechi tofauti zilizowahi kuoneshwa na televisheni ya super sports.

No comments:

Post a Comment