Search This Blog

Wednesday, July 6, 2011

KAGAME CUP: YANGA VS RED SEA PREVIEW


Mabingwa wa soka Tanzania bara wanaingia uwanjani leo kuijaribu kuwafuata wenzao wa

Simba ambao jana walitangulia kufuzu kwa nusu fainali baada ya kuwafunga Bunamwaya

toka Uganda kwa mabao mawili kwa moja . Yanga wanacheza na Red Sea toka Eritrea na kwa mawazo ya haraka unaweza kufikiri kuwa huu utakuwa mchezo rahisi kwa mabingwa hawa wa soka Tanzania bara , lakini huu mpira bwana na kama wasemavyo wahenga mpira unadunda na hii inamaanisha kuwa lolote linaweza kutokea Yanga wanaweza kupoteza kama ambavyo wanaweza kushinda .


Ni muhimu kuutazama mchezo huu dhidi ya Red Sea kwa kutupia jicho yaliyotokea kwenye michezo mitatu ya Yanga na katika michezo mine ya Red Sea . Yanga wanaonekana kuwa na safu kali ya ushambuliaji ambayo inasaidiwa sana na safu nzuri pia ya kiungo ambayo inaonekana kuwa safi chini ya Rashid Gumbo na Nurdin Bakari huku Julius Mrope akisumbua san upande wa kulia na Kigi makassy akifanya mambo yake kwenye upande wa kushoto .Kenneth Asamoah , Davis Mwape na Hamis Kiiza wameonekana kuwa wasumbufu sana kwa safu mbalimbali za ulinzi kwa uwezo wao wa kujipanga na kuchachafya huku wakitumia nguvu na akili inapotakiwa na hadi kufikia mchezo dhidi ya Red Sea Yanga wameshafunga nane huku wakiwa na wastani wa angalau mabao mawili kila mechi huku Hamis Kiiza na Davis Mwape wakiwa wameshatupia bao mbili kila mmoja na kuna kila sababu ya kuamini kuwa wana uwezo wa kuongeza mabao hayo kwenye mchezo dhidi ya Red Sea .


Tatizo moja kwa Yanga limeonekana kuwa kwenye eneo la ulinzi ambapo pamoja na mabao nane ambayo yanga imeyafunga kwenye imeruhusu nusu ya idadi ya mabao hayo. Hii inamaanisha kuwa yanga imeruhusu wastani wa angalau bao moja kila mechi na hii ni hatari kwa kwa sababu siku ambapo Yanga itakutana na timu ambayo ina walinzi wenye nidhamu na kipa aliye na ubora hali inaweza kuwa ngumu . Red Sea inaweza kuwa timu ya aina hii , tazama jinsi walivyoweza kuwazuia Simba na kumaliza mchezo bila wavu wao kutikiswa na hapo utaona hatari ambayo Yanga wanaweza kukutana nayo .


Red Sea kwa upande wao wamecheza michezo mine ambapo ambapo wameza kushinda michezo miwili wakishinda moja bila dhidi ya Vital’O, na mchezo mwingine wakishinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Enticelles ya Rwanda na wamefungwa mchezo mmoja na Zanzibar OceanView ambao walifungwa mabao 2-0 na wametoka sare ya bila kufungana na Simba . Ukitazama matokeo hayo utagundua kuwa Red Sea wako kama Yanga kwa sababu wamefunga mabao matano na wameruhusu wavu wao kuguswa mara tatu huku wakicheza michezo miwili ambapo walikomaa na kuondoka na “Clean Sheet” .


Matokeo haya yanaonyesha kuwa Yanga hawapaswi kuwadharau Red Sea kwa sababu wameonyesha kuwa hawatabiriki , hujui utgemee lini toka kwao kwa sababu mashabiki wengi ambao walishuhudia Red Sea ikifungwa na Ocean View walitaraji kuwa Simba wangewamaliza kabisa lakini haikuwa hivyo na hata kwenye ufungaji wanaonekana wanao uwezo wa kufunga hivyo kama ngome ya Ynga iliyoko chini ya kina Canavarro na Chacha Marwa , Godfery Taita na Shadrack Nsajigwa na wakati mwingine Oscar Joshua haitajipanga vyema maajabu yanaweza kutokea ila kwa waliowatazama Red Sea kwa jicho la tatu hawatashangaa kwa sababu wameshaona ishara zote za hilo kutokea .


Yaw Berko golikipa namba moja wa Yanga ni kipa imara ambaye huwapa mashabiki uhakika wa asilimia mia moja na hamsini awapo golini kwa ustadi wake na uweoz wake mkubwa wa kudaka hata pale kwenye zile “one-on-one situation” lakini kama ilivyo kwa kipa yoyote ulimwenguni kuna vipindi ambapo mabeki wake hawampi ulinzi wa kutosha na ndio maana hadi leo ameruhusu wavu wake uguswe mara zisizopungua nne .


Hii ni hatua ya mtoano ambapo baada ya dakika tisini matokeo yakiwa sare mwamuzi ni penati na kwa aina ya mchezo ambao Red Sea wanaucheza usishangae wakaiingia na mtazamo wa kutafuta sare huku wakilenga matuta ili wawashangaze wapinzani wao ambao uenyeji wao unawapa ‘edge’ muhimu ya kushinda .


Mi vyema Yanga wakaamua kulinda kiukweli kwenye mchezo wa leo , Cannavaro na Chacha ambao ni wakabaji wazuri ila miongoni mwao hakuna wa kumuongoza mwenzie hali inayosababisha wakatike mara kwa mara na wakati mwingine kuchanganyana na kumwacha adui apite katikati yao kama ilivyokuwa kwenye mcezo wa kwanza dhidi ya El Mereikh , pia Taita na Nsajigwa wana kawaida ya kupandisha mashambulizi na kujisahau na kukamatwa kwenye ‘counter-attack” . Pia kama akicheza , Oscar Joshua ana kawaida ya kutumia nguvu nyingi kuliko maarifa hali ambayo vijana wa Red Sea wanaweza kuitumia na kuanza kujiangusha na kumtafutia kadi ambayo itaidhuru Yanga .


Kama safu ya ulinzi ya Yanga ikicheza kwa mipango na kwa nidhamu basi Yanga wana walau asilimia 75 ya uhakika wa kushinda kwa sababu kwenye ushambuliaji hawana matatizo mengi .

COPA AMERICA KUMBUKUMBU: NORBERTO "TUCH" MENDEZ


Kipindi michuano ya Copa America ikiwa inaendelea kutimua vumbi nchini Argentina huku tukishuhudia mataifa makubwa kisoka yakishindwa kufurukuta.Leo katika historia tunajaribu kumkumbuka mchezaji mwenye historia kubwa na mashindano haya, Norberto “Tuch” Mendez kutoka Argentina.

The “Tuch” alizaliwa mwaka 1923 jijini Buenos Aires, Argentina na aliaga dunia 22, June in 1998.

Ni moja kati ya wachezaji waliojijengea jina kubwa katika historia ya soka nchini Argentina na duniani kwa ujumla.

Akiwa moja ya wachezaji waliokuwa wakiunda kikosi cha Argentina kilichotawala bara la Amerika kwa kuchukua makombe la Copa Amerika mara 3 mfululizo chini ya kocha anayeongoza kuchukua kombe hilo – Guillermo Stabile, Norberto alifanikiwa kufunga mabao 17 katika mechi 17 za mashindano yote matatu kuanzia mwaka 1945-1947 huku akiweka rekodi ya kuwa moja ya wafungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo sambamba na Mbrazili Thomas Soares da Silva “Zizinho” wote wakiwa wametupia mipira nyavuni mara 17.

Tuesday, July 5, 2011

Simba ilivyocheza dhidi ya Bunamwaya…



Michuano ya Kagame Castle Cup imeendelea tena leo hii na watanzania wametoka uwanjani wakiwa na roho nyeupe baada ya moja ya wawakilishi Simba Sports Club kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuwafunga Bunamwaya toka Uganda kwa mabao 2-1.
Kwa mawazo ya haraka watanzania na wanasimba wote kwa ujumla wana kila sababu ya kuwa na raha kwa ushindi huo ambao unamaanisha kuwa timu ya Tanzania imejihakikishia angalau nafasi ya kufika hatua ya nusu fainali kwa vilabu vyetu viwili vya Tanzania.
Ila kwa jicho la tatu ambalo linatazama mbali zaidi ya michuano hii ya Kagame kikosi cha Simba kina mapungufu kadhaa ambayo kama yasipotatuliwa mapema basi huenda hata michuano yenyewe ambayo Tanzania ni mwenyeji inaweza kuota mbawa na kuwaacha watu wakishuhudia Kombe likipanda ndege na waliojipanga.

Simba kwenye mchezo wa leo walianza na kikosi cha wachezaji Juma kaseja akiwa golini , Juma said Nyoso , Derrick waluhya , Kevin Yondani na Amir Maftah wakiwa mabeki . Viungo walikuwajerry Santo, Patrick Mafisango , Mohamed Banka , Ulimboka mwakinge na Musa Hassan Mgosi akicheza kama kiungo mshambuliaji anayetokea upande wa kushoto na kwenye nafasi ya ushambuliaji alikuwepo Haruna Moshi Boban .
Kwenye kiungo…. Mafisango was Super!
Ukitazama kuanzia nafasi ya kiungo sehemu ya chini ya uwanja ambako alikuwepo Jerry Santo kurudi hadi golini Simba walikuwa vizuri kwa sababu kila idara imetimia kwa watu ambao wanacheza kwenye nafasi zao za asili japo kulikuwa na dosari kwa upande wa beki ya kulia ambako alilazimika kucheza Derick waluhya ambaye baadaye aliumia na Said Nassor Cholo alichukua nafasi yake na upande wa beki ya kushoto Amir Maftah alikuwa anajisahau kwa kupanda sana na kuchelewa kurudi kutimiza jukumu lake la kukaba . ukija kwa viungo wa upande wa juu wa uwanja kuanzia kwa Patrick Mafisango na wenzie wawili waliokuwa wanacheza pembeni Ulimboka Mwakingwe na Mgosi nako hakukuwa na tatizo sana kwani Mafisango ambaye sasa anaonekana kuzoeana na wenzie alicheza ipasavyo akitoa mipira ambayo ilikuwa haipotei mara kwa mara , alikuwa akimiliki na kuchia mipira kama nafasi yake inavyohitaji labda mwishoni tu alionekana kuwa na mbwembwe kupita kiasi ambapo mara moja au mbili alipoteza mipira kizembe , vivyo hivyo kwa Mgosi na hata Ulimboka .


kwenye idara ya ushambuliaji..
Shida kubwa ilikuwa ni ile ile ambayo imekuwa ikiwanyima wanasimba usingizi tangu mwanzo wa michuano hii nayo ni sehemu ambayo kwa asilimia kubwa ndio sehemu muhimu kuliko zote uwanjani nayo ni sehemu ya ushambuliaji ambako leo hii namba tisa alilazimika kucheza Haruna Moshi na mshambuliaji wake wa pili alikuwa Mohamed Banka na walikuwa wakibadilishana nafasi hizo mara kwa mara kuendana na ‘movement’ ya mpira . Eneo hili la ushambuliaji limekuwa tatizo sugu kwa Simba kwa sababu ambazo binafsi nashindwa kuzielewa . Simba haina mshambuliaji asili na hilo pekee ndio tatizo kubwa . Tazama timu iliyoanza na utagundua kuwa hakuna mchezaji yeyote kati ya kumi na moja walioanza na hata wale walioingia kina Cholo , Shija Mkina na Salum Machaku ambaye anabeba jukumu la ufungaji magoli . kuanzia kwa Banka , Mafisango , Mgosi , Boban , Ulimboka hakuna yoyote kati ya hawa ambaye ni mshambuliaji asilia .
Wanasimba mtakubaliana na mimi kuwa Simba hii ya leo si ile ambayo iliwahi kutwaa kombe la muungano huku ikitoa wafungaji bora watatu Emanuel Gabriel , Nteze John na Joseph Kaniki kwenye michuano hiyo hiyo .
Kocha mkuu wa Simba Moses Basena hakubaliani na ukweli huu , inawezekana ameshindwa kutambua tatizo hili lakini anajaribu kulikwepa .
Kipindi cha usajili kilikuwepo lakini Simba iliishia kuwasajili kina Boban , Ulimboka , na wengineo iliyowasajili lakini haikusajili mtu aliyezaliwa kufunga .

Haruna Moshi kuchezeshwa nafasi ya ushambuliaji…
Kwenye mechi dhidi ya Bunamwaya,Simba ilipata nafasi mbili za wazi, ya kwanza aliipata Haruna Moshi kwenye kipindi cha kwanza, alichohitaji kufanya kilikuwa ni kusogea na mpira na kulitazama lango na kuukwamisha mpira wavuni , kama angekuwa mshambuliaji asili angefanya hivyo lakini Haruna Moshi si mshambuliaji maskini ya Mungu , Haruna ni kiungo ambaye akili ya soka lake iko kwenye ufundi wa kumtengenezea mtu mwingine ndio aje afunge , alichofanya Haruna ni kutuliza mpira na kutazama mbele na kutoa pasi kwa Banka , kwa bahati mbaya pasi haikufika na nafasi ya goli ikapotelea hapo .



Viungo wasiokua na uwezo wa kufunga…
Kipindi cha pili wakati Simba wakionekana kukata tamaa huku mashabiki wakililia goli,Ulimboka alipata mpira karibu kabisa na lango tena mabeki walikuwa wamejisahau wakidhani Uli amejenga kibanda , Uli alipiga shuti lakini alimlenga kipa na nafasi ikapotea hapo . Baadae Simba walipata goli lililofungwa na Jerry Santo, bao lililotosha kuwapa ushindi lakini pengine wangeweza kupata ushindi wa uhakika zaidi ya huo wa mabao mawili kwa moja .
Kuna wakati kwenye mchezo huo wachezaji wa Simba walikuwa wanacheza kama Barcelona au Arsenal , wakipiga pasi kwa madaha na uhakika wa hali ya juu , na hili walikuwa wanafanikiwa kwa sababu unategemea nini zaidi ya pasi za visigino unapokuwa na Mafisango , Banka , Boban , Ulimboka , Mgosi ,Machaku na wengineo ila pungufu ni moja tu nalo ni ‘end product’ au matokeo ya pasi za visigino ambayo ni magoli kwani hadithi kwa Simba imekuwa ni pasi tamu za visigino halafu mwisho wa siku anatokea mtu anapaisha mpira .
Kama viongozi wa Simba wakiendelea kulifumbia macho tatizo la ufungaji basi mwaka huu wanaweza kuyasikia mafanikio kwenye bomba kwa sababu watani zao wana washambuliaji wanne ambao wanaweza kufunga na kwenye mechi za Yanga tumeshuhudia kuwa tatizo la ufungaji si kama la Simba kwani walau wastani wa mabao mawili kila mechi unatia matumaini.

MASOMO YA ZIADA (TUITION) YAMEUA MICHEZO

Makala yangu ya leo nataka niwakumbushe mbali kidogo, yaani tulipotoka na kufananisha na tulipo leo.
Kilichonishawishi kuandika makala haya ni kuangalia wako wapi wanamichezo wale niliokuwa nikiwaona zama zile na leo siwaoni kama vile Suleima Nyambui, Fillbert Bayi, Gidamis Shahanga, Mwinga Mwanjala, Kilangazi wa Kijibweni, Simkoko katika riadha, Titus Simba(sasa marehemu) Habibu Kinyogoli, Hugo, Lucas Msomba, Nashoni Nyabwa, Mzee Kwimba wa Bandari katika ndondi. Rose Walele, Judith Ilunda, Edna John, Maimuna Mrisha na Rose Temba katika Netiboli; achilia mbali katika soka ambako ndio hasa mahsusi kwa leo.

Najua watu wengi waliokuwepo miaka
ya nyuma wanaweza wakanielewa zaidi nitakapoizungumzia makala yangu ya leo. Nini hasa kilichotukumba hadi watu hao juu siwaoni au hatuwaoni leo.

Suala la elimu, kwa kiasi kikubwa ndio lilichangia sana kuua michezo. Leo, ninapozungumzia elimu nina maana ya kushuka kwa thamani ya mwalimu na kushuka kwa kiwango cha ufundishaji (sio elimu yenyewe) mashuleni.

Zama zile, mtu akiitwa mwalimu au mtoto wa mwalimu, alikuwa anaheshimika sana na ilikuwa si rahisi mwanafunzi wa wakati ule kukaa meza moja na mwalimu kupiga soga tofauti na ilivyo leo. Waalimu wakati huo, walikuwa wanajiheshimu sana kimavazi na kimaadili kwa ujumla. Walimu wa wakati huo walizingatia ule usemi wa wahenga kuwa “ualimu ni kazi ya wito”.

Suala la ufundishaji, namuangalia mwanafunzi wa wakati ule asubuhi akiingia darasani tu anakutana na somo la Hesabu, Kiswahili, Kiingereza halafu tunaenda mapumziko ya dakika kama 25 hivi tukirudi darasani unakutana na somo la Historia, Jiographia, Siasa halafu unatoka mnaenda kupata chakula cha mchana mkirudi mnakutana na Sayansi, Sanaa na maarifa ya nyumbani na kwa wiki mara moja mnakutana na somo la dini. Masomo yote hayo, walimu ni lazima waingie darasani na kufundisha kwa ufasaha na kuwapa na kazi za kufanya nyumbani “Home work”. Ukirudi nyumbani, baba akiangalia kazi nzuri iliyofanywa na walimu hana neno na wewe, hivyo unakuwa huru kuanzia saa kumi hadi saa moja usiku, hivyo unaenda kucheza michezo ikiwemo kandanda au soka.

Mwanafunzi wa leo anapotoka shuleni mzazi ukichukua madaftari yake kuangalia nini alichojifunza machozi yatakutoka; ni masomo hayazidi manne na ndani yake Hesabu na Kiingereza huyakuti, hivyo kwa mzazi mwenye kupenda maendeleo ya mwanao, ni lazima ile saa kumi ya kucheza mtoto atapelekwa kwenye masomo ya ziada yaani “Tuition”.
Hapo ndipo kipaji cha mtoto kinapozidi kupotea kama sio kufa kabisa.

Zama zetu, ile ikifika saa kumi kila mtoto yupo kiwanjani na viwanja vya mtaani vilikuwa vingi sana; lakini hiyo siyo mada yangu leo ya kwa nini leo viwanja sivioni!

Kimsingi, wote tulikuwa viwanjani tukicheza michezo ya aina mbalimbali ambayo iliboresha vipaji vyetu.
Mfano tukicheza mchezo wa kugusa mara moja huku unafunga goli la mwenzako “One touch”. Mchezo huu ulisaidia kupata wachezaji wenye uwezo wa kumiliki mpira na kuachia mara moja kama vile akina Aluu Ally, Method Mogella, Ramadhani Lenny, Jumanne Shengo, Mtemi Ramadhani, Hussen Masha na wengine wengi. Kulikuwa na mchezo unaitwa gombania goli; huo unakuwa na golikipa mmoja na wote mnamfunga yeye, hivyo kila mtu anapigana ili afunge akakae golini, hivyo tuliwapata akina Omary Mahadhi(sasa marehemu), Elias Michael(sasa marehemu), Athuman Mambosasa(sasa marehemu), Iddy Pazi, Juma Pondamali, Moses Mkandawile, Spear Mbwembwe, Kichochi Lemba, Hamis Kinye, Joseph Fungo na wengineo. Pia tuliwapata wafungaji kama vile akina Adam Sabu(sasa marehemu), Zamoyoni Mogella, Abdallah Burhani, Peter Tino, Gibson Sembuli(sasa marehemu), Venance Mwakalukwa “Best maridadi”, Ally Machela na wengineo.

Kulikuwa na mchezo wa kona, mtu mmoja anapiga kona wengine tunapiga vichwa kufunga, hapo vile vile tuliendeleza vipaji vya kupiga kona. Tulipata watu wapiga kona wazuri sana kama Abdulhamid Juma(sasa marehemu) Mohamed Kajole(sasa marehemu), Yusuph Bana(sasa marehemu), Fred Felix Minziro(sasa marehemu), Kenny Mkapa, Abubakari Kombo na wengineo wengi tu.

Pia tulipata wapiga vichwa wazuri sana kama Kitwana Manara Popat, Abdallah Luo(sasa marehemu), Abeid Mziba, Issa Athuman(sasa marehemu, Riziki Nassoro, Anthony Kifaro na wengine wengi.
Tulikuwa na mchezo unaitwa dobo dunda. Mtu akiingiziwa mpira katikati ya miguu yake, anapigwa magumi hadi akimbie aende akashike mahali ambapo mmepanga; ni mbali kama mita 50 vile. Kwa tukio hilo tulitengeneza wakimbiaji wazuri sana kama akina Willy Mwaijibe(sasa marehemu), Leonard Chitete(sasa marehemu), Sunday Juma, Kingsley Mwalilo na wengineo.

Kulikuwa na mchezo wa kushindana kupiga danadana, mtu anapiga hadi 1000; inakujenga uwezo wa kumiliki mpira kama walivyokuwa nao akina Mbwana Bushiri ‘Director’, Mohammed Hassan ‘Msomali’, Captain John Lymo; Sunday Manara ‘Computer’, Method Andrew ‘Master’, Charles Boniface, Samweli Owu, Ally Maumba, Hamis Thobias Gaga, Maico Paul ‘Nailon’.

Michezo hiyo yote tulikuwa hatufundishwi na walimu, ilikuwa inaanza kabla ya kupiga mtanange wenyewe wa watu 11, yaani ‘full game’.

Michezo hiyo yote hatuioni leo kwa sababu watoto hawana muda na wakati huo wachezaji wote ni lazima watoke mashuleni tofauti na ilivyo leo.

Asilimia 70, ukiacha ule uzao wa Kipingu wa kina Kaseja Juma, Mussa Mgosi, Nico Nyagawa, Haruna Moshi, Fred Mbuna na Wazir Mahadhi, wachezaji wengi baada ya kushindwa masomo na kukaa nyumbani, ndio wakaamua kwenda viwanjani kutafuta maisha katika njia nyingine ya soka. Hapo ndio unawakuta akina Juma Nyoso, Godfrey Taita, George Kavila, Ramadhani Chombo, Athumani Iddy na wengineo ambao wamecheza bila misingi ile ya awali waliyokuwa nayo akina Ahmed Amasha, Raha Msigalla, George Kulagwa, Nichodemus Njohole na Abdallah Mwinyimkuu (sasa marehemu), ambao tulianza kuwaona shuleni hadi ngazi ya juu ya elimu ambayo pia tuliwakuta akina Mwalusako, Leonard Tadeo, Denis Mdoe, Madundo Mtambo na wengineo.

Nasikia serikali leo inataka kurudisha michezo mashuleni, ni jambo zuri, lakini serikali ni lazima itambue tatizo liko wapi ili ifanikishe azimio hilo lililokusudiwa, vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.

Serikali ni lazima itoe kwanza kipaumbele katika suala la walimu; ni lazima iboreshe mishahara yao ili walimu wasitegemee kuuza visheti na karanga shuleni au kutegemea masomo ya ziada kwa wanafunzi.

Pia serikali ni lazima ihakikishe inawalipa walimu mishahara kwa muda unaotakiwa na kupatiwa vifaa vilivyo bora vya kufundishia.

Walimu pia ni lazima waelimishwe maadili ya ualimu kama wazazi. Wanatakiwa wawe kioo cha jamii; wawe wanajali kulea na kuwafundisha vijana kwa muda wote ili wazazi tusiwapeleke watoto wetu masomo ya ziada na jioni wakajumuike katika viwanja vya soka hapo ndio michezo inaweza ikarudi kama zamani.


E-mail: kennymwaisabula@yahoo.com

KENEDY MWAISABULA
“MZAZI”

DIRISHA LA USAJILI BARANI ULAYA.

KLABU YA REAL MADRID ITALAZIMIKA KULIPA ADA YA UHAMISHO YA EURO MILIONI 30 KWA AJILI YA BEKI WA KUSHOTO WA BENFICA FABIO COENTRAO MARA TU ATAKAPOFUZU VIPIMO VYA AFYA IKIWA NI PAMOJA NA YEYE BINAFSI KUMALIZANA NA KLABU HIYO.

Top 10 YA MABEKI GHALI

1 - Rio Ferdinand £29.1m (Leeds United to Manchester United, 2002)
2 - Fabio Coentrao £27m (Benfica to Real Madrid, 2011)
3 - Pepe £25m (Porto to Real Madrid, 2007)
4 - Daniel Alves £23.5m (Sevilla to Barcelona, 2008)
5 - Dmytro Chygrynskiy £22.5m (Shakhtar Donetsk to Barcelona, 2009)
=6 - Joleon Lescott £22m (Everton to Manchester City, 2009)
=6 - Lilian Thuram £22m (Parma to Juventus, 2001)
8 - David Luiz £21.3 (Benfica to Chelsea, 2011)
9 - Alessandro Nesta £21m (Lazio to AC Milan, 2002)
10 - Ricardo Carvalho £20m (Porto to Chelsea, 2004)

NINI KAZI YA DRFA KATIKA SOKA LA BONGO?

AMIN BAKHRESSA MWENYE SHATI JEUSI.




Nimejaribu kuangalia ligi ambazo zilikua zinashirikisha mabingwa wa mikoa katika vituo mbali mbali lakini nimeshtushwa kuona kwamba mwaka huu mkoa wa kinondoni haukua na timu ambayo ingeuwakilisha katika ligi ya kituo ili kuweza kupata timu ambazo zingekwenda daraja la kwanza kama ilivyo kwa Cosmo na Sifa Politani hii ni kutokana na ukiritimba ambao DRFA imeuleta kwa kuandaa ligi ya kanda ya Dar es salaam.
Sasa nabaki najiuliza hii ligi ya kanda ina faida gani wakati Kinondoni, Ilala, na Temeke tayari zinatambulika kimikoa zaidi ya wilaya katika mpira wa miguu na kwa kuthibitisha hilo tumeona katika michuano mbalimbali ya kitaifa hakuna mkoa unaoitwa Dar es salaam sasa hivi bali tuna mikoa kama hiyo nilioitaja hapo awali yaani ya KINONDONI, ILALA, na TEMEKE. Ukiangalia michuano ya Taifa Cup na Copa Cocacola je uhai wa Dar es salaam kimpira upo wapi? Na kama ingekua ipo mbona hatuioni pindi timu zinazotoka Dar es salaam zikishiriki michuano mbalimbali nje ya Dar es salaam? Nimekua kiongozi wa mpira katika ngazi ya wilaya mpaka ya Taifa nikiwa na Timu ya Villa Squad ya Dar es salaam katika ligi tofauti na sijawahi kupata ushirikiano wowote kutoka DRFA zaidi ya kusikia fitna na majungu ambacho chombo hiki kinaleta katika mpira wa Tanzania kwanza Management hawana zaidi ya Amini Bakhressa
Kwa kuthibitisha hili nyaraka mbalimbali za chama hiki hazikai ofisini zaidi ya kukaa ndani ya buti la gari la Bakhressa unapotoka nje utagundua kwamba viongozi wa vyama mbalimbali husika utawaona jinsi wanavyotoa maximum support kwa timu zinazotoka katika mikoa yao husika tofauti na DRFA ambayo hujikita zaidi pindi timu zinapopanda daraja na kukuta fomu za mapato zikiandika asilimia Fulani zinakwenda katika chama hiki ambacho hakina msaada wowote na timu husika.
Hebu tuiangalie Management ya DRFA na majukumu yake ni yapi in depth analysis kwangu mimi sioni zaidi ya kuzorotesha kama hivi Kinondoni haikutoa team katika ligi ya kituo na nikizidi kuangalia kwa umakini zaidi nimegundua haina management team zaidi ya mtu mmoja ambae ni Amini Bakhressa sasa sijui labda tuweke mjadala na kuitizama kwa sababu tunataka kulikomboa soka la Tanzania na kama tutaendelea kukumbatia vyombo au watu kwa maslahi yao hatutopiga hatua kwa sababu kuna mambo mengi ya kufanya zaidi kuliko kurundika vyama hewa ambavyo havina majukumu yoyote ndani ya soka la Tanzania.
Mdau wa blog IDDI GODIGODI.

KAGAME CASTLE CUP RESULTS.





ROBO FAINALI YA KWANZA YA MICHUANO YA KAGAME CASTLE CUP KATI YA EL MERREKH YA SUDAN NA ULINZI FC TOKA NCHINI KENYA IMEMALIZIKA PUNDE.


EL MERREKH WAMEFANIKIWA KUKATA TIKETI YA NUSU FAINALI BAADA YA KUFANIKIWA KUIFUNGA ULINZI KWA MIKWAJU YA PENALTY BAADA YA DAKIKA 90 KUMALIZIKA KWA TIMU HIZO KUFUNGANA BAO 1:1.,


MECHI INAYOFUATA SAIVI NI KATI YA BUNAMWAYA TOKA NCHINI UGANDA DHIDI YA SIMBA YA TANZANIA,


NUSU FAINALI YA PILI KATI YA SIMBA NA BUNAMWAYA IMEMALIZIKA KWA SIMBA KUSHINDA MABAO 2-1. JERRY SANTO KIUNGO WA KIMATAIFA TOKA NCHINI KENYA NDIYE ALIYEIFUNGIA SIMBA BAO LA USHINDI.

THOMAS MLAMBO IN DAR.

HAPA TULIKUATANA KTK JIJI LA CAPE TOWN NCHINI AFRIKA YA KUSINI MWAKA 2009 KWENYE SHUGHULI ZA UPANGWAJI WA RATIBA YA WOZA 2010.

VIWANGO VYA UBORA VYA WACHEZA TENNIS


WANAUME

1: NOVACK DJOKOVICH – SERBIA & MONTENEGRO

2: RAFAEL NADAL – SPAIN

3: ROGER FEDERER – SWITZERLAND

4: ANDY MURRAY – GREAT BRITAIN

5: ROBIN SODERLING – SWEDEN

6: DAVID FERRER – SPAIN

7: GAEL MONFILS – FRANCE

8: MARDY FISH – USA

9: TOMAS BERDYCH – CZECH REPUBLIC

10: ANDY RODDICK - USA


WANAWAKE



1: CAROLINE WOZNIACKI - DENMARK

2: KIM CLIJSTERS- BELGIUM

3: VERA ZVONAREVA - RUSSIA

4: VICTORIA AZARENKA - BELARUS

5: MARIA SHARAPOVA - RUSSIA

6: LI NA - CHINA

7: PETRA KVITOVA - CZECH

8: FRANCESCA SCHIAVONE - ITALY

9: MARION BARTOLI - FRANCE

10: SAMANTHA STOSUR – AUSTRALIA

NATAKA KUONDOKA MAN CITY - TEVEZ


Drama boy Carlos Tevez amesema wazi kuwa anataka kuondoka Eastlands.

Margentina huyo leo usiku amepeleka rasmi maombi ya kutaka kuondoka Manchester City akitoa sababu ya kutaka kuwa karibu na watoto wake Katie na Florencia.

Mpaka sasa matajiri wa Eastlands bado hawajajibu wala kujaribu kuongea Tevez ambaye kwa sasa yupo katika michuano ya Copa America na timu ya taifa ya Argentina.

“Ninasikita kuitaarifu Manchester City kwamba ningependa kuondoka katika klabu hii.Pia ningependa kusema kuwa nina heshima kubwa kwa klabu hii, mashabiki wake na mmiliki, Sheikh Mansour ambaye amekuwa na heshima kubwa kwangu.Natumaini watu wataelewa hali ngumu niliyokuwa nakabiliana katika kuishi hapa bila familia yangu.

Kuishi bila wanangu mjini Manchester imekuwa ni vigumu sana kwangu.Kila kitu ninachofanya, nafanya kwa ajili ya wanangu Katie na Florencia.Nahitaji kuwa karibu nao na kutumia muda mwingi kuwa nao pamoja.Nahitaji wawe na furaha kwa sababu maisha yangu yote yanahusu furaha yao.Nataka kuwa sehemu ambayo wataweza kuishi.

Kuwa nahodha wa City, kufaulu kucheza Champions League, kushinda FA Cup na kumaliza kama mfungaji bora kumenifanya nijisikie fahari.”

“Natumaini kwamba wengi wa mashabiki wa City wataelewa kuwa niliwapa kila kitu uwanjani na nilijitolea kwa asilimia 100 dimbani.Naamini nimetoa mchango kiasi katika kusaidia City kuendelea na mission ya kuwa mabingwa wa England na hatimaye wa ulaya.”

“Naamini na sina mashaka kuwa wachezaji na uongozi wa Manchester City watafanikiwa kwa kiasi kikubwa mbeleni.”-Alisema Tevez.

HAYE ASHIKA NAMBA 3 KWA UBORA HUKU AKITAKA MARUDIANO NA KLITSCHKO


Bondia muingereza David Haye amesema anataka pambano la marudiano kati yake na Wladimir Klitshchko baada ya kushindwa kwa pointi katika pambano lao lililopita jumamosi wiki iliyopita.
Akizungumza na BBC, Haye alisema "Ningependa nipate nafasi ya kushindania tena mataji yake, pindi atakapogundua kuwa hakuna bondia mwingine wa uzito wa juu ambaye anaweza kupambana nae vizuri, labda anaweza atarudi kwangu na kuniomba nicheze nae na nitakuwa tayari."
Haye ambaye alisema kuwa maumivu ya kidole chake kilichovunjika wiki 3 kabla ya pambano, yupo tayari kurudiana Klitschko kabla muda aliopanga kustaafu mwezi wa 10, na sasa ikiwa wanandugu wa Klitshchko wakiwa hawataki kupigana wenyewe, Haye ndiye bondia pekee anayebaki wa kupambana nae.
Hata hivyo Manager wa mabondia wa familia ya Klitschko amesema hawana na mpango wa kuwa na pambano la marudiano kati ya wanandugu hao wawili dhidi ya Haye.

Wakati huo huo listi ya ubora wa mabondia imetoka na ipo kama ifuatavyo:

1. Wladimir Klitschko

2. Vitali Klitschko

3. David Haye

4. Tomasz Adamek

5. Robert Helenius

6. Alexander Povetkin

7. Odlanier Solis

8. Alexander Dimitrenko

9. Chris Arreola

10. Denis Boytsov

11. Ruslan Chagaev

12. Nikolai Valuev

13. Eddie Chambers

14. Sam Peter

15. Jean-Marc Mormeck

16. Tony Thompson

Monday, July 4, 2011

CECAFA KAGAME CASTLE CUP:TAKWIMU NA KANUNI ZA CECAFA KWA MICHEZO YA ROBO FAINALI.



Hapo jana jioni kilifanyika Kikao kati ya CECAFA na wawakilishi wa vilabu vilivyoingia hatua ya Robo Fainal ya Michuano ya KAGAME CASTLE CUP.

Kwa pamoja walikubaliana mambo yafuatayo:

1} Kadi zote za Njano ambazo wachezaji walikuwa nazo kabla ya michezo ya robo fainal zimefutwa na kuanzia michezo ya robo fainal kila timu itaanza na Clean Sheet ya Card kasoro wachezaji wawili wa timu ya Ulinzi ambao ni Antony Edridu aliyepata kadi nyekundu kwenye Mchezo Uliopita na Laurence Owino ambaye ana kadi mbili za njano pamoja na Ssali Edward wa klabu ya Bunamwaya ambaye ana kadi mbili za njano ndio watakao kosa michezo ya Robo fainal na timu zao.


2} Kwa Michezo ya Robo fainal na ule wa kumtafuta mshindi wa tatu baada ya dakika 90 sheria ya Mikwaju ya Penalt itatumika,kasoro michezo ya nusu fainal na fainal ndipo italazimika kutumia dakika 30 za ziada kama timu zitachoshana nguvu katika muda wa kawaida.

NA

3} Timu zitakazofuzu katika Michezo yao ya Robo fainal ya kwanza siku ya Jumanne ya tarehe 5 ndizo zitakazocheza nusu fainal ya kwanza siku ya Alhamis ya tarehe 7 ya mwezi huu.


Wakati, Huo huo takwimu za Michuano hii hadi hivi sasa ni kama Ifuatavyo,

Simba ndiyo timu yenye nidhamu hadi hivi sasa baada ya kuwa na kadi mbili tu za njano toka mchezo wao wa kwanza,wakati timu ya Ports Fc ya Djibouti ndiyo inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi za njano(11),

Pia jumla ya kadi za njano 66 na kadi 9 nyekundu zimekwisha tolewa hadi sasa.

Jumla ya magoli 67 yamekwishafungwa kwa vituo vyote viwili vya Dar es Salam na Morogoro.









11 BORA KUTOKA SHAMBANI LA MASIA




LA MASIA ni neno la kihispania lenye maana ya nyumba ambayo inakuwa ndani ya shamba.
La Masia ni jina la kituo cha mafunzo ya soka cha klabu bingwa ya ulaya Barcelona F.C.Ndani ya academy hii wamepatikana wachezaji ambao wameupa mchezo wa soka ladha ya kusisimua.Kutokea katika kizazi cha baba mzazi wa Sergio Busquets mpaka kizazi hiki cha akina Leo Messi.
La Masia ilifunguliwa katika miaka ya 1970s kutokana na ushauri wa mchezaji aliyekuwa akiondoka katika klabu hiyo Johan Cruyff.
Mdachi huyu ambaye ni moja ya wachezaji waliofanikiwa sana akiwa ndani ya kikosi cha Catalan club, lakini mpaka anaondoka Nou Camp mwaka 1978, Barca bado walikuwa wanakikimbiza kivuli cha wapinzani wao wakubwa Real Madrid.Hivyo Johan Cruyff alimwambia raisi aliyekuwa akiingia madarakani kipindi hicho Josep Lluis Nunez kuwa ili kuweza kukabiliana na kuwashinda Madrid inabidi wafungue kituo bora cha soka kama ambacho Ajax Amsterdam wanacho.
Matunda ya kituo hiki cha soka yalianza kuonekana kipindi Cruyff aliporudi Nou Camp akiwa kocha miaka 10 baada ya kuondoka Catalunya, na tangu wakati huo La Masia imetoa mchango mkubwa katika kutoa wachezaji ambao wameiletea mafanikio makubwa timu ya Barcelona na Spain national team katika kuutawala ulimwengu wa soka.
Ndani ya kipindi hiki cha usajili vipaji kutokea katika shamba la LA MASIA wamekuwa gumzo na sasa kupitia blog hii tunawaletea listi ya wachezaji 11 waliotengenezwa la masia waliowahi na wanaoutikisa ulimwengu wa soka duniani.


GUILLERMO AMOR

Age: 43


Position: Midfielder


Country: Spain (37 caps, 4 goals)


Career apps: 524 (69 goals)


Barca apps*: 421 (67)


Trophies at Barca: 17


La Masia fact: Amor alikuwa ndio mchezaji wa kwanza kutoka La Masia kufanikiwa katika kikosi cha kwanza cha Barca.



Guillermo Amor alizaliwa katika katika sehemu maarufu ya utalii eneo la Benidorm, lakini alijulikana zaidi katika maeneo ya fukwe za mji wa Barcelona baada ya kufaulu kutoka La masia na kung'ara katika kikosi cha Johan Cruyff.Kiungo huyu alifanikiwa kucheza michezo 40 katika kikosi cha Spain, aliwakuwemo ndani kikosi cha Barca kwa mara 400 huku akishinda makombe 17 katika timu iliyokuwa inaundwa kocha wa sasa wa Barca Pep Guardiola, Hristo Stoichkov, Micheal Laundrup, Romaria na baadae Ronaldo na Luis Figo.Miaka 10 baada ya kuitumikia Catulanya, Amor aliuzwa Fiorentina na kocha Louis Van Gaal mwaka 1998.




SERGIO BUSQUETS

Age: 22


Position: Midfielder


Country: Spain (30 caps, no goals)


Career apps: 170 (4 goals)


Barca apps*: 139 (5)


Trophies at Barca: 10


La Masia fact: Sergio na baba yake Carles Busquets ambaye alikuwa golikipa wa zamani wa Barca wote ni madini ya La Masia.


Sergio Busquets ana umri wa miaka 22 tu, lakini kiungo huyu mkabaji ameshashinda makombe 10 tangu aingie katika kikosi cha kwanza mwaka msimu 2008-09.Ameshajitegenea nafasi ya kudumu katika vikosi vyenye ushindani vya Barca na timu ya taifa ya Spain.


CESC FABREGAS

Age: 24


Position: Midfielder


Country: Spain (58 caps, 4 goals)


Career apps: 303 games (57 goals)


Barca apps*: -


Trophies at Barca: -


La Masia fact: Fabregas anakumbuka aliambia siku moja na Guardiola, "Siku moja utakuwa utakuwa namba


Cesc Fabregas ndio mchezaji pekee katika listi hii ambaye hajawahi kuichezea Barca katika kikosi cha kwanza, lakini historia hii inaweza kufutika hivi karibuni.

Fabregas akiwa ndani ya La Masia kocha wake alikuwa anamficha pindi maskauti wanapokuja kuangalia wachezaji, kwa sababu aliogopa angechukuliwa lakini mwisho wa siku alishindwa kumzuia pindi mchezaji alipoona ufinyu wa nafasi yake katika kikosi cha wakubwa hivyo akaamua kujiunga na Gunners akiwa na miaka 16.

Kwa sasa akiwa na miaka 24 Barcelona wanajipanga kumrudisha Cesc nyumbani.Inakumbukwa kipindi wazazi wake Fabregas walipotengana, Guardiola alikutana na Fabregas na kutia saini katika fulana ya Cesc na akaandika "One day you will be Barca's No. 4." kitu ambacho kinaweza kikatokea muda wowote kutokea sasa.



PEP GUARDIOLA

Age: 40


Position: Midfielder


Country: Spain (47 caps, 5 goals)



Career apps: 477 (25 goals)


Barca apps*: 384 (11)


Trophies at Barca : 16 (plus 10 more as coach)


La Masia fact: Pep alikuwa ni kijana muokota mipira Nou Camp.

Pep Guardiola siku zote amekuwa akijuta maisha yakiungana na Barca.Guardiola alipoingia La Masia kama mchezaji aliwapigia simu wazazi wake na akawaambia ni jinsi gani alifurahi kuwepo mahali pale kwani alikuwa anaweza kuona uwanja wa Nou Camp kupitia dirisha la chumbani kwake.Hata baadae alipoondoka kwenda kucheza nchini Qatar na Mexico uwanja ule haujawahi kuwa nje ya mawazo yake.Guardiola kama mchezaji aliacha alama ya kukumbukwa ndani historia ya Barca, ingawa hakufunga mabao mengi, hakuwa mwepesi lakini alikuwa fundi na kiungo muhimu katika kikosi cha Johan Cruyff, Bobby Robson na baadae Van Gaal.Sasa anafanya walichokuwa wanafanya makocha wake akiwa na mafanikio zaidi.


ANDRES INIESTA ALIPOKUWA DOGO

Age: 27


Position: Midfielder


Country: Spain (58 caps, 9 goals)


Career apps: 415 (38 goals)


Barca apps*: 363 (33)


Trophies at Barca: 15


La Masia fact: Iniesta alikuwa na picha ya Guardiola aliyoibandika katika ukuta wa chumba chake alipokuwa La Masia.

Andres Iniesta ametokea katika ukanda wa Albacete - Spain, lakini wazazi wake walikuwa wanafahamiana na kocha wa Barcelona hivyo walimuomba amchukue mtoto wao afanye majaribio na timu hiyo.Barca waliona kipaji chake na Iniesta akahamia La Masia, ingawa ilikuwa vigumu sana kwa Iniesta kutengana na wazazi wake anakiri alilia sana kwa tukio hilo.

Kijana huyu mwenye aibu, uwezo wake unajidhihilisha wenyewe uwanjani akiwa na swahiba wake XAVI wametengeneza mfumo ambao ni hatari kwa sasa kwenye ulimwengu wa soka.Mwaka jana wote wawili walitajwa katika kugombea tuzo za Ballon d'Or . Pia Iniesta amewahi kutajwa na Wayne Rooney kama ndiye kiungo bora.Mwaka jana Iniesta ndio alifunga bao lililoipa ubingwa wa dunia timu ya taifa ya Spain, pia ameshinda makombe 15 akiwa na Barcelona.





LIONEL MESSI

Age: 24


Position: Forward


Country: Argentina (56 caps, 17 goals)


Career apps: 291 (186 goals)


Barca apps*: 269 (180)


Trophies at Barca: 15


La Masia fact: Messi Barca baada ya klabu hiyo kukubali kulipia matibabu kwa ajili ya ugonjwa wa upungufu wa homoni.


Lionel Messi amekuwa akitajwa kuwa ndio mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya soka, lakini inawezekana asingekuwa mchezaji kabisa kwa kuwa Margentina huyu alikuwa na matatizo ya upungufu wa homoni za ukuaji na familia yake ikiwa haina uwezo wa kugharamikia matibabu na hakuna klabu yoyte nchini Argentina ilikuwa tayari kumsaidia hivyo Barca kupitia scouts wake waligundua kipaji cha mchezaji na wakaamua kulipia matibabu, kilichofuata na kila mtu anajua.

Messi alikuwa mdogo sana alipojiunga na kikosi B ndani la masia hata kufikia Gerard Pique kuwahi kusema wachezaji wenzie walikuwa hawajui kwanini alikuwepo pale.Messi kwa sasa ni star asiyeshindika ndani ya historia ya Barcelona akiwa amefunga magoli 100 ndani ya misimu miwili iliyopita pekee.Ama kwa hakika Barca hawatajuta kamwe kulipia gharama za matibabu yake.


PEDRO RODRIGOEZ

Age: 23


Position: Forward


Country: Spain (13 caps, 2 goals)


Career apps: 177 (62 goals)


Barca apps*: 122 (45)


Trophies at Barca: 10


La Masia fact: Pedro ni moja kati ya wachezaji watatu waliopandishwa timu ya wakubwa na Pep Guardiola mara baada ya kuwa manager.


Pamoja na kuwa kipaji, Pedro anakumbukwa na watu wa La Masia kutokana na kujituma kwake.Alizaliwa mjini Tenerife, alikwenda Catulunya akiwa kijana mdogo na haraka akafanikiwa kumvutia kocha wa timu B - Guardiola katika msimu wa kwanza, na mara Guardiola alipopandishwa katika kikosi cha kwanza akamchukua Pedrito.

Winga huyu sasa ni moja wachezaji tegemeo katika kikosi cha Guardiola akiweka rekodi ya kufunga katika mashindano sita tofauti ndani ya msimu 1.Pedro pia ni mmoja ya wachezaji watatu waliopeleka kiio jijini Manchester baada ya kuitungua United katika UCL final 2011.Uwezo anaouonyesha Barca umemuongezea imani kwa kocha wa timu ya taifa ya Spain.



GELARD PIQUE AKIWA FABREGAS LA MASIA

Age: 24


Position: Defender


Country: Spain (33 caps, 4 goals)


Career apps: 196 (16 goals)


Barca apps*: 145 (11)


Trophies at Barca: 10


La Masia fact: Pique alianza kucheza kama kiungo mkabaji akiwa La masia.


Gerard Pique aliondoka Barca akiwa mdogo na kwenda kujaribu bahati yake nchini England kama ilivyokuwa kwa Fabregas, lakinit tofauti na mwenzie Pique alikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara akiwa na United hivyo akapelekwa mkopo Zaragoza na baadae akarudi tena United.

Pep Guardiola aliamua kumrudisha Pique nyumbani na baba Shakira akaishinda vita ya kugombea namba ya kushirikiana na Carles Puyol dhidi ya Rafael Marquez na Gabi Millito, halafu akafanikiwa kujenga moja ya safu bora za ulinzi duniani ndani ya kikosi cha Barca na timu ya taifa ya Spain.


CARLES PUYOL

Age: 33


Position: Defender


Country: Spain (94 caps, 3 goals)


Career apps: 605 (15 goals)


Barca apps*: 516 (9)


Trophies at Barca: 15


La Masia fact: Puyol alikuwa anakaribia kuuzwa kwa Malaga.


Carles Puyol alianza kucheza soka kama beki wa upande wa kulia na alipewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na mdachi Van Gaal.Ingawa alikuwepo Barca kwa muda mrefu lakini ilimbidi kusubiri mpaka mwaka 2004 kuweza kushinda kombe.Tangu kipindi hicho, Puyol ameendelea kushinda makobe kila kukicha, akiwa tayari ana medali 3 za Champions League, 5 za la liga na medali nyingine tofauti.

Puyol ni kiongozi asiyetia shaka ndani ya timu, akiwa beki wa kati anajua jinsi ya kuwapanga wachezaji wenzake, anajituma nakufanya kazi kubwa katika kuondoa na kupanga mashambulizi ya timu.Kufungwa kwa Barca mara nyingi katika msimu uliopita kulitokea alipokosekana uwanjani, kitu ambacho kinaelezea vizuri umuhimu wake ndani ya timu hiyo.



VICTOR VALDES AKIWA PEPE REINA

AGE : 29


Position: Goalkeeper


Country: Spain (4 caps)


Career apps: 483


Barca apps*: 406


Trophies at Barca: 15


La Masia fact: Valdes aliwahi kuondoka Barca na kwenda Tenerife kwa miaka 3 lakini baadae alirudi.


Victor Valdes alianza kuwemo ndani ya kikosi cha Barca chini ya Radomir Antic na alishikilia nafasi yake hata baada ya kuingia kwa raisi Joan Laporta ambaye alimsajili Rustu Recber . Valdes amekuwa mtu asiyeshindika katika nafasi yake akiwa moja ya magolikipa bora katika kizazi hiki cha soka.

Valdes sio golikipa pekee aliyetokea La masia , Pepe Reina nae alitokea shambani.




XAVI HERNANDEZ AKIWAKILISHA

Age: 31


Position: Midfielder


Country: Spain (101 caps, 9 goals)


Career apps: 638 (62 goals)


Barca apps*: 577 (58)


Trophies at Barca: 16


La Masia fact: Xavi alikuwa ndani ya kikosi cha Barca B kilichofanikiwa kucheza ligi ya daraja la pili mwaka 1998.


Xavi alionekana ndio mrithi wa Pep Guardiola, kitu ambacho kilimpa mzigo mkubwa kijana mdogo kutokana na mategemeo makubwa juu yake, hali ambayo ilipelekea Xavi kufikiria kuondoka Barca.Xavi alipata nafasi katika kikosi cha kwanza baada ya Guardiola kuumia na baadae alimrithi kabisa baada ya Pep kuondoka Nou Camp kelekea Brescia.

Kwa sasa Xavi amejiandikia historia ya kuwa moja ya viungo bora kuwahi kutokea katika historia ya soka duniani, na amekuwa ndio moyo wa klabu yake na timu ya taifa ya Spain.


KWAHERI LONDON-CLICHY AJIUNGA NA MAN CITY


Gael Clichy akiingia ndani ya makao makuu kwenda kusaini mkataba wa na kutambulishwa rasmi kama ndio mchezaji wa kwanza kusainiwa na matajiri hao kutoka Eastlands-Manchester.

CLICHY AWASILI JIJINI MANCHESTER KWA AJILI YA VIPIMO


GAEL CLICHY yupo jijini Manchester kwa ya kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha uhamisho wa kuelekea Eastlands. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa na Arsenal jana usiku alionekana akitoka katika mgahawa mmoja katikati ya jiji akiwa na mshauri wake Darren Dein.
Clichy anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo ili kuweza kukamilisha deal la £7m na Manchester City wiki hii.



COPA AMERICA:BRAZIL YANG'ANG'ANIWA NA VENEZUELA

Sunday, July 3, 2011

KLITSCHKO AMALIZA UBISHI WA DAVID HAYE



GUILLERMO STABILE MBABE WA COPA AMERICA


Wakati michuano ya Copa America ikaanza kupamba moto nchini Argentina, taifa la hilo la Amerika ya kusini kwa pamoja na Uruguay ndio mataifa mawili yanayoongoza kuchukua kombe hilo, yakiwa yamebeba kombe hilo mara 14 kila mmoja.

Katika makombe 14 yaliyochukuliwa na Argentina, makombe sita waliyachukua chini ya uongozi wa kocha Guillermo Stabile.

Chini ya Guillermo Argentina walitawala soka la Amerika ya kusini kwa kuchukua makombe 6 ya Copa America kati ya mwaka 1941, 1945, 1946, 1947, 1955 na 1957.Pia Guillermo ni moja ya makocha wachache wa timu ya taifa ya Argentina waliotimiza mechi zaidi ya 100, akiifundisha timu hiyo mechi 123 huku akishinda michezo 83.

Guillermo Stabile vilevile amewahi kuwa mchezaji mahiri katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina na aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi chache katika kombe la dunia, alicheza mechi 4 katika World Cup 1930 huku akifunga mabao nane.

Guillermo Stabile alistaafu kuifundisha Argentina mwaka 1960 na kuamua kuchukua majukumu ya kuwa mkurugenzi wa michezo katika shule ya mpira wa miguu, alitumikia nafasi hiyo mpaka mauti yalipomkuta mwaka 1966.