Search This Blog

Wednesday, July 6, 2011

COPA AMERICA KUMBUKUMBU: NORBERTO "TUCH" MENDEZ


Kipindi michuano ya Copa America ikiwa inaendelea kutimua vumbi nchini Argentina huku tukishuhudia mataifa makubwa kisoka yakishindwa kufurukuta.Leo katika historia tunajaribu kumkumbuka mchezaji mwenye historia kubwa na mashindano haya, Norberto “Tuch” Mendez kutoka Argentina.

The “Tuch” alizaliwa mwaka 1923 jijini Buenos Aires, Argentina na aliaga dunia 22, June in 1998.

Ni moja kati ya wachezaji waliojijengea jina kubwa katika historia ya soka nchini Argentina na duniani kwa ujumla.

Akiwa moja ya wachezaji waliokuwa wakiunda kikosi cha Argentina kilichotawala bara la Amerika kwa kuchukua makombe la Copa Amerika mara 3 mfululizo chini ya kocha anayeongoza kuchukua kombe hilo – Guillermo Stabile, Norberto alifanikiwa kufunga mabao 17 katika mechi 17 za mashindano yote matatu kuanzia mwaka 1945-1947 huku akiweka rekodi ya kuwa moja ya wafungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo sambamba na Mbrazili Thomas Soares da Silva “Zizinho” wote wakiwa wametupia mipira nyavuni mara 17.

No comments:

Post a Comment