Search This Blog

Sunday, July 3, 2011

GUILLERMO STABILE MBABE WA COPA AMERICA


Wakati michuano ya Copa America ikaanza kupamba moto nchini Argentina, taifa la hilo la Amerika ya kusini kwa pamoja na Uruguay ndio mataifa mawili yanayoongoza kuchukua kombe hilo, yakiwa yamebeba kombe hilo mara 14 kila mmoja.

Katika makombe 14 yaliyochukuliwa na Argentina, makombe sita waliyachukua chini ya uongozi wa kocha Guillermo Stabile.

Chini ya Guillermo Argentina walitawala soka la Amerika ya kusini kwa kuchukua makombe 6 ya Copa America kati ya mwaka 1941, 1945, 1946, 1947, 1955 na 1957.Pia Guillermo ni moja ya makocha wachache wa timu ya taifa ya Argentina waliotimiza mechi zaidi ya 100, akiifundisha timu hiyo mechi 123 huku akishinda michezo 83.

Guillermo Stabile vilevile amewahi kuwa mchezaji mahiri katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina na aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi chache katika kombe la dunia, alicheza mechi 4 katika World Cup 1930 huku akifunga mabao nane.

Guillermo Stabile alistaafu kuifundisha Argentina mwaka 1960 na kuamua kuchukua majukumu ya kuwa mkurugenzi wa michezo katika shule ya mpira wa miguu, alitumikia nafasi hiyo mpaka mauti yalipomkuta mwaka 1966.

No comments:

Post a Comment