Search This Blog

Wednesday, April 9, 2014

UCL ROBO FAINALI: BAYERN ISIYO NA HISTORIA NZURI ALLIANZ ARENA DHIDI YA TIMU ZA ENGLAND VS UNITED WANAOTAKA KUFANYA MAAJABU - ATLETICO HAWAJAIFUNGA BARCA NYUMBANI KWAO TANGU MWAKA 2014

Club Atlético de Madrid (1) v FC Barcelona (1)
• Atlético hawajawahi kuifunga Barcelona katika uwanja wao wa nyumbani tangu mwezi February 2010 wakati Diego Forlán na Simão walipoiwezesha kushinda 2-1. Barcelona hawajafungwa katika mechi tano walizoenda Vicente Calderón na walishinda mara mwisho kwenye uwanja huo ilikuwa katika mechi ya La Liga match mwezi May 2013, wakati Alexis Sánchez na goli la kujifunga la Gabi ikaipa ushindi wa 2-1 baada ya Radamel Falcao kuanza kuifungia Atletico.
• Atlético wanapigania kuingia katika nusu fainali ya kwanza tangu mwaka 1974 katika UCL wameshinda 16 kati ya 17 za mwisho walizocheza katika uwanja wao wa nyumbani kwenye michuano ya UEFA, ikiwemo michezo miwili mfululizo msimu huu.

Katika mechi 5 zilizopita kati ya Barcelona vs Atletico mshambuliaji Lionel Messi goli hata moja, hii ndio timu ambayo Messi hajaifunga kwa muda mrefu kutoka Spain.


FC Bayern München (1) v Manchester United FC (1)
• Manchester United ilikatisha rekodi ya Bayern Munich kushinda mechi 7 mfululizo walipotoka sae ya 1-1  Old Trafford wiki iliyopita - hii ni mara ya kwanza Bayern walishindwa kushindwa kushinda mchezo wa kwanza wa hatua ya kutoana katika michuano hii tangu walipofungwa na 1-0 na FC Basel 1893 msimu wa 2011/12 raundi ya 16. Mchezo wa pili uliisha kwa FC Basel kupigwa 7-0.
• Bayern wameshindwa kushinda mchezo wowote dhidi ya timu za England katika michezo minne iliyopita katika uwanja wao wa Allianz Arena lakini wameshinda mechi zote kasoro mbili kati ya 18 za UEFA ambazo walitoka sare katika mchezo wa kwanza, zikiwemo mechi 11 walizotoka sare 1-1 mechi ya kwanza. United wameshinda mechi 5 na kupoteza sita katika michezo yao 11 ya UEFA Iliyopita ambapo walitoka sare 1-1 katika mchezo wa kwanza  - pia wameshinda mechi 3 na kupoteza 2 wakati wanalipopata matokeo ya sare 1-1 nyumbani.

No comments:

Post a Comment