Search This Blog

Wednesday, April 9, 2014

DIEGO FORLAN: NILIMSHAURI LUIS SUAREZ AJIUNGE NA MANCHESTER UNITED

Mshambuliaji Diego Forlan, ambaye kwa sasa anacheza soka katika ligi kuu ya Japan na klabu ya Cerezo Osaka, amefunguka na kutoa kauli kuhusu mahusiano yake na mshambuliaji wa Liverpool  Luis Suarez.
Kwa mujibu wa makala ya Forlan katika jarida 442, amenukuliwa akisema kwamba alimshawishi sana Suarez kujiunga na Manchester United na sio Liverpool wakati Mruguay mwenzie alipokuwa Ajax 2011.
Forlan aliandika:
Tuna ukaribu na tunaelewana sana. Ni mpole na mstaarabu na anapenda kujifunza, mara zote huniuliza maswali na ushauri. Wakati Liverpool walipotoa ofa kwa ajili yake, nilimshauri aende Manchester United, lakini pia niliiongelea kwa uzuri Liverpool na historia yao. Nilimwambia namna nilivyofunga goli la kuwatoa Liverpool kwenye Europa League nikiwa na Atletico , mashabiki wao walinishangili baada ya mchezo.
Anapenda kuichezea Liverpool. Anaipenda Premier League – na mashabiki wanampenda kwasababu ni mshambuliaji na mchezaji mzuri kiujumla."

Pia Forlan akasema kama angeambiwa amchagua mchezaji bora wa EPL msimu huu basi ingekuwa ngumu kumchagua Kun Aguero au Suarez.

No comments:

Post a Comment