Search This Blog

Tuesday, April 8, 2014

TRANSIT CAMP, PAMBA FC, MKAMBA RANGERS ZASHUKA DARAJA!!

Pamba fc enzi hizo ilikuwa timu bora, lakini siku hizi hawana makali tena


Timu tatu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zitacheza Ligi ya Mkoa katika mikoa yao msimu ujao baada ya kushika nafasi za mwisho katika makundi yao, hivyo kushuka daraja.

Transit Camp imekata nafasi ya mwisho katika A wakati Mkamba Rangers imeshuka daraja kwa kukamata mkia katika kundi B. 
Nayo Pamba SC imerudi kucheza Ligi ya Mkoa wa Mwanza baada ya kuwa ya mwisho kwenye kundi C. 

Timu zilizopanda daraja kutoka FDL kwenda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao ni Ndanda SC ya Mtwara kutoka kundi A, Polisi Morogoro ya kundi B na Stand United ya Shinyanga iliyoibuka kinara katika kundi C.

No comments:

Post a Comment