Search This Blog

Thursday, April 10, 2014

RAIS WA TFF JAMAL MALINZI ATUA BUKOBA LEO HII, TAYARI KWA MKUTANO MKUU WA KRFA

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) Jamal Emil Malinzi amewasili leo Alhamis tarehe 10-4-2014 saa nne asubuhi katika Uwanja wa ndege wa Bukoba Mjini na kupokelewa na Wadau wengi, Huku ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe Rais wa TFF.
Bw. Jamal Malinzi baada ya kutua amezungumza na Viongozi wa Soka Mkoani hapa Kagera na baadae kuhudhulia Kikao cha kamati Tendaji ya KRFA na siku inayofuata utakuwepo mkutano mkuu wa KRFA.
Kulia ni Bw. Pelegrinius .A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF makao makuu, nae alikuwepo Uwanja wa Ndege Bukoba kwa mapokezi ya Rais wa TFF Ndugu Jamal Malinzi. Na hapa wakiteta jambo kwa kushirikishana na wadau pamoja na Viongozi.
Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi (kulia) akizungungumza na baadhi ya Viongozi wa Soka na wadau waliojitokeza kumpokea leo kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo. Kushoto ni Bw. Salum Chama Katibu wa KRFA Kagera, Anayefuata ni Bw. Ndg Ruge Masabala

Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Emil Malinzi kwenye picha na Mwandishi wa Mtandao wa Jamii Bukobasports.com leo muda mchache alipotua kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo.
Kwa furaha tele..Bw. Al-amin Abdul Abdul baada ya kumuona Kiongozi, Rais wa TFF leo hii kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe Rais wa TFF.
Karibu Mkuu, Bw. Al-amin Abdul Abdul  akimkarisha nyumbani Bukoba Bwana Jamal Malinzi
Bw. Pelegrinius .A. Rutayuga (kulia) akisalimiana na Al-amin
Bw. Willy O. Rutta, (Willy Kiroyera) nae alikuwepo uwanjani hapo kumpokea Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi.
Picha ya pamoja ilipigwa
Siku nyingi sana!!
Karibu Mkuu, Willy Kiroyera akimkaribisha Rais wa TFF
Hapa ndio Bukoba Mkuu, Mambo yamebadilika kwa muda mfupi tuu!
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akishuka kwenye gari kwenye Hotel aliyofikia ya Victoria Perch.
Karibu sana..
Wadau wa Soka Mkoani Kagera
Bw. Pelegrinius .A. Rutayuga akizungumzia swala zima la mkutano mkuu wa KRFA utakao fanyika hivi karibuni.Bw. Willy O. Rutta

1 comment:

  1. Jamani tumechoka na "Promo". Tunataka maendeleo kwenye Mpira. Kasi ya kupiga picha iendane na kasi ya kuleta maendeleo ya soka.

    ReplyDelete