Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ikiwa katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo.
Keptain Msaidizi wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) Frank William akipeana mkono na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo .
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia wakiwa wameshikilia Kombe la ushindi la Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC)baada ya timu hiyo kutembelea Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo.
Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ambao ni Bingwa wa
Dunia kwa mpira wa miguu kwa watoto wa mitaani wakiwasili nyumbani kwa
Waziri Mkuu leo mjini Dodoma mara baada kutembelea Bunge Maalum la
Katiba .
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa nahodha msadidizi wa timu ya
soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, Frank William, kombe la ubingwa
wa dunia wa soka la watoto wa Mitaani wakati alipowaandalia chakula cha
mchana kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11,2014. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)Wachezaji
wa Timu ya Soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, waliotwaa ubingwa
wa Dunia wakipata Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kwa ajili yao kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11,
2014. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu
ya Soka ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani, waliotwaa ubingwa wa Dunia
katika Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kwa ajili yao kwenye makazi yake mjini Dodoma Aprili 11, 2014. (Picha
na Ofiai ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo –Dodoma
Mfungaji
bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani kutoka Mwanza Tanzania, (TSC)ambayo
iliibuka mshindi katika mashindano Kombe la Dunia la Watoto hao
yaliyofanyika Brazil, mwaka huu Frank William ameishauri , Serikali na
jamii kuwasaidia watoto wa mitaani ili kuweza kukuza vipaji vyao.
Kauli
hiyo ilitolewa leo mjini Dodoma na William wakati walipolitembelea
Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma , wakiwa na viongozi wao ,ambapo
walipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia.
Alisema
siri ya ushindi wetu ni ushirikiano na kujituma, tukilikwenda
kuwakilisha watoto wengine wa mitaani. Hivyo aliomba jamii kuwasaidia
watoto wengi wa mitaani ambao hawana uwezo wa kupata elimu lakini wana
vipaji mbalimbali ili waweze kuvikuza.
Kwa
upande wake kipa bora wa timu hiyo, Emmanue Amos, alishauri Serikal
iweze kuwasaidia ili waweze kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018
ya kombe hilo.
Mchezaji
mwingine wa timu hiyo ,Denis David aishauri jamii isiwadharau kwa kuwa
ni watoto wa mitaani kwani wanavipaji wakipata watu wa kuwasaidia,
hivyo aliitaka iwekeze katika soka la vijana kwa sababu baada ya
miaka 20 ijayo mchezaji bora anapatikana kwa njia hiyo.
Aliwaomba wajumbe wa Bunge hilo ,kuwasaidia ili waweze kuvikuza vipaji vyao.
Naye
Kocha wa timu hiyo,Suileiman Jabir alisema wadau mbalimbali
kuwasaidia na kuwaendeleza watoto hao I, ambao ni wengi ambao wanaweza
kuwa na vipaji vya sanaa na utamaduni.
Akizungumzia
kuhusu mafanikio ya ushindi huo, ni kuwa na mpango wa kutafuta vijana
wenye vipaji ambapo wanaviendeleza na kuvikuza kwa kufanya maandalizi
ya kiutalaamu na kiufundi.
Jabir aliongeza kuwa waliwandaa kisaikolojia ili waweze kushinda katika mashindano hayo ya kimataifa.
Aliwataka
wajumbe wa Bunge hilo, kuhakikisha was aula la watoto hao, linapewa
kipaumbele na kuweka sheria itakayowadhibiti wakina baba wanatekeleza
watoto,huku akiisa jamii kuwasaidia watoto pale wazazi au walezi
wanapofariki dunia.
Rais
wa timu hiyo, Altaf Hirani aliiomba Serikali kuweza kuwasaidia kupata
kiwanja cha michezo kwa ajili ya watoto jijini Mwanza au kwenye
maeneo mengine ya nchi.
No comments:
Post a Comment