Search This Blog

Wednesday, April 2, 2014

CHAMPIONS LEAGUE ROBO FAINALI: MADRID KULIPIZA KISASI KWA DORTMUND - PSG VS CHELSEA VITA YA MATAJIRI NA MBWEMBWE KATI YA ZLATAN VS MOURINHO


Robo fainali ya Champions league inaendelea leo baada ya Manchester United kutoka sare ya 1-1 na Bayern - wakati Barca nao walitoka sare ya 1-1 na Atletico. Leo hii Real Madrid wapo nyumbani wakiwakaribisha Dortmund na PSG wanaumana na Chelsea jijini Paris. 
  
 Real Madrid vs Borussia DortmunD
Kwa upande wa Real Madrid, wishlist yao ilikuwa simple kidogo; Avoid Bayern Munich and Barcelona! Na kama wangeruhusiwa kujichagulia timu, bila shaka wangechagua Atletico Madrid au Manchester United.
Katika draw hii Real wamepewa Borussia Dortmund. Hii unaweza kusema ni repetition ya semi final ya mwaka jana ambapo Madrid waliambulia kichapo cha mbwa mwizi na kutolewa kwenye mashindano kwa aggregate ya mabao 4-3. Katika ushindi huo, ambapo Robert Lewandoski alifanikiwa kufunga mabao manne katika first leg, season hii amekuwa suspended kwenye first leg itakayofanyika Bernabeu na hiyo ni boost kubwa kwa Real kufanya revenge. Pia timu hizi mbili zime move katika directions mbili tofauti katika kipindi hiki cha miezi 12, Real Madrid chini ya Carlo Ancelotti imekuwa tishio zaidi na wapo katika nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa wa Spain, wakati Dortmund wao wanaonekana ku struggle katika ligi yao huku wakiandamwa na majeruhi ya key players wengi waliocheza kwenye katika nusu fainali iliyopita ya Jurgen Klopp kuwa ngumu kiasi dhidi ya Madrid
TAKWIMU
Real Madrid wanafanikiwa kuingia kwenye robo fainali kwa msimu wa nne mfululizo, na wameshinda kuvuka hatua ya nusu fainali kwenda fainali katika misimu mitatu mfululizo.
Rekodi ya Madrid ya nyumbani dhidi ya timu za Ujerumani ni Ushindi mechi 19, sare 4 na kufungwa 2, mechi mbili hizo wamefungwa na Bayern mwaka 2000 na 2001, Bayern ndio pekee ya Ujerumani iliyofanikiwa kushinda Santiago Bernabeu. Rekodi ya jumla ya Madrid dhidi ya timu za Ujerumani katika UCL - W12 L8.
Rekodi ya Dortmund dhidi ya timu za La Liga ni ushindi mechi 5 na wamefungwa 2, wameweza kushinda mara 1 tu katika ardhi ya Spain.
Msimu uliopita Madrid walitolewa na Dortmund nusu fainali , je msimu huu wataweza kuvuka kizingiti cha watoto wa Jurgen Klopp?

Paris Saint-Germain vs Chelsea
Pande zote mbili hazitakuwa too upset na draw hii. Kama ikikubalika kwamba Real Madrid na Bayern Munich are the class of this year`s competition, ukiacha Barca, PSG na Chelsea ndio next favourites kwenye mashindano.
PSG na Chelsea wote wanaonekana impressive kwa namna tofauti, walifanikiwa kufika hapo walipo baada ya kuwatoa Bayern Leverkusen na Galatasaray kwenye round iliyopita.
Kivutio kikubwa katika mechi za Chelsea mara nyingi kimekuwa maneno ya mbwembwe kutoka kwa manager wake, Jose Mourinho (the special one) ambaye anajivunia kikosi imara kinachoweza kuitikisa timu yeyote, mfano mzuri waulize mashabiki wa Arsena!
Kwa upande wa PSG wakiwa chini ya mchezaji wa zamani maarufu, mfaransa Laurent Blanc wakiwa wanaundwa na kikosi chenye wachezaji matata kama, Edison Cavan na thiago Mota Zlatan Ibrahimovich ambapo Chelsea kama wanataka kufika hatua ya nusu fainali basi ni lazima waweke mikakati ya kuwanyamazisha.

TAKWIMU
Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana katika hatua ya makundi ya michuano hii msimu wa 2004/05, Chelsea walishinda 3-0 jijini Paris, goli la kichwa la John Terry, na mengine mawili kutoka kwa Didier Drogba - na kumpa Mourinho ushindi wa kwanza katika UCL akiwa na Chelsea baada ya kutoka Porto.
Mara ya mwisho PSG kucheza nusu fainali ilikuwa msimu wa 1994/95 walipofungwa na AC Milan.
PSG hawajafungwa kwenye uwanja wa nyumbani katika mechi 28 za ulaya. Timu ya mwisho kushinda Parc des Princes katika michuano ya UEFA ilikuwa ni Hapoel Tel-Aviv.

Chelsea wapo katika kuisaka nusu fainali ya 7 katika misimu 11 iliyopita - je wataweza kuwanyoosha Ibrahimovic na wenzie?

No comments:

Post a Comment