Search This Blog

Tuesday, April 1, 2014

BAYERN MUNICH WASISITIZA HAWATOWAUZIA MAN UNITED TONI KROOS MWISHONI MWA MSIMU

Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesisitiza kwamba Toni Kroos hatojiunga na Manchester United mwishoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo mwenye miaka 24 hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo, mkataba wake wa sasa unaisha mwakani, wakati David Moyes alipigwa picha akizungumza na wakala wa mchezaji huyo January mwaka huu.

Mapema mwezi uliopita Kroos alikataa kukanusha kwamba kuna uwezekano wa kuhamia United baadae mwaka huu, lakini Bayern wamesisitiza kwamba mchezaji huyo hatoruhusiwa kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

"Kwa hakika Toni Kroos atacheza akiwa amevaa jezi ya Bayern Munich msimu ujao," Rummenigge told reporters on Monday.

Kroos amegoma kuwapa Bayern uhakika wa kuendelea kubaki na alipoulizwa kuhusu kujiunga na timu ambayo haitocheza Champions league msimu ujao alisema: "Nimegundua mengi yamekuwa yakiandikwa kuhusu hatma yangu. Hakuna kipya kati yangu na Bayern, sijaamua chochote, hakuna makubaliano yaliyofanyika na klabu yoyote," alisema Kroos. 


"Hili jambo litapata uamuzi wake wakati wa kiangazi ligi itakapoisha. Sio siri kwamba ligi kuu ya Uingereza inavutia sana."

No comments:

Post a Comment