Search This Blog

Tuesday, April 1, 2014

EXCLUSIVE: FRANK DOMAYO ASAJILIWA SIMBA - KUTUA MSIMBAZI MSIMU UJAO

Siku chache baada ya kugundulika mkataba wake ndani ya klabu ya Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu huu, klabu ya Simba imefanikiwa kumsajili rasmi kiungo Frank Domayo kutoka kwa mahasimu wao wa Wajangwani.

Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba Domayo anakaribia kumaliza mkataba wake na Yanga, na Simba walipogundua hilo wakazungumza haraka na mchezaji huyo na kufanikiwa kumpa mkataba mzuri huku Domayo akilamba millioni 40 kama fedha ya usajili.

Mchezaji huyo atajiunga na Simba baada ya ligi kumalizika. Simba wamejipanga kisawasawa kujiimarisha msimu ujao baada ya kufanya vibaya msimu huu - na usajili wa Domayo ni mwanzo tu wa kuimarisha timu yao.

*Happy fools day my dear readers*

13 comments:

 1. April Fool day...just fool yourself!!!

  ReplyDelete
 2. Happy Fools day !!!

  ReplyDelete
 3. DOMAYO HAWEZI KUSAJILIWA NA MBUMBUMBU,MUDA WA SIKU YA WAJINGA UMESHAMALIZIKA ULICHELEWA WAPI?

  ReplyDelete
 4. Jinga jinga weweeww...

  ReplyDelete
 5. Kama muda umemalizika basi mhandishi atakuwa sahihi............

  ReplyDelete
 6. Shafih acha kutupa presha wanajangwan

  ReplyDelete
 7. Mbona post ni ya monday 31st March? Alijidanganya mwenyewe

  ReplyDelete
 8. Welldone cimba we are waiting to see more than that

  ReplyDelete
 9. Nanyi pia msijidanganye wenyewe, siku ya wajinga ipo tarehe 31? Nafahamu ukweli wa tukio zima hadi anasaini Simba kwa Mkataba wa miaka Miwili kwa Sh 40 Mil. Ni kweli wapenzi wa Simba na Yanga... Domayo kasaini Simba

  ReplyDelete
 10. Nini Damayo!!!!????? Walikuwepo akina Semnuli na chama likaendelea....let him go

  ReplyDelete