Search This Blog

Tuesday, March 18, 2014

YAGUNDULIKA NAMNA QATAR WALIVYOTUMIA MLUNGULA KUSHINDA TIKETI YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2022

Ofisa mkuu wa FIFA Jack Warner yupo katika matatizo makubwa baada ya kutoka kwa taarifa kuhusu rushwa ilivyotumika katika kuipa Qatar uenyeji wa kuandaa michuano ya kombe la dunia 2022.

Gazeti hilo la Uingereza linaripoti kwamba familia ya Warner ililipwa takribani $1.2m na kampuni ya Qatar inayohusika na uandaaji wa World Cup.

Fedha zilitumwa kwa baadhi ya wanafamilia wake muda mfupi baada ya jaribio la Qatar kuandaa fainali hizo kufanikiwa.

Pia kampuni hiyo iliyotumika kumlipa Warner imetajwa kumilikiwa  Mohamed Bin Hammam, mjumbe wa kamati kuu ya FIFA kupitia Qatar, malipo hayo yanaonekana yalifanyika 2011.

$750,000 alilipwa kwa kuwekwa kwenye akaunti za watoto wake wa kiume na fedha nyingine $400,000 zililipwa kupitia akaunti ya mmoja wa wafanyakazi wake.

Shirika la ujasusi la Marekani FBI tayari limeripotiwa kuanza kufanyia uchunguzi tuhuma hizo dhidi ya Jack Warner. 

No comments:

Post a Comment