86 days to go
© Getty Images
Michuano ya kombe la dunia iliyofanyika Mexico mwaka 1986 iliacha kumbukumbu nzuri ambazo ni vigumu kusahaulika. Ukiachana na kiwango bora kabisa cha Diego Maradona aliyeiongoza Argentina kutwaa ubingwa, pia timu moja kutoka Afrika ya kaskazini - Morocco ilitengeneza rekodi.
Baada ya kutoka suluhu na England pamoja na Poland kisha wakaifunga Ureno 3-1, Simba wa Atlas sio tu waliweka historia ya kuwa taifa la kwanza la kiafrika kufuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya dunia - bali pia waliongoza kundi.
Ushindi mwembamba wa 1-0 wa Ujerumani dhidi yao ukawaondoa waarab hao kwenye kombe la dunia.