Rekodi za ufungaji wa mabao wa washambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na Daniel Sturridge msimu huu ni bora kuliko zote katika ligi kuu ya EPL tangu msimu wa 1965.
Suarez na Sturridge sio tu kwamba wanaongoza kwa ufungaji wa mabao na kushika nafasi mbili za juu katika msimamo wa ufungaji katika EPL, lakini hawa ndio washambuliaji pea ambao wamefunga mabao angalau mabao 18 kila mmoja katika hatua hii ya msimu tangu walipofanya hivyo washambuliaji wawili wa Blackburn Andy McEvoy na John Byrom mnamo mwaka 1965.
Mpaka wakati timu zikiwa zimecheza mechi 28, McEvoy alikuwa kashafunga mabao 25 wakati John Byrom alikuwa kashafunga mabao 18.
Suarez mpaka sasa kashafunga mabao 24 na Sturridge 18.
No comments:
Post a Comment