Search This Blog

Thursday, March 20, 2014

SIMBA NA YANGA WAPIGWA FAINI YA MILLIONI 25 KWA VURUGU KWENYE YA AL AHLY

Klabu za Yanga na Simba zimeagizwa kulipa jumla ya sh. milioni 25 kutokana na uharibifu wa viti na vurugu zilizofanywa na washabiki wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga italipa sh. milioni 15 ambayo ni gharama ya uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki kwenye mechi hiyo. Pia imepigwa faini ya sh. milioni tano kutokana na vurugu za washabiki wake. Nayo Simba imepigwa faini ya sh. milioni tano kutokana na washabiki wake kuhusika katika vurugu hizo.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.


Tunatoa onyo kwa washabiki wa mpira wa miguu kujiepusha na vurugu viwanjani ikiwemo uharibifu wa miundombinu mbalimbali ya viwanja ikiwepo viti, na tutachukua hatua kali zaidi kwa klabu na washabiki wake iwapo vitendo hivyo vitajitokeza tena.

2 comments:

  1. Nyie TFF mburula kweli, sasa simba hapo anaingiaje hadi muwapige faini? Mechi ile simba alikuwa na interest gani hadi muwahusishe na vurugu? Au kwa vile viti vimevunjwa upande unaosemekana wanakaa wana simba, kama sababu ni hiyo, mnaweza thibitishia umma wa watanzania kuwa kuna ushahidi wowote unao onyesha kuwa uwanja wa Taifa umegaiwa pande mbili, kuna upande wa Yanga na Simba! Udhaifu wenu na vyombo vya usalama kushindwa kuwakamata wahalifu wanaovunja viti, mnawapa mzigo hata wasiohusika. Wale Polisi mnaowapeleka uwanjani wanakwenda kuangalia mpira au kusimamia usalama? Wao ndio waliotakiwa kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa, na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao, hapo kusingekuwa na kuihusisha Yanga wala Simba, mnge dili tu na hao wahalifu.

    ReplyDelete
  2. .Kiuhalisia ni kweli kwamba vurugu zile zilianzishwa na washabiki wa simba waliokasirika kitendo cha washabiki wa yanga kwenda kukaa eneo lile,ingawaje kisheria ni vigumu kuthibitisha kama walikuwa washabiki wa simba kwa kuwa simba haikuhusika na mechi ile. simba kama klabu haikuwa inahusika na mechi ile hivyo ingekuwa vigumu kwao kuwajibika na udhibiti wa washabiki wake katika mechi isiyowahusu.Hata hivyo ukweli unabaki kwenye udhaifu wa vyombo vya usalama kuwadhibiti wahalifu hawa kwani watu wenye tabia ya kung'oa viti hawazidi 10 ni rahisi kuwadhibiti iwapo tutaacha ushabiki wakijinga na polisi nao kufanya kazi iliyowapeleka uwanjani.Wakati wa vurugu zile hakuna kiongozi yoyote wa juu wa TFF aliyeonekana kujali na askari badala ya kwenda kukamata wafanya fujo wakawa bize kuwafukuza washabiki wa Yanga waliokwenda kushangilia timu yao badala ya kuwadhiti wang'oa viti ambao timu yao ilikuwa haichezi lakini walikwenda kuishangilia timu ya Misri

    ReplyDelete