Search This Blog

Saturday, March 22, 2014

NINI MAONI YAKO KUHUSU HALI YA MAN UNITED BAADA YA VAN PERSIE KUTANGAZWA KUIKOSA MANCHESTER DERBY PAMOJA NA ROBO FAINALI VS BAYERN MUNICH

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Robin van Persie ameripotiwa kwamba amepata majeruhi ya goti baada ya kuumia katika mchezo wa raundi ya pili wa hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Olympiakos uliopigwa katika dimba la Old Trafford, jumatano wiki hii.

Van Persie ambaye alifunga hat trick iliyoipeleka Man United hatua ya robo fainali alitolewa nje na machela katika mchezo huo katika dakika za mwisho za huo, na leo hii baada ya kufanyiwa vipimo kiundani imegundulika amepata majeruhi yatakayomuweka nje kwa muda wa wiki 4-6.

Kwa maana hiyo mdachi huyo ataukosa mchezo dhidi ya Manchester City pamoja na mchezo wa kwanza wa robo fainali ya UCL dhidi ya Bayern Munich, hivyo kuiachia timu yake pigo zito.

Nini maoni yako kuhusu kukosekana kwa Van Persie katika kikosi cha United hasa katika kipindi hiki kigumu cha mwishoni mwa msimu?

2 comments:

  1. mm naamini timu bado nzuri tatizo lipo kwa moyes namna ya kuipanga timu na ndio tatizo la cku zote, rvp kukosa mchezo dhidi ya bayern hakika ni pengo japo mpira ni dk 90 lolote laweza kutokea hata hvyo bayern wanapewa nafasi kubwa kushinda hata kama rvp angekuwepo, unapocheza na bayern nafasi moja ya kufunga unapopata ni mhm sana sasa kwa man utd rvp ni mwny target anauwezo wa kufunga wkt wwte, kweli ni pengo kukosekana kwake lkn hata kama atakuwepo hawana nafasi kuitoa bayern

    ReplyDelete