Search This Blog

Saturday, March 22, 2014

CHELSEA VS ARSENAL: WENGER HAJAWAHI KUMFUNGA MOURINHO - LEO ANATIMIZA MECHI 1000, JE ATAIVUNJA REKODI YA KUTOPOTEZA MECHI 75 YA MOURINHO DARAJANI


Arsene Wenger anatimiza mechi ya 1,000 leo katika mchezo dhidi ya timu ambayo inafundishwa na kocha ambaye Wenger hajawahi kumfunga hata mara moja - Jose Mourinho.

Wenger akiwa na Arsenal amekutana mara 10 na Chelsea inayofundishwa na Mourinho, katika mara hizo zote Wenger hajaambulia ushindi hata mmoja, zaidi ya sare 5 na vipigo vitano.

Mourinho na rekodi bora ya katika uwanja wa nyumbani Stamford Bridge - hajapoteza mechi hata moja kati ya 75 Chelsea ilizocheza uwanjani hapo chini ya Mourinho.

Kuelekea mchezo wa leo Je rekodi ya Mourinho itaendelea, au Wenger atatimiza mechi ya 1,000 na ushindi dhidi ya kocha aliyemdharau kwa kumuita 'bingwa wa kufeli'?

Jibu litapatikana majira ya 9 kwa saa za Afrika Mashariki wakati mahasimu wa jiji la London watakapokutana kukata mzizi wa fitna.

No comments:

Post a Comment