Search This Blog

Friday, March 21, 2014

NADIR HAROUB, AMEJIIMARISHA NA KUIMAIRISHA SAFU YA ULINZI YA YANGA SC



Na Baraka MbolemboleMchezaji anatakiwa kupiga hatua siku zote katika uchezaji wake.
Unapopewa jukumu kama nahodha wa timu, linakuwa ni jambo la changamoto nyingine na linachangia kumfanya mchezaji kuwa bora, na ni kitu ambacho kinaweza kumfanya mchezaji kubadilika katika uchezaji wake kiujumla. 
Kama nahodha unakuwa na kiwango kisichobadilika, hasa katika
kupandisha kiwango cha uchezaji, watu watakusema kwa namna
wanavyotaka.

Kiwango cha sasa cha nahodha wa timu ya Yanga SC, Nadir Haroub kimeonekana kuimarika na kupanda. Wakati, Yanga ilipocheza michezo miwili dhidi ya Al Ahly ya Misri, katika ligi ya mabingwa Afrika, mapema mwezi huu na kuruhusu bao moja katika muda wa dakika 180, safu ya ulinzi ilionekana kucheza kwa umakini mkubwa huku, Nadir na Kelvin Yondan wameonekana kucheza kwa maelewano mazuri.

Unapobadilishiwa mtu wa kucheza nao kama beki wakati mwingine
linapelekea mchezaji kupata wakati mgumu kutokana na mazoea ambayo mara nyingi hujenga uimara wa beki kama safu muhimu ya timu. 
Nadir, amekuwa akicheza sambamba na Kelvin kwa msimu wa pilisasa, lakini kiwango chao wakicheza pamoja katika michezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Azam FC, na namna ubadilikaji wa walinzi mchezo ni mzuri tofauti na walivyokuwa wakicheza katika siku za nyuma.

Hakuna kitu kigeni katika soka. Wakati mwingine mchezaji unatakiwa kuzoea kucheza tofauti na mchezo uliouzoea kutokana na msaidizi wako anavyokuwa akitimiza majukumu yake. Nadir ameonekana kupunguza makosa yake ya kuondoka mara kwa mara katika eneo lake la muhimu, kwa kuachana na stahili yake ya kucheza kwa kumfuata mshambuliaji wa timu
pinzani. 
Kama, Namba Tano, Nadir anatakiwa kucheza kwa kuwaongoza
wasaidizi wake huku yeye akicheza kwa kusahihisha makosa yanayokuwa yanafanywa na wenzake.

Katika umri wa miaka 31 sasa, mchezaji huyo ameonekana kutulia chini ya kocha, Hans. Kuwa nahodha inasaidia kujenga mtazamo wa ushindi muda wote kwa mchezaji. 
Kama unakuwa nahodha na huna sifa hizo si kitu kizuri, Nadir ni mchezaji mwenye usongo wa kupata ushindi uwanjani.

Wakati mwingine beki unapitwa na timu inafungwa, ni kitu ch
a kawaida. Lakini ni lazima kufanya jitihada kuzuia hilo kadri
iwezekanavyo. 
Mlinzi makini ni yule anayetazama mambo yaliyo muhimu na kuyazingatia, si vizuri kusikiliza sana yale yanayokuwa yakisemwa juu yako unapokuwa mchezaji.

Unapocheza vizuri watu wakakusifia inamfanya mchezaji ajisikie
vizuri, lakini ukisemwa vibaya unatakiwa kuwa na umakini wa ziada ili kutofanya makosa zaidi. 
Nadir, amecheza na walinzi wengi wa kati katika klabu yake tangu aliposajiliwa mwaka 2007. Lulanga Mapunda, Wisdom Ndlovu,Isack Boakey, Chacha Marwa, Ibrahimu Job, Mbuyu Twite,
ila kiwango chake cha sasa akicheza na Kelvin kinaonesha kuimarika na kupevuka kiuchezaji. Ni wakati mzuri sasa kwa upande wake, na timu yake pia.

Nadir, ametokea kujiamini sana, kupunguza papara, kuondosha mipira inayoingia katika maeneo yao ya hatari, amekuwa akiwapanga wenzake na yeye binafsi katika mchezo, jambo ambalo limemfanya kucheza akiwa huru na kujiamini. 
Kama watazidi kuboresha mahusiano yao ya kiuchezaji na
Kelvin, Nadir atacheza kwa muda mrefu katika timu hiyo kawaida.
Lakini ni lazima kufanya jitihada kuzuia hilo kadri iwezekanavyo.
Mlinzi makini ni yule anayetazama mambo yaliyo muhimu na kuyazingatia

Si vizuri kusikiliza sana yale yanayokuwa yakisemwa juu yako unapokuwa mchezaji. Unapocheza vizuri watu wakakusifia inamfanya mchezaji ajisikie vizuri, lakini ukisemwa vibaya unatakiwa kuwa na umakini wa ziada ili kutofanya makosa zaidi. 

Nadir, amecheza na walinzi wengi wa kati katika klabu yake tangu aliposajiliwa mwaka 2007. 
Lulanga Mapunda, Wisdom Ndlovu,Isack Boakey, Chacha Marwa, Ibrahimu Job, Mbuyu Twite, ila kiwango chake cha sasa akicheza na Kelvin kinaonesha kuimarika na kupevuka kiuchezaji. Ni wakati mzuri sasa kwa upande wake, na timu yake pia. Ukuta wa Yanga umeimarika sasa, na kiwango cha Nadir kinapelekea safu nzima ya ulinzi kucheza kwa mpangilio na umakini wa kuepuka makosa yasiyo na ulazima.

5 comments:

  1. Hivi wewe ni wa wapi?Inasikitisha uonapo watu kwa makusudi kabisa wanapoamua kuibadilisha mieleka na kuiita soka.Siku zote sifa za kijinga na mpira wa magazetini ndivyo vinaliponza soka la bongo na kulifanya lisikue.Hakuna wakala/ kocha yeyote mwenye uweledi anayeweza kukubaliana na simulizi yako.Soka letu bado sana,hadi pale tutakapotengeneza kina SAMATA na ULIMWENGU wa kutosha,ndipo tutaweza kufikia ndoto tunazozitamani ktk soka,vinginevyo ni porojo na unazi wa kawaida tu.Jipange.

    ReplyDelete
  2. Ni vizuri kuchangia hoja bila kumponda mtoa hoja,yeye ametoa maoni yake na wewe unatakiwa kutoa ya kwako sio kujibu utumbo.Hivi kwa style hii ya kuchangia utumbo badala ya hoja wabongo tutapata katiba mpya kweli?

    ReplyDelete
  3. Kweli wewe ni division V,kama umekaa na kuamini kuwa ccm watatupatia katiba mpya iliyo bora basi utakuwa na matatizo ya kifikra au upo ndani ya mfumo unaotetea maslahi ya matumbo yao,kama sivyo unaweze kuwa Lumumba b7 project fame fc.Sote tumeona kwa macho yetu jinsi ccm na wapambe wao walivyong'ang'ania kura ya Ndiyoooo ktk kila jambo litakalohitaji maamuzi kwa njia ya kura.Kama watawala wangekuwa na nia njema na Taifa hili,basi kusingekuwa na mvutano na vitisho vya kuwadhibiti wajumbe wao ili kuwashinikiza wadimamie misimamo ya chama badala ya maslahi ya Taifa.Usijitie upofu na kutawaliwa na mahaba ya kiitikadi,kuwa mtu huru utauona ukweli.La mwisho usituletee utumbo wa siasa za bongo huku,zipeleke kwenye majukwaa husika,huku tunajadili soka letu ambalo mdau aliyetangulia hapo juu amelifananisha na mieleka.

    ReplyDelete
  4. haya mwingine naye huyo, utumbo plus,hujaelewa somo nenda kajipange.Mwenzako amehitimisha hoja yake kwa mfano wa katiba wewe badala ya kujikita kwenye hoja yake unajikita kwenye mfano wa katiba mbumbumbu

    ReplyDelete
  5. Kama huna hoja unakaa kimya unawaacha wenye hoja wachangie mada badala ya kuwajibu wanaochangia na kutoka nje kabisa ya mada.mtoa mada amefanya hivyo ili kupata maoni ya wenzake kuhusu alichokiamini na sio ufundi wa kukosoa wachanga madas wakei.Hapa hatuko uwanja wa taifa kwa wang'oa viti ambako hoja dhaifu huwa zinaishinda dhidi ya hoja zenye nguvu sababu tu wenye hoja dhaifu wanajua sana kutukana na kupayuka bila kuwa na pointi

    ReplyDelete