"
Mechi ambayo siwezi kuisahau katika maisha yangu ni ile ya Simba dhidi ya
Zamalek, kule Misri. Ukitoa maandalizi yetu kuelekea katika mchezo ule.
Wachezaji tulifanya kazi kubwa uwanjani. Mechi ilikuwa ngumu tangu mwanzo na
jamaa ( zamalek) wakapata bao ila maajabu mwamuzi alikataa. Ilikuwa katika
dakika kama ya 23 hivi, Matola alijifunga wakati akijaribu kuzuia mpira wa
krosi. Ilikuwa ni maajabu waarabu kukataliwa bao katika uwanja wao. Tukajua
ilikuwa ni nafasi yetu. Hatukupata muda wa kupumzika uwanjani. Muda wote
tulikuwa tukikimbizwa. Walipopata bao tukajiambia wasipate lingine. Tukafika
katika mikwaju ya penati tukiwa hoi, ila tukashinda mechi. Zamalek Vs Simba,
2003 ni mechi ngumu kuwahi kucheza katika maisha yangu ya soka "
No comments:
Post a Comment