Search This Blog

Friday, March 28, 2014

HATIMAYE MASHABIKI WASIOMTAKA MOYES KUPITISHA NDEGE JUU YA PAA LA OLD TRAFFORD ITAKAYOBEBA UJUMBE WA KUMTAKA KOCHA HUYO AONDOKE

Mashabiki wa Manchester United wanaochukizwa na mwenendo wa timu yao chini ya uongozi wa David Moyes wamefanikiwa kupata ndege itakayopita juu ya paa la uwanja wa Old Trafford jumamosi hii - huku ndege hiyo ikiwa imebeba bango la ‘Moyes Out’.
Ndege hiyo imepangwa kupita juu ya paa la OT kwa dakika 10 kabla ya mchezo kuanza na baadae kwa dakika 5 na wakati wa mchezo dhidi ya Aston Villa.
Kundi la mashabiki hao tayari limethibitisha kwamba kesho ndege hiyo yenye bango la  “Wrong One: Moyes Out.”
Bango hilo ni kinyume ya lile walilotaka kulishusha kutoka kwenye jukwaa la Stretford End linalosomeka  ‘Chosen One’.

No comments:

Post a Comment