Search This Blog

Wednesday, March 5, 2014

FRED CHIMELLA AACHWA KATIKA SAFARI YA TAIFA STARS BAADA YA KIPINDI CHA MIAKA 8.....


   Fred Chimella ( kulia ) akiwa na Shaffih Dauda.


Mtunza wa vifaa wa timu ya taifa ya Tanzania Fred Chimella ameachwa katika safari ya timu hiyo iliyoenda kuivaa Namibia katika mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA.
Hapo awali  alibaki aweze kuondoka na wachezaji Hassani Mwasapili na Edward Charles ambao walikuwa hawana hati ya kusafiria,lakini baada ya hati za wachezaji hao kuchelewa kutoka ilibidi safari hiyo isiwepo tena. 

Chimella ambaye safari yake ya kwanza nje ya nchi ilikuwa wakati Tanzania inaenda kupambana na Msumbiji mwaka 2006 - wakati ikiwa chini ya kocha mbrazil Marcio Maximo.

Taifa Stars ilikodisha ndege ya serikali kwenda nchini Msumbiji, lakini katika hali isiyoeleweka jina la Chimella halikuwekwa kwenye orodha ya wanaosafiri na timu. Hivyo timu ilipotoka kambini Msasani kuelekea Airport, Chimella alibaki hotelini.

Timu ilipofika uwanja wa ndege wachezaji wote na viongozi  waliingia kwenye ndege tayari kwa safari, lakini kocha Marcio Maximo alipoingia kwenye ndege hakumuona kit manager wake bwana Chimella, alipomuulizia mahala alipo,wachezaji wakamjibu kabaki hotelini kwa sababu jina lake halikuwemo kwenye listi ya wanaosafiri kwa sababu alikosa nafasi.
Maximo akachukua listi akaliona jina la Afisa Habari wa TFF wakati huo bwana Florian Kaijage na akawaambia viongozi wa msafara Mohamed Dewji na Crescentus Magori kwamba wamuondoe Kaijage kwa sababu hakuwa na msaada kwake na badala yake asafiri Fred Chimela. 


Hivyo iliwabidi Magori na Dewji wamfuate Chimela Msasani wakiongozwa na Polisi Escort ili wasikae kwenye foleni, hatimaye walifanikisha kumfuata Chimella na akasafiri na timu.Tangu wakati huo Chimella mwenye cheti cha utunzaji vifaa vya michezo alichokipata nchini Brazil hajawahi kuikosa safari ya Taifa Stars.

3 comments:

  1. Bado sana,baada ya kumaliza kuwaondoa "watu wa Tenga" makao makuu ya TFF sasa ni zamu ya walioko kwenye maeneo mengine ya TFF.Hata team manager Leopold Mukebezi Tasso:sijaona jina lake kwenye msafara huo.Kuna mwingine juzi tu ameshtakiwa kwenye kamati ya Maadili kwa kosa ambalo kimsingi anayetakiwa kuwajibishwa ni Katibu Mkuu wa TFF kwa kuwa ndiye katibu wa vikao vya kamati za TFF na ndiye anayeweza kuzidanganya au kuzipotosha kamati hizo.Hawa wanaondolewa ili kupisha nafasi kwa ndugu au marafiki wa baadhi ya viongozi wa juu wa TFF au watu waliosaidia viongozi hao kuingia madarakani

    ReplyDelete
  2. Maximo alikua ni kocha anayejielewa. Nasikitika sana mlipiga majungu had akaondoka...

    ReplyDelete
  3. Kuna ujinga wa kuwakomoa watu wanaodhaniwa kuwa ni wa rais Tenga kwenye huu uongozi wa malinzi,ambao mimi binafsi umeshaanza kunitia wasiwasi kama unao uwezo wa kutupeleka mbele kutokana na tantalila kuwa nyingi,ikumbukwe kuwa uongozi wa tenga ulikua na kazi moja kuu,kuijenga tff kuwa Taasisi inayoaminika,Hilo walifanikiwa halina ubishi,ushahidi ni makampuni kujitokeza kuwekeza fedha zao tff kutokana na trust yao kwa tff as a taasisi,kina malinzi walipoungia madarakani kazi yao kuu sasa tulitegemea Iwe ni kuujenga mpira wa uwanjani ili tuanze kupata ushindi,yani ilitakiwa wao kuboresha na kuyashughulikia mambo ya kiufundi sio tena kuanza upya kuunda taasisi mpya ya watu wao wapya,wanakosea na kupoteza muda,semina elekezi kama ile ya singida ilikua ya kazi gani?kila siku now zaidi ya siku 100 madarakani bado wanapanga safu ya uongozi na kuteua wajumbe wa kamati,kuunda kamati n.k.mpira watacheza lini ?malinzi aache uoga,ujinga mwingine ni kwenda kujitambulisha ofisini kwa Yule mbunge wa monduli,for real???rais wa tff unakwenda kujitambulisha kwa mbunge tu wa jimbo fulani badala ya kwa waziri mkuu ama spika!

    ReplyDelete