Search This Blog

Tuesday, March 4, 2014

FERGUSON AZUNGUMZIA UHAMISHO WA RONALDO - ASEMA MANCHESTER UTD INGEWEZA KUMUUZA £150M

Sir Alex Ferguson amefunguka kwamba alimwambia mkurugenzi mkuu wa Manchester UNITED David Gill kuweka bei ya £150 million kwa timu yoyote ambayo ingetaka kumsajili  Cristiano Ronaldo.

Ronaldo alijiunga na miamba ya soka ya Spain mnamo mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho iliyoweka rekodi ya dunia £80million lakini Ferguson anaamini Raisi wa Real Madrid Florentino Perez angeweza kulipa mara mbili zaidi ya fedha ya hizo walizolipa kumpeleka mwanasoka bora wa dunia Santiago Bernabeu. 
Katika mahojiano na gazeti la AS, Ferguson alisema: "Nilimwambia David Gill apange bei ya £150 million. Perez angeweza kulipa hicho kiasi cha fedha." 
Lakini matakwa ya kocha huyo hayakusikilizwa na Gill. "Kitu pekee kinachoniumiza nililisema hili kwa David Gill mara nyingi, kiasi ambacho amekitaja kwa Real hakikuwa sahihi. 
"Nilimwambia David, taja kiasi cha £150m.' 'Acha ujinga," akaniambia. 'Hawawezi kulipa kiasi hicho." 
Lakini, Real walivunja rekodi ya usajili kwa kutumia kiasi cha  £85 million kwa ajili ya kumsajili winga wa Wales Gareth Bale, jambo lilopelekea Ferguson, 'Vipi kama tungewaambia walipe £150m???" 
"Najiuliza kila siku Perez angesema nini kama tungewaabia walipe £150m. Ukizingatia wamemsajili Gareth Bale kwa £85 million, naamini wangekubali kulipa kiasi cha zaidi ya £80m .
"Nina uhakika, kwa sababu Perez alikuwa anajua kabisa aina ya ubora mchezaji aliokuwa nao, kama takwimu za Cristiano zinavyoonesha." 
Winga huyo mreno, ambaye alijiunga na United kutoka Sporting Lisbon 2003, tangu wakati huo mpaka leo ameshafunga mabao 238 katika mechi 233 akiwa na Real Madrid pia alifunga mabao 91 katika misimu yake mitatu ya mwisho Old Trafford.
"Kama tungelipwa £150 million, ningeongea kuhusu hilo jambo kwa kipindi chote kilichobaki cha maisha yangu, kwa sababu ingekuwa jambo kubwa na zuri kupokea kiasi hicho cha fedha, sio tu kutoka kwa Madrid bali timu yoyote. 
"Hata hivyo, Cristiano aliondoka akiwa na baraka zangu na tulipata kiasi kikubwa cha fedha."  

No comments:

Post a Comment