Search This Blog

Thursday, March 20, 2014

CRISTIANO RONALDO AIFIKIA REKODI YA MABAO YA FERENC PUSKAS

Cristiano Ronaldo amefikia rekodi ya mabao ya gwiji wa klabu ya Real Madrid Ferenc Puskas baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 wa raundi ya 16 Champions League dhidi ya Schalke.

Mshindi huyo tuzo ya Ballon d'Or alifikisha jumla ya mabao 242 katika mechi 236 alizoichezea Real, hivyo kumfikia Puskas.

Ronaldo amefikia rekodi hiyo ya Puskas akiwa amecheza mechi 25 pungufu ya zile alizocheza Puskas, pia Ronaldo ametimiza mabao hayo katika kipindi cha miaka 5 wakati Puskas alifunga mabao hayo katika kipindi cha miaka 8.

Endapo Ronaldo atafunga goli katika mcheo ujao wa Madrid ataingia katika nne bora ya wafungaji bora wa muda wote wa Madrid  huku Santillana (290), Alfredo di Stefano (307) na Raul (323) ndio watakaokuwa wamemtangulia.

No comments:

Post a Comment