Search This Blog

Thursday, March 27, 2014

BAYERN MUNICH YA GUARDIOLA INAWEKA REKODI NA KUZIVUNJA YENYEWE


Bayern Munich wameshinda mechi 10 za mwisho walizocheza ugenini katika ligi. Rekodi iliyokuwepo ilikuwa mechi 9 - waliiweka wenyewe msimu uliopita.

Bayern wameshinda mechi 19 kwenye ligi - hii ni rekodi mpya ya Bundesliga. Rekodi ya nyuma huko ilikuwa ushindi wa mechi 15, rekodi hii waliiweka Bayern wenyewe mwaka 2005.

The Bavarians wamefunga magoli mawili au zaidi katika mechi zao 19 walizoshinda - hii ni rekodi mpya kwenye ligi.

Huu ni ubingwa 24 Bayern Munich wa Bundesliga - rekodi mpya pia.

Boss wa Bayern Pep Guardiola alishinda makombe 14 katika miaka miaka yake minne ndani ya FC Barcelona, na sasa anaweza kushinda matano ndani ya msimu wake wa kwanza na Bayern.

Guardiola hajapoteza mchezo wowte wa ligi tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo - pia kwa ujumla Bayern hawajafungwa katika Bundesliga ndani ya miezi 18.

1 comment: