Search This Blog

Wednesday, March 19, 2014

AZAM YACHOMOA, YATOKA SARE NA YANGA,ZAFUNGANA BAO 1:1

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Didier Kavumbagu (wa pili kulia), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara ilipopambana na Azam  FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. (Picha na Francis Dande)
Heka heka: Golikipa wa timu ya Azam FC, Aishi Salum akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Mfungaji wa bao la Yanga, Didier Kavumbagu akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Azam FC.
Beki wa Azam FC, Gadiel Michael akimiliki mpira (kushoto) akiwania mpira huo ni mshambuliaji wa yanga, Hamis Kiiza. 
Mashabiki wa Yanga, wakishuhudia pambano hilo.
Mshambuliaji wa Yanga, simon Msuva akimtoka beki wa Azam FC, Bolou Michael.

9 comments:

  1. Bado ninajiuliza kwa nini timu zote zinaridhika na matokeo ya sare zinapocheza na Yanga?wiki iliyopita tulishuhudia Mtibwa wakipoteza muda uwanjani ili wapate sare,jana pia tumeshuhudia Azam baada ya kusawazisha bao wakipoteza muda ili wapate sare.hivi hizi timu hazihitaji ushindi zinapocheza na Yanga?Kama Azam na ukubwa wao na kocha wa kiwango cha juu,wachezaji wa kimataifa na uwekezaji wa kiwango cha juu bado inalilia sare badala ya kutafuta ushindi ili ijiimarishe kileleni itakuwaje kwa timu ndogo kama Rhino,Simba,JKT Ruvu,Mgambo JKT na JKT Oljoro?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe utakuwa taahira kabisa, ndo maana sishangai unaposema Simba ni timu ndogo

      Delete
  2. Sidhani km kuna umuhimu wa kujibiwa ingawa unalazimisha ufanyiwe hivyo pale unapocoment huo ufinyu wa mawanda ktk soka umejaa ushabiki kuliko uanasports kwani kwa mwanasports yeyote huwezi kushangaa kwann timu zilizocheza na Yanga zikifurahia droo coz droo hugeuka ushindi kutoka na mazingira mf Simba alipgwa 3-0 first ahalf bt second ahalf wakachomoa zote why wasishangilie na Yanga wakajutia!? Hivi hili nalo tukufundishe!! Jana Azam wapo pungufu wanachomoa goli ktk mechi ngumu why wasishangilie!!! Mtibwa wapo punguf ktk mechi ngum wamefanikiwa kutopoteza game why wasishangilie tena walifanya hivyo hata walipicheza na Simba mbna hawajalalamika why ww!! Hv ushawahi kuiona hyo timu yako unayona bora ikishinda ama wakidroo ktk game ngum wakiwa pungufu?? Je ushawahi kuiona ikichomoa goli zaidi ya 2 ktk game ngumu itaje hyo game km ipo heshimu walichowez kukifanya usichoweza kufanya mbna Yanga walishangilia kutolewa kwa penalt kule Cairo ushajiuliza hilo acha ushabiki SOKA LA MIPANGO NJE YA UWANJA TUTAISHIA HATUA ZA AWALI KIMATAIFA BADILIKENI!! Mazingira ya droo ni ushindi acha wafanye walivyofanya!!!

    ReplyDelete
  3. maneno ya mkosaji hayo

    ReplyDelete
  4. Sasa nimeelewa kwa nini Rage huwa anawaita watu fulani mbumbumbu.Hoja hapa sio kushangilia sare bali kupoteza muda ili upate sare wakati timu yako inahitaji ushindi ili ipate pointi tatu sio pointi moja.Kumbuka kwamba utakapokosa ubingwa kwa ajili ya pointi mbili ulizozikosa kwa sare kigezo cha kwamba ulikuwa pungufu uwanjani hakitakuwa na mashiko.Hakuna kocha anayeandaa timu yake kwa ajili ya sare na hapa ukiona wachezaji wanapoteza muda badala ya kutafuta ushindi na kocha anafurahi ujue kuna tatizo.Ukitaka kuthibitisha hili fuatilia comments za Kibadeni baada ya ile sare ya 3-3 uzilinganishe na comments za julio baada ya mechi hiyo,wakati Kibadeni anasikitika kwa matokeo hayo kwa sababu alijiandaa kushinda ,julio yeye anafurahia utafikiri aliandaa timu kwa ajili ya sare..Magoli ya Yanga yalifungwa ndani ya dakika 90 na pia yale ya simba yalifungwa ndani ya dakika 90,hakuna aliyerudisha goli la mwenzake bali alifunga la kwake,labda kama timu moja ilijiandaa kufungwa kwanza ili iwe inarudisha.Kucheza pungufu ya mtu mmoja siyo kigezo cha kutotafuta ushindi kwani zipo timu zinacheza pungufu na zinafunga magoli kama vile kwenye mechi ya mtani jembe ambapo timu moja iliweza kufunga goli huku ikiwa pungufu uwanjani.

    ReplyDelete
  5. OK sa nimeelewa kumbe timu ikiwa pungufu basi haina haja ya kutafuta ushindi bali sare inatosha.Kwa mtazamo huu soka la Tanzania bado lina safari ndefu sana

    ReplyDelete
  6. Ama kweli simba mambumbumbu.Mchangiaji katoa maoni yake kwa njia ya swali kwa nini timu zinapoteza muda ili zipate sare zinapocheza na yanga na hakuuliza kwa nini timu zinashangilia zinapotoka sare na yanga. wachangiaji badala ya kujibu hoja wanatoa matusi kama ya mwenyekiti wao Rage anavyowatukana.Hoja hujibiwa kwa hoja na sio utumbo na matusi.Inaonekana kwa washabiki wengi wa simba sc hasa wanaocomment humu walichojaliwa na Mungu vichwani mwao ni matusi,ndio maana hata awe profesa au mbunge ilimradi ni shabiki wa simba sc lazima atajibu matusi hata pale ambapo hayahitajiki,Hivi kwa matusi hayo ndio mtamuondoa Rage kweli?

    ReplyDelete
  7. Simba ni timu ndogo huwezi kuilinganisha na Yanga na Azam ndiio maana malengo ya Simba ni kushiriki mapinduzi cup na mtani jembe tofauti na wenzao ambao malengo yao ni ubingwa wa afrika na kombe la Kagame

    ReplyDelete
  8. Kung'oa viti wapi akili wapi

    ReplyDelete