Search This Blog

Wednesday, March 19, 2014

LIVE MATCH CENTRE: YANGA SC 1 - 1 AZAM FC FULL TIME



Azam imeendeleza record yake ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi kuu msimu huu.

FT: Yanga 1 Azam 1. (Kavumbagu 14, Friday 84)

92(+3)’ Yanga 1 Azam 1.

Mashabiki wa Yanga wanatoka uwanjani

88’ Yanga wanapata kona ya 8. Anatoka Kiiza anaingia Javu Hussein.

85’ Kipa wa Azam kalala chini na anapatiwa matibabu.

Kelvin Friday ana miaka 19 tu, lakini shuti alilopiga unaweza ukadhani ni mtu mzima

83’ Kelvin Friday anawasawazishia Azam

78’ Michael Gadiel wa Azam anaoneshwa kadi ya njano

77’ Yanga 1 Azam 0. (Kavumbagu 14)

73’ Yanga wanapata kona ya 5. Ngassa anaingia kuchukua nafasi ya Kavumbagu

71’ Erasto Nyoni wa Azam anapewa kadi nyekundu

69’ Yanga wanapata penalty baada ya beki wa Azam kushika, lakini Hamis Kiiza anakosa.

64’ Yanga 1 Azam 0. (Kavumbagu 14)

62’ Yanga 1 Azam 0. (Kavumbagu 14)

Dakika ya 60, Young Africans 1 - 0 Azam FC

58’ Yanga wamefanya shambulizi zito langoni mwa Azam kipa kaokoa. Hatari

57’ Yanga wanapata kona ya 3.

50’ Kelvin Friday anapoteza nafasi ya wazi baada ya kupokea pass maridadi toka kwa Kipre Tchetche.

Kusema ukweli kiwango cha Emmanuel okwi kimepungua kiasi ukilinganisha na wakati anaondokakwenda nchini Tunisia, Hii inaweza kuwa kutokana na kukosa kucheza mechi za ushindani kwa muda mrefu.

49’ Azam sub: Hamis Mcha anatoka anaingia Kelvin Friday.
Kiiza aliukokota mpira kutoka katikati akampasia Okwi, Okwi alipojaribu kumrudishia pasi kiiza kipa wa Azam Aishi Manula akadakaTatizo linatatuliwa na kipindi cha pili kinaanza.

Naona wachezaji wa Azam wanaonyesha uzalendo kwa kusaidiana na marefa kutengeneza nyavu

Mpira unachelewa kuanza inavyoonekana kuna tatizo kwenye nyavu za goli la kaskazini.
Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Azam FC

Dakika 1 imeongezwa kabla ya kwenda mapumziko.

43' Himid Mao anamchezea rafu mbya Hassan Dilunga. Teke lake limetua tumboni mwa Dilunga.

Dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza: Yanga 1, Azam 0

40’ Yanga 1 Azam 0.

35’ Yanga 1 Azam 0. (14 Kavumbagu)

Mara nyingi David Mwantika anamchezea madhambi Okwi, kwa mtazamo wangu Yanga walistahili penati.

32’ Yanga inapata kona ya kwanza. (1-0)

31' Shuti  kali la mbali kutoka kwa Okwi linatemwa na kipa Aishi Manula.

25' Shuti la Kavumbagu linadakwa kwa ustadi mkubwa na Aishi Manula

Erasto Nyoni anapewa kadi ya njano dk 24 kwa kumkwatua OkwiAzam wanawashambulia sana Yanga, Kipre anaisumbua sana ngome ya Yanga22' Shuti kali la Kipre linagonga Mwamba na kurudi ndani.

Azam wanapata bao lakini kabla ya mfungaji Kipre Tchetche alimfanyia madhambi Juma Abdul

20' Azam wanapata konba lakini inaokolewa na Yanga

18' Saimoni Msuva anakosa bao la wazi

Dakika ya 15, Young Africans 1 - 0 Azam FC

14' Goooooal Didier Kavumbagu anaipatia Yanga bao la kwanza baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Azam FC.

DK 12 Azam wanapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari, amefanyiwa madhambi Mcha Viali
5' Azam wanalishambulia lango la Yanga.

4' John Bocco amelala chin I baada ya kugongwa na kaseja wakti akitaka kuunganisha kona, lakini anainuka na kurudi uwanjani.

Azam wanapata kona baada ya Nadir kuurudisha mpira mkubwa kwa kipa wake.

2' krosi ya Gadiel Michael inadakwa na Juma Kaseja

Mpira umeanza uwanja wa taifa - Yanga 0 - 0 Azam

KIKOSI CHA YANGA

1. Juma Kaseja - 29
2. Juma Abdul - 12
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Kelvin Yondani - 5
6. Frank Domayo - 18
7. Saimon Msuva - 27
8. Hassan Dilunga - 26
9. Didier Kavumbagu - 7
10. Hamisi Kizza - 20
11. Emmanuel Okwi - 25
Subs:
1. Barthez, 2.Luhende, 3. Chuji, 4.Nizar, 5. Javu, 6. Tegete, 7. Ngasa


KIKOSI CHA AZAM FC
Aishi, Nyoni, Michael, Morad, Balou, Himid, Sure Boy, Bocco, Kipre Tchetche na Mcha

7 comments:

  1. Mwandishi mzuri anatakiwa kuwa fair sasa wewe line ya Yanga umeirembaaa halafu ya Azam unaandika kifupi kabisa huoni kama huo ni unazi

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa, mwandishi inabidi usioneshe mapenzi kwa team

    ReplyDelete
  3. Usimuhukum mwandishi tumfikirie vema kwani huenda hajapewa lineup ya Azam yenye namba ametumia uzoefu wake kuandika hiyo list

    ReplyDelete
  4. Atarekebisha baadae punguza hisia hasi

    ReplyDelete
  5. unacoment kwa jaziba ili iweje si bure utakuwa wa simba safi shafii dauda yanga oyeeee

    ReplyDelete
  6. wakati mwingine timu za Tanzania wachezaji wanakuwa hawana majina katika jezi zao fanya uchunguzi kwanza huenda amepata listi kwa njia hiyo nawewe usiulize kwa jazba no research no right speech friend.

    ReplyDelete
  7. wachezaji wa azam wana majina ktk jenzi zao mbona nalo hajalitumia wakati yanga hawana majina ktk jenzi lakini bado ameremba why?

    ReplyDelete