Search This Blog

Sunday, February 16, 2014

YAFICHUKA: SIMU YA DROGBA KWA GERVINHO ILIYOPELEKEA ABRAMOVICH KUMWAMBIA HAZARD ATAMPA MSHAHARA MARA 3 YA ALIOKUWA AKIPATA LILLE ILI AJE DARAJANI


Roman Abramovich mwenyewe binafsi aliongea na mchezaji wa zamani wa Lille Eden Hazar kumhaidi kumlipa mara 3 ya mshahara aliokuwa akilipwa na klabu ya Ufaransa kama angekubali kujiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011, imefahamika.

Mmiliki huyo wa Chelsea alizungumza na Hazard kwa njia ya simu wakati akiwa kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu ya Ufaransa - mbele ya wachezaji wenzake wa timu hiyo.

Boss wa Lille Rudi Garcia - ambaye alimfundisha Hazard wakati huo - alishuhudia kiteno hicho na ametoa siri hiyo kwenye kitabu chake kipya. 


Garcia anaelezea namna Didier Drogba alivyompigia simu Gervinho na kumuuliza kama Hazard - ambaye sasa amehamia Chelsea - yupo nae karibu. Gervinho akajibu: "Ndio, nipo nae hapa."
Hazard akachukua simu na Garcia anasema kwamba Drogba akampa simu Abramovich ambaye akamwambia Hazard: 'Sifahamu unalipwa kiasi gani hapo Lille, lakini nitakulipa mara 3 ya unavyolipwa ukihamia kwenye timu yangu."

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, ambaye alihamia Stamford Bridge kwa ada ya uhamisho wa £32million mnamo mwaka 2012, amekuwa kwenye fomu nzuri akiisadia Chelsea kushinda mechi muhimu na kuiweka timu hiyo ya Jose Mourinho katika kilele cha mbio za kugombea ubingwa. 

No comments:

Post a Comment