Search This Blog

Wednesday, February 26, 2014

REAL MADRID NA MKOSI NDANI YA ARDHI YA UJERUMANI - TANGU MWAKA 1979 IMESHINDA MARA 1 TU - HISTORIA KUENDELEA KUWAHUKUMU DHIDI YA SCHALKE?

Real Madrid CF wamekuwa wakitawala michuano ya ulaya kwa takribani miongo sita iliyopita, lakini kuna sehemu moja imekuwa ikiwapa shida sana: Ujerumani. Kipigo chao cha mabao 4-1 dhidi ya Borussia Dortmund msimu uliopita ilikuwa ni mara yao ya 25 na kipigo chao cha 18; wameweza kupata suluhu sita na ushindi mmoja tu - dhidi ya Bayern Leverkusen mnamo mwaka 2000. Angalia historia ya mechi zao walizocheza ndani ya ardhi ya Ujerumani. 

Hamburger SV 5-1 Real Madrid
1979/80 European Champion Clubs' Cup nusu fainali

Madrid walikuwa wameshaweka mguu moja kwenye fainali baada ya kuifunga Hamburger 2-0 Bernabeu katika mchezo wa kwanza. Lakini ndoto zao za kucheza fainali zikaenda kuisha na kipigo cha 5-1 ndani ya ardhi ya Ujerumani. 
1. FC Kaiserslautern 5-0 Real Madrid
1981/82 UEFA Cup robo fainali

Mwaka mmoja baada ya kuadhibiwa na Hamburger, Madrid wakaenda Ujerumani wakiwa wameshashinda 3-1 mchezo wa kwanza, lakini wakaenda kuangukia pua na kupigwa 5-0 na Kaiserslautern.
VfL Borussia Mönchengladbach 5-1 Real Madrid
1985/86 UEFA Cup raundi ya 3

Uwanja wa Mönchengladbach wa Bökelbergstadion ulikuwa mdogo kuweza kuhimili umati wa mashabiki uliokuwa ukitaka kuona mtanange huu, hivyo ikabidi mechi ipelekwe kwenye dimba la Dusseldorf – unaochukua mashabiki 65,000 ambao timu yao haikuwaangusha. Kikosi cha Jupp Heynckes kikaadhibu Madrid 5-1. 
Mchezo wa pili Madrid wakaenda kushinda 4-0 nyumbani na kufanikiwa kufuzu kwa faida ya goli la ugenini. 
FC Bayern München 4-1 Real Madrid
1999/2000 UEFA Champions League hatua ya pili ya makundi

Madrid walikuwa wakipewa nafasi kwenye mechi hiyo, lakini Bayern wakawashangaza mara mbili ndani ya siku 9 mnamo March 2000. Waliwapiga 4-2  Santiago Bernabéu na wakaenda nyumbani kwao wiki iliyofuatia na wakawaonyoosha 4-1. Kiwango cha Bayern msimu huo kiliendelea na kuepelekea kutwaa ubingwa msimu huo. 
FC Bayern München 2-1 Real Madrid
2000/01 UEFA Champions League nusu fainali

Miezi 12 baadae magwiji hawa soka ulaya wakakutana tena. Elber aliiwezesha timu yake kushinda 1-0 katika dimba la Bernabeu na goli lake la kichwa ndani ya dakika 8 za mwanzo za mchezo wa marudiano zikiweka Bayern mbele zaidi. Luis Figo akaisawazishia Madrid, lakini Mahmet Scholl akaongeza la pili na kuua ndoto za Madrid kabisa.. 
Borussia Dortmund 4-1 Real Madrid
2012/13 UEFA Champions League nusu fainali
Kipigo cha sita mfululizo kwa Madrid ndani ya ardhi ya Ujerumani kwa hakika kilikuwa kibaya zaidi baada ya Robert Lewandoski kuwanyoosha vijana wa Jose Mourinho, mshambuliaji huyo wa kipolish akawa mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne katika nusu fainali ya UEFA Champions League. Mechi ya marudiano Madrid wakashinda 2-0 mabao ya dakika za mwisho lakini ushindi huo haukotisha kuwapeleka fainali. 
Bayer 04 Leverkusen 2-3 Real Madrid
2000/01 UEFA Champions League hatua ya makundi. 

Majaribio ya Madrid kushinda ndani ya ardhi ya Ujerumani yalikuja kufanikiwa mnamo msimu wa 2000/01. Baada ya kujaribu mara 24 bila mafanikio hatimaye Los Blancos wakapata ushindi ndani ya Ujerumani ingawa ushindi huo ulikuwa kwenye mazingira magumu. Madrid walikuwa wakiongozwa kwamabao mawili ya Bernd Schneider na Michael Ballack, Roberto Carlos na Guti wakasawazisha, Carlos tena katika dakika 15 za mwisho akaifungia Madrid bao la ushindi. 
Leo hii takribani miaka 14 tangu washinde Ujerumani katika michuano ya UCL - Real Madrid wanakutana na Schalke - Je historia itaendelea kuwahukumu au wataandika mpya.

No comments:

Post a Comment