Search This Blog

Wednesday, February 26, 2014

PREVIEW: GALATASARY VS CHELSEA - MOURINHO DHIDI YA VINYAGO ALIVYOVICHONGA MWENYWE

Galatasaray AŞ walifungwa 5-0 wakati Chelsea FC walipokwenda Uturuki kwa mara ya mwisho, ingawa hivi sasa wana mtu anayeijua vizuri Chelsea Didier Drogba, mshindi wa UCL na Chelsea mwaka 2012. Gala chini ya kocha mpya Roberto Mancini watakuwa wakitumaini kulipiza kisasi.

Mechi zilizowakutanisha nyuma. • Tore André Flo aliipa Chelsea uongozi wa mabao mawili katika mchezo wa makundi baina ya timu hizi miaka 15 iliyopita akifunga kwenye kila lango ndani ya vipindi viwili. Mabao mengine kipindi cha pili yalifungwa na Gianfranco Zola na Dennis Wise pam naoja Gabriele Ambrosetti.
• Vikosi vilivyocheza kwenye mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Ali Sami Yen Spor Kompleksi mnamo 20 October 1999 vilikuwa:
Galatasaray: Mehmet Bölükbasi, Popescu, Emre Belözoğlu, Arif Erdem, Okan Buruk, Fatih Akyel (Ümit Davala 46), Hagi (Hasan Şaş 46), Tugay Kerimoğlu, Hakan Ünsal, Hakan Şükür (Saffet Akyüz 65), Capone.
Chelsea: De Goey, Ferrer, Leboeuf, Desailly, Le Saux, Deschamps (Wise 66), Morris, Poyet (Petrescu 66), Babayaro, Flo, Zola (Ambrosetti 75).
• Mchezo uliochezwa London mnamo 28 September 1999 uliisha kwa ushindi wa 1-0 kwa Chelsea bao la Dan Petrescu dakika 52. 
• Kipigo cha mabao 5-0 cha nyumbani kwa Galatasary kilikuwa cha pili katika michezo nane dhidi ya timu za EPL. Wakiwa wameshinda dhidi ya Liverpool katika michezo miwili katika hatua ya makundi msimu wa 2006/07 (3-2) na Manchester United FC (1-0) msimu uliopita - rekodi yao ya nyumbani W3 D3 L2. Yote dhidi ya timu za EPL W3 D7 L7. 
• Mnamo msimu wa 1999/2000 Galatasaray iliifunga Arsenal FC 4-1 kwenye hatua ya penati kwenye fainali ya UEFA Cup jijini Copenhagen ambayo iliisha bila kufungana kwenye muda zaida, ikiwa timu ya kwanza ya Uturuki kushinda mashindano hayo ya UEFA.
• Katika mchezo wao wa mwisho na klabu ya kutoka Uturuki, Chelsea walifungwa 2-1 na Fenerbahçe SK msimu wa katika robo fainali, lakini wakashinda 2-0 nyumbani na kusonga mbele. Pia walikutana na  Beşiktaş JK katika hatua ya makundi msimu wa 2003/04, walifungwa 2-0  Stamford Bridge lakini wakashinda 2-0 ugenini.

Habari za timu
David Luiz ana majeruhi ya paja na John Obi Mikel ana majeruhi lakini hajulikani na alikosa mchezo wa wikiendi iliyopita, Oscar ana tatizo la enka.

Aydın Yılmaz ana tatizo la enka na Gökhan Zan ana majeruhi ya misuli wote wamepona na watacheza leo. 

No comments:

Post a Comment