Search This Blog

Friday, February 14, 2014

NIONAVYO MIMI:SAKATA LA OKWI,MCHEZO UMEKWISHA


Na Oscar Oscar Jr .
0789-784858

Sakata la usajili wa mshambuliaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi hatimaye limefikia ukomo tarehe 13.02.2014 baada ya Shirikisho la soka Duniani FIFA kuthibitisha kuwa mchezaji huyo yuko huru kukipiga na mabingwa watetezi wa Tanzania bara klabu ya Dar es salaam Young Africans.

Rais wa Etoile Du Sahel,Ridha Charfeddie klabu ambayo mshambuliaji Emmanuel Okwi alikuwa akiitumikia baada ya kuondoka Simba sc kwa kitita kinachosemwa kufikia dola za kimarekani 300,000 ameibuka baada ya FIFA kuthibitisha kuwa Okwi ruksa kukipiga na wababe hao wa Jangwani na kudai kuwa,mchezaji huyo bado ni mali yao.

Ukichunguza vizuri utagundua kuwa,Rais huyo wa Etoile Du Sahel klabu yenye makazi yake nchini Tunisia,ameshastukia kuwa Okwi sio wao tena na deni wanalodaiwa na klabu ya Simba,kwao ni kama hasara.Kulipa dola 300,000 wakati mchezaji yuko zake mitaa ya Twiga na Jangwani,hiki ndicho kinachomfanya aweweseke!!

Lakini sakata la Okwi linatakiwa kuwa somo sana kwa viongozi wa vilabu Tanzania hasa Simba na Yanga.Hakukuwa na sababu kwa viongozi wa simba sc kujihusisha kwa aina yoyote ile na Usajili wa Okwi kwenda Yanga,wao nadhani wangejikita zaidi kuomba msaada wa kisheria toka TFF na FIFA ili kuhakikisha kwamba wanalipwa fedha zao za mauzo ya Okwi na klabu ya Etoile Du Sahel.

Mashabiki na wapenzi wa timu hizi za Kariakoo kuna kitu nawalaumu sana.Hivi kwa nini wanapenda kujua pesa za mauzo ya mchezaji zilikokwenda bila kujua pesa za kumleta mchezaji huyo klabuni zilitoka wapi? Nadhani ukiwa mwanachama unatakiwa kujua pesa za kuwaleta hao "MAPRO" zinatoka wapi,ukijua hilo,haitokusumbua wanapouzwa kujua pesa zinakokwenda.

Ni kweli mpira ni biashara na sina tatizo na klabu ya Simba kumuuza Okwi kwa kitita hicho cha dola laki tatu lakini,unawezaje kumuuza mchezaji wa aina ya Okwi kwa mkopo? Okwi alikuwa miongoni mwa wachezaji muhimu sana kwenye klabu ya Simba.Sikushangaa kuuzwa,nilishangaa kuuzwa bila timu kupokea hata senti moja!

Hivi ungewaelewa kweli klabu ya Tottenham Hotspurs endapo wangemuuza Gareth Bale kwenda Real Madrid kwa mkopo? ungewaelewa bodi ya Arsenal endapo wangemuuza Roben Van Persie kwenda Manchester united bila kupata chochote? kesho ukiamka na kusikia Eden Hazard kajiunga na klabu ya PSG bila Chelsea kupewa chochote,utawaelewa kweli?

Kuna baadhi ya watu wanaamini usajili wa Okwi bado unautata,binafsi siamini hilo.Utata wa Okwi ulimalizika pale FIFA ilipothibitisha uhalali wa Okwi kukipiga na mabingwa hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani,full stop.FIFA wanatambua mgogoro kati ya Simba na Etoile Du Sahel unaohusu malipo,FIFA wanatambua mgororo wa Okwi na Etoile Du Sahel unaohusu madai ya Okwi ya fedha zake na yale ya Klabu kuhusu utovu wa nidhamu wa Okwi na kukiuka mkataba wake,FIFA inatambua kujiunga kwa Okwi Sc Villa,FIFA inatambua kama Okwi kauzwa Yanga,FIFA inajua kama TFF wamemzuia Okwi kucheza VPL na pia wanatambua kama CAF imemzuia kucheza michuano ya klabu bingwa Afrika.Leo hii wameridhia Okwi kucheza Yanga,utata unatoka wapi?

Kama klabu ya Yanga itamtumia Okwi kwenye michezo yake ya ndani na ile ya Afrika halafu baadae ikagundulika kuwa Yanga wamemtumia mchezaji ambaye hakustahili na kupelekea kunyang'anywa pointi,hapo ndipo nitakapo amini kuwa shirikisho la soka Duniani,yaani FIFA linaongozwa na wahuni na sio watu wenye taaluma ya mchezo wa soka.i'm sorry!

10 comments:

  1. Mwandishi ukuzingatia weledi huwezi sema kosa la simba ni kujihusisha moja kwa moja ktk usajil wa okwi kwenda yanga,ww ulitaka wahusike wap!simba wanadai pesa yao kwa kumuuza nan sasa kama unataka wasihusike kuuzwa kwa okwi!unasema kuwa hakuna sbb ya simba kumuuza mchezaj tegemeo kama okwi ww unajua kwann walimuuzq!kama unakumbuku yanga walianza kumrubuni tangu awal so simba kupunguza kelele na ukizingatia ess wamefika bei ulitaka simba wafanyaje!kilichowaponza simba ni huruma yao kwa wachezaji wake walimsaidia okwi akapate maslah zaidi uko aenda sasa hayo mengine yametokea cos simba sio malaika wangejua kitawatokea nn mbeleni,hata ktk suala la kapombe kauzwa kwa mkopo kwa maslah yake na tanzania kwamba mchezaj afaidike kwanza timu ifaidike baadae,wangebaniwa mngeleta maneno ohoo tunawarudisha wachezaj nyuma cos tunawabania,suala la okwi simba lazima wahusike kwa kiasi kikubwa inafanana na baba aliyemuoza bint yake no matter kamuoza kwa kipande cha kanga au bure atakapoa achwa lazima baba ajue bint yake yupo wap na anafanya nn,sio mume na mume mwenzio wapeane bila baba kuhusishwa hiyo haikubaliki ndio sbb simba imehusika moja kwq moja kwenye sakata hilo huwezi sema simba wamejiingiza sio kwel wamejiingiza kwa sbb mchezaj anaanzia kwao wao simba.

    ReplyDelete
  2. We oscar jr. Naomba uwe unaedit kazi za shafii kabla hajaweka mtandaoni! Tumsamehe hajielewi!

    ReplyDelete
  3. nami nakuunga mkono kaka kwa hayo maneno uliyosema

    ReplyDelete
  4. Katika hili suala la Okwi bwana Shaffii inabidi uwe na uwezo wa kuchambua hoja si kukubali tu kwa sababu FIFA wameamua! Hizi transfer za Okwi zina utata na walakini ndani yake na hata hao wanofanya maamuzi na maamuzi kama haya siyatofautishi na mahakama ya kimataifa ya ICC ambayo wao upenda kuona viongozi waafrika ndio wenye makosa peke yao! Hili suala halina tofauti sana na sakata la mchezaji Janvier Besala Bokungu aliyevunja mkataba na Esperance ya Tunisia na kujiunga na TP Mazembe hali iliyopelekea TP kuondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Simba! Naamini kama suala kama hili lingetokea kwenye klabu za Ulaya FIFA wasingetoa maamuzi kama haya waliyotoa hapa Afrika...chunguza hili suala kwa makini angalia sheria za FIFA pia tafuta wanaojua sheria milijadili muone ukweli hupo wapi? Naamini hata TFF waliliona hili ndo maana wakasita kutoa ruhusa moja kwa moja...TAFAKARI!

    ReplyDelete
  5. mhh inabidi uongee hivo ukizungumzo tofauti na hivo utatukanwa kama alivoshambuliwa shafii

    ReplyDelete
  6. Labda hujui unachokisema, sitaki kubishana na mawazo yako, lakini unauliza eti Simba SC walimuuza Okwi kwa mkopo???

    Je unajua mchezaji anauzwaje kwa mkopo katika soka, je ndo walivyofanya Simba SC, au kwa kuwa Simba hawakupewa pesa hata kidogo basi we ndo unajua mkopo, mnarukia mambo tu hata msiyoyajua!

    ReplyDelete
  7. HUYU MUANDISHI NI WAZI YUPO KIUSHABIKI ZAIDI AU PENGINE ANAOGOPA KUITWA ADUI WA YANGA KAMA AITWAVYO SHAFFIH NA BIN ZUBEIRY.

    MUANDISHI INAONEKANA WAZI HII HABARI UMEIANDIKA KWA KUTUMIA MAWAZO YA WATU WA YANGA WALA SI MAWAZO YAKO.

    ReplyDelete
  8. Kwa mtazamo wangu suala la okwi limeumiza zana vichwa vya watz , naoni [1] cmba waendelee kudai pesa yao toka etoile du sahel ya tunisia sababu cmba wamefungua kesi ya madai ya pesa tu na sio mchezaji ,[2] na etoile du sahel ya tunisia wamefungua kesi ya utoro wa okwi , [3]na okwi amefungua kesi ya kutolipwa mshahara . kila mmoja afatilie kesi yake

    ReplyDelete
  9. Simba wafuatilie malipo yao ya mauzo ya Okwi tunisia,waache kujihusisha na uhamisho wa Okwi kwenda Yanga kwa kuwa huyu hakuwa mchezaji wao tena.Kumbuka kwamba Okwi alinzia kucheza Villa ya Uganda na baadae ndio akaenda Simba sc kabla ya kuzwa Etoile na baade kurudi Villa kabla ya kuuzwa Yanga.Hivyo kama ni suala la baba kumuoza binti yake,kati ya Villa na Simba sc nani anyehusika na Okwi zaidi?Na kumbuka kwamba Simba bado wanadaiwa na Villa asilimia 20 ya mauzo ya Okwi kwenda Etoile kwa sababu Villa ndio ilyomlea Okwi akiwa na umri chini ya miaka 18

    ReplyDelete