Search This Blog

Saturday, February 22, 2014

MSHAHARA WA WAYNE ROONEY KWENYE NAMBA - FEDHA ANAYOINGIZA KWA WIKI INAZIDI MSHAHARA WA MWAKA MZIMA WA BARACK OBAMA


Tuuchambue mshahara wa Wayne Rooney kwenye namba maalum:

£160,000 - Hii ndio fedha ambayo itabaki kwenye akaunti ya Rooney kwa wiki - baada ya kulipia kila kitu, kodi na bima. 
£30,000 - Wastani wa mshahara wa wiki kwa mchezaji wa ligi kuu ya England, hii ni kwa mujibu wa  Deloitte's sports business group.
£517 - Huu ni wastani wa mshahara wa wiki wa mtu anayefanya kazi ndani ya UK.  Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anapata £2,740 kila wiki. 
65 - Itamchukua wiki 65 kwa Barack Obama, raisi wa taifa kubwa duniani Marekani, kuweza kutengeneza kiasi anacholipwa Rooney ndani ya siku saba tu  - Obama analipwa £240,000 kwa mwaka.

1885 - Huu ulikuwa mwaka wa kwanza kwa mwanasoka kuweza kulipwa kutokana na kucheza soka. 

£4 - Hiki ndio kilikuwa kiwango cha juu kabisa cha malipo katika Football League mwaka 1901. 
60 - Namba ya miaka iliyotumika mpaka kufikia mwisho wa sheria ya kulipwa kiasi kisichozidi paundi 4 kwa mwanasoka. Sheria hii ilikufa mwaka 1961. Muda mfupi baada ya kufutwa kwa sheria hii, mchezaji wa Fulham na Engand  Johnny Haynes alikuwa mchezaji wa kwanza kulipwa kiasi cha  £100 kwa wiki.
£1,200 - Kiasi ambacho golikipa Peter Shilton alitengeneza kila wiki mwaka 1979 wakati alipoweka rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi Uingereza kwa kusaini mkataba mpya na Nottingham Forest.
£10,000 - Mchezaji wa kwanza kulipwa kiasi cha tarakimu 5 alikuwa Chris Sutton, wakati mshambuliaji huyo alipojiunga na  Blackburn Rovers akitokea Norwich City mnamo 1994.
£100,000 - Sol Campbell aliondoka Tottenham na kujiunga na Arsenal mnamo mwaka 2001, akasaini mkataba ambao ulimfanya kuwa muingereza wa kwanza kulipwa mshahara wenye tarakimu 6 kila wiki. 

2 comments:

  1. Ina maana Obama analipwa £5000 kwa wiki?

    ReplyDelete
  2. una taarifa tofauti sana na za kuvutia. you shouldnt have a blog, you should have "WEBSITE" like kandanda.com

    ReplyDelete