Search This Blog

Monday, February 24, 2014

MAPATO: MECHI ZA SIMBA NA YANGA ZAINGIZA MILLIONI 101



Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zilizohusisha timu za Yanga na Simba, na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki zimeingiza jumla ya sh. 101,165,000.

Yanga ambayo iibugiza Ruvu Shooting mabao 7-0 mechi yake iliingiza sh. 68,450,000 kutokana na washabiki 11,972 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Katika mechi hiyo kila klabu ilipata mgao wa sh. 15,687,488 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 10,441,525.42. Gharama za tiketi ni sh. 3,813,600 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata sh. 4,877,538.71. Uwanja sh. 8,129,231.19.

Gharama za mchezo zilikuwa sh. 4,877,538.71 wakati Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,438,769.36. Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata sh. 945,110.

Nayo mechi ya Simba na JKT Ruvu ilishuhudia na watazamaji 5,850 na kuingiza sh. 32,715,00 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 4,990,423.73.

Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 7,428,742 wakati tiketi ni sh. 2,542,400 huku gharama za mechi zikiwa 2,266,395.86. Uwanja ulipata sh. 3,777,326.44 wakati Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ni sh. 2,266,395.86.

Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulipata mgawo wa sh. 1,133,167.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 881,376.17.

RWIZA KUSIMAMIA MECHI YA TP MAZEMBE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza Kishongole kuwa Kamishna wa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya TP Mazembe na Asres De Douala ya Cameroon.

Mechi hiyo ya hatua ya 16 itafanyika kati ya Machi 7, 8 au 9 mwaka huu jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na kuchezeshwa na waamuzi kutoka Uganda.

Mwamuzi wa kati atakuwa Denis Batte wakati wasaidizi wake ni Mark Ssonko, Samuel Kayondo na Mashood Ssali.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

1 comment:

  1. Hv kwa nini waamuzi ktk bongo huishia kuwa makamisaa na si wa kati?

    ReplyDelete