Search This Blog

Monday, February 24, 2014

KUANGALIA MECHI YA TWIGA STARS, ZAMBIA BURE - CHAMAZI COMPLEX


Washabiki wa mpira wa miguu nchini watashuhudia bure mechi ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) dhidi ya Zambia (Shepolopolo).

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itachezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili alasiri.

Twiga Stars ambayo ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Lusaka, Februari 14 mwaka huu kwa mabao 2-1 iko kambini chini ya Kocha Rogasian Kaijage na msaidizi wake Nasra Juma ikijiwinda kuwakabili Wazambia wanaotarajiwa kutua nchini Alhamisi (Februari 26 mwaka huu).


Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis Iratunga kutoka Burundi kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa (Februari 26 mwaka huu). Kamishna Fran Hilton Smith kutoka Afrika Kusini yeye atatua nchini Februari 27 mwaka huu kwa ndege ya South Africa Airways.

No comments:

Post a Comment