Search This Blog

Wednesday, February 5, 2014

KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014, CHANGAMOTO, FURSA KWA BIDHAA KWA AJILI YA KUTANUA MASOKO NCHINI BRAZIL.



Mwaka 2014 umetawaliwa na tukio kubwa zaidi la kimichezo nalo ni kombe la dunia. Ni wakati wa makampuni yenye misuli mikubwa na hata washirika na wadhamini kujipanga kwa ajili ya kwenda sawa na kipyenga kitakachopulizwa rasmi jijini Sao Paulo nchini Brazil.
Chapa kama Adidas, Coca-Cola, Visa, Continental na McDonald zimewekeza paundi bilioni 5.5, kwa ajili tu ya kushiriki kupata haki ya kufanya biashara kwenye michuano hiyo, inayoandaliwa kila baada ya miaka minne na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA.  Ni wakati wa kujiuliza sasa ni zipi changamoto na fursa zitakazozikumba chapa hizi nchini Brazil?
Kombe la dunia ni nafasi kwa bidhaa mpya pia washirika wa kibiashara kupata nafasi ya kuwasiliana na asilimia 50 ya watu wote duniani, kwani mashabiki zaidi ya bilioni 4 watawasha televisheni zao kuangalia michuano hiyo, pia ulimwengu wa digitali pamoja na mitandao ya kijamii, hivyo ni nafasi kwa bidhaa kupata umaarufu ingawa kutakuwa na ushindani kwenye kupata nafasi.
Nani atawika? Hilo ni swali muhimu sana kwetu. Brazil ni nchi ambayo  itatawaliwa na rangi za kila aina kutoka kila kona ya dunia, pamoja na ushabiki uliotukuka wa mchezo wa soka nchini humo, na ni muda pia wa bidhaa kufikia malengo ya kibiashara kwa kuwa huo ni muda wa thamani.
Adidas kwenye ubora wametumia njia zote kukabiliana na wapinzani wao NIKE, ambayo ni bidhaa maarufu katika bara la Amerika kusini. Mnamo mwezi Disemba Adidas walizindua mpira maalum utakaotumika kwenye kombe la dunia uliopewa jina la BRAZUCA, ambapo kampuni hiyo kubwa kwa kuzalisha vifaa vya michezo yenye makazi yake nchini Ujerumani, ilifanya utafiti kwa kuwahoji wakazi zaidi ya milioni moja nchini Brazil, ili kufahamu namna walivyoupokea huo mpira, lakini pia kampuni hiyo ya Adidas iligawa mpira mmoja mmoja kwa kila mtoto aliyezaliwa ile siku ya uzinduzi. mmmhh mambo hayo!
Wanachi wa Brazil ni moja ya wateja lakini kwa upande mwingine watatumika kama njia ya kutangaza  bidhaa, na makampuni mengi yanategemea kufaidika na michuano hiyo kwa kuitumia  kama ngazi  kwa kuwa karibu na wananchi kupitia mitandao ya kijamii pia na biashara za kutembeza mitaani.
Mitandao ya kijamii ni njia nzuri na bora kwa mashabiki kufuatilia  michezo  kwa kubadilishana uzoefu kupitia Twitter, Facebook and YouTube.
Coca-Cola kama wadhamini wa michuano ya kombe la dunia, wameshaanza kutumia nafasi ya kufanyika kipindi cha kiangazi kwa kutumia ziara ya kombe la dunia wakijihusisha na mashabiki moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram jambo ambalo linamvuto kwa mashabiki wa soka.
Pamoja na kufanya mitandao ya kijamii ni vyema  kwa mameneja bidhaa kutumia fursa  kama ilivyokuwa kwa (Super Bowl 2013 ) na Adidas (2012 kwenye michuano ya Olympic ) kufanikisha kuwatumia walaji kama mabalozi kupitia idadi zao kwenye mitandao ya kijamii..
Walaji watakuwa  na uwezo wa kuangalia video kwa mahitaji ya Brazil, na kutokana na mazingira kumetoa fursa kwa technolojia kuweza kumsaidia mlaji kupata fursa ya kushuhudia matukio .
Wadhamini wengine wa Kombe la dunia la FIFA 2014 ni kampuni ya VISA, wameikuza technolojia yao ya digitali kwa walaji  kupitia bidhaa yao ‘Go World’ inayofanana na ile ya  kampeni  ya michuano ya Olympic 2012.
VISA ni maarufu kwenye mtandao wa YouTube, kwa maudhui maalum ya video zinazoonyesha maisha halisi ya watu,  pia mashindano ya mbio  kuendana na matakwa ya walaji. Sasa katika hili itasaidia sana kujenga imani ya watu  juu ya VISA.
Moja ya changamoto kwa bidhaa ni wananchi kukosa imani na bidhaa husika kutokana na umaarufu wao, kwenye kujikita katika tasnia ya michezo.  Changamoto ya kombe la dunia la Fifa  2014 kwa washirika wa kibiashara,  ni kutafuta  nafasi ya  kujikita  kwenye nyoyo za watu ili kupata nafasi ya kuzungumza  kutakakopelekea kupata uhuru wa kujitawala kibiashara kwa muda mrefu, na bidhaa kupata fursa mpaka siku ya fainali  

No comments:

Post a Comment