Search This Blog

Sunday, February 23, 2014

KAGERA SUGAR 1 v RHINO RANGERS 0, SELEMAN KIBUTA AITUNGUA RHINO AKITOKEA BENCHI!!

Timu zikisalimiana
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Kagera Sugar wakiikaribisha timu ya Rhino Ranger leo kutoka Tabora kwenye Ligi  kuu ya Vodacom (VPL) wameifunga bao 1-0. katika mchezo huo ulio pigwa hii leo jumamosi katika kipindi cha kwanza timu zote mbili zilienda mapumziko zikiwa 0-0. Kipindi cha pili Kagera Sugar walifanya mabadiliko kwa kumuingiza mchezaji wao Seleman Kibuta na katika dakika ya 52 kipindi hicho hicho cha pili mchezaji huyo aliwapachikia bao la pekee. Bao hilo limepatikana baada ya kupigwa frii kiki na Hussein Mohamed(Shabalala) na kugonga posti upande wa juu na hatimaye  Seleman Kibuta kuumalizia mpira huo ndani ya lango la Rhino Rangers.
Bao hilo limedumu mpaka dakika za mwisho wa kipute hicho na Kagera Sugar kumaliza mtanange huo na ushindi wa pointi tatu muhimu kwenye uwanja wao wa Nyumbani Kaitaba. Ushindi huu wa Kagera Sugar umewapandisha hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 26 huku Rhino Rangers wakiendelea kushika nafasi ya mwisho kwenye ligi hiyo wakiwa na pointi 13.
Picha ya waamuzi na timu kapteni wakiteta jambo muda mfupi kabla ya mtanange kuanza
Picha ya pamoja
Viongozi wa timu ya Rhino Rangers pamoja na wachezaji wa akiba
Sehemu ya Kagera Sugar, Viongozi na wachezaji wa akiba
Patashika kwenye lango la Kagera Sugar
Kimbiza kimbiza
Kocha wa timu ya Rhino Rangers Jumanne Charles akitoa maelekezo
Nivute nikuvute!!!
Mchezaji wa Rhino akiuchota mpira kutoka kwa mchezaji wa Kagera Sugar
Patashika kwenye lango la Kagera Sugar, Chupuchupu wafungwa ...Salum Kononi ameuondosha mpira uliopigwa kichwa kabla haujavuka mstari ndani ya lango.
Kanoni akimiliki mpira huku mchezaji wa Rhino akiwa amemnyemelea kwa nyuma!
Mchezaji wa Kagera Sugar akiwekwa chini...
katika kuwania mpira
Kagera Sugar wakifanya mabadiliko kipindi cha pili...
Seleman Kibuta akishangilia bao lake la pekee kwa timu yake Kagera Sugar katika kipindi cha pili dakika ya 52.
Kipa wa Rhino akiwapanga wachezaji wake wakati wa frii kiki iliyokuwa inaelekezwa kwenye lango lake.
Salum Kanoni akiwakimbiza Rhino Rangers
Kocha wa Kagera Sugar akiwapongeza wachezaji baada ya mpira kumalizika
Wametwibia bao bwana..
Wachezaji wa Rhino Rangers wakiwatuhumu waamuzi baada ya mpira kumalizika jioni hii.

No comments:

Post a Comment