Search This Blog

Sunday, February 16, 2014

AZAM FC YATOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO,YAFUNGWA MABAO 2-0 NA FERROVIARIO.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la shirikisho AZAM FC leo wametolewa kwenye mashindano hayo baada ya kufungwa mabao 2-0 na timu ya Ferroviario de Beira.
Azam imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kushinda bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa juma lililopita kwenye uwanja wa Chamazi.


1 comment:

  1. Inauma sana unapoona timu kama Azam ilyofanya uwekezaji mkubwa katika soka inaishia kwenye hatua hii ya mashindano haya ya pili kwa ukubwa katika ngazi ya klabu hapa Afrika.Baada ya kufanya mabadiliko ya mara kwa mara kwenye benchi la ufundi na pia kwa wachezaji,nafikiri umefika wakati sasa kwa Azam kujiangalia upande wa utawala kama inao watu sahihi wa kuongoza timu hiyo kwa kuzingatia malengo yake na uwekezaji inaoufanya.Sio vibaya sasa kama itaangalia kupata watendaji wenye utallamu na weledi zaidi ya ilionao sasa.Vinginevyo ijaribu kuangalia mfumo wao wa uendeshaji klabu hiyo kama bado unaleta tija kwa kuzingatia malengo ya klabu na uwekezaji uliopo.Kwa maoni yangu Azam sasa inabidi kubadilisha baadhi ya watendaji(menejimenti) na pia kujifunza kutoka kwenye vilabu vilivyopiga hatua kibiashara na kisoka kama kule south africa ,egypt,Tunisia n.k naamini watajifunza kitu na kuufanyia mabadiliko mfumo wa uendeshaji klabu.Kwa upande wabenchi la ufundi bado naamini Hall ndiyo mtu sahihi kwa Azam kwa miaka miwili zaidi ijayo

    ReplyDelete