Na BARAKA MBOLEMBOLE
Wakati ligi kuu ikianza, mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi, Mganda, Emmanuel Okwi amekuwa mmoja wa watazamaji mwenye thamani kubwa. Je, Yanga wameingia ' mkenge' katika usajili wake?. Hili linaweza kuwa swali ambalo majibu yake yapo wazi. Kwanza, Okwi ni mchezaji wa Etoile du Salehe ya Tunisia ambao walimnunua kutoka timu ya Simba.Kwa nini yupo Yanga?. Alikuwa akiichezea timu ya SC Villa ya kwao Uganda kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita akitokea Etoile. Narudia tena, alikuwa akiichezea Villa kwa mkopo. Fifa ilimruhusu Okwi kucheza Villa kwa muda wakati kesi tatu zinazomuhusu Mganda huyo zikitafutiwa mhuafaka. Okwi kwa upande wake anadai kuwa Watunisia hao walivunja mkataba kwa kushindwa kumlipa pesa zake kama ilivyotakiwa. Simba nao wanadai malipo yao kutoka kwa Etoile.
Okwi aliruhusiwa kuichezea Villa ili kulinda kiwango chake, na wala hakuwa mchezaji anayemilikiwa na timu hiyo. Alizuiwa kuichezea timu ya Taifa ya Uganda katika michuano inayoendelea ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, CHAN, kwa kuwa alikuwa Villa kwa mkopo kutoka timu ya ng'ambo. Ila, ni Villa ndiyo wanaosemekana kumuuza Okwi kwa timu ya Yanga. Kwa mamlaka gani?. Hadi hapa Yanga watakuwa wameliwa. Kwa kuwa Okwi ni mchezaji wa Etoile si Villa.
Yanga wamemsaini Okwi huku wakijiaminisha kuwa wapo sahihi. Wanaamini Okwi ni mchezaji huru au wa Villa. Ila, alitakiwa kucheza Villa kwa miezi sita, lakini akaitumikia miezi isiyozidi miwili tu na kununuliwa. Caf, Shirikisho la soka Afrika wamemuhidhinisha Okwi kuichezea Yanga. Kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji imemzuia matumizi yake hadi watakapopata ufafanuzi kutoka FIFA, Shirikisho la soka ulimwenguni.
Ndiyo, wapo sahihi kwa kuwa FIFA, ndiyo waliosema mchezaji huyo acheze Villa kwa miezi sita wakati kesi zake zikishughulikiwa.
FIFA, wanaweza kumruhusu Okwi kuchezea Yanga kwa maslai ya kipaji chake. Ila, wanaweza pia kumzuia endapo watajua kuwa mchezaji huyu amekiuka maagizo yao ya awali ambayo walimwambia acheze Villa. Inawezekana mchezaji huyo akaonekana tapeli, kwa kuwaadaa Yanga wakati akijua fika mkataba wake upo Etoile. Wapo wachezaji walioshinda vita kama hii ya Okwi, ila wapo pia walioingia katika vifungo vya FIFA.
Huenda Yanga wakamtumia Okwi siku za mbele, ila kwa sasa ni uhalali wa mchezaji huyo. Kama, Etoile wataendelea kushikilia msimamo wao kuwa hawajui mchezaji wao mahali alipo, Okwi ataoneka ni mtoro. Endapo, Okwi ataonekana ni halali madai yake anaweza kulipwa fidia na Etoile, ila kasheshe ni wapi ambapo Villa walipata kibali cha kumuuza Okwi kwa timu ya Yanga?
Kila upande udai una wanasheria wake. Duh!. Lakini mwanasheria wa Okwi anaweza kuwa mjanja zaidi, mwenye akili zaidi, kwa kuweza kupata saini na mamillioni ya Yanga kwa ufafanuzi wake wakati akimpigia debe mteja wake kuwa hana tatizo. Kama sheria iliwekwa ili ivunjwe, na kama mikataba siku zote inaweza kutenguliwa, Yanga watamtumia Okwi, ila tusije kushangaa FIFA, wakisema mchezaji huyo mali ya Etoile. Yanga walimnunua wapi Emmanuel Okwi? Labda hapa ndipo kuna hoja ya msingi.
Huu ni uandishi wa kimburula kupata kutokea hapa Tanzania,sina mengi lkn nina wasiwasi na uwezo wako wa kupambanua mabo,how unamuhukumu mtu hali ya kuwa hauja jua hatma yake,hakika unazi wenu ndio kifo cha soka letu.
ReplyDeleteetoile hawajapeleka jina la Okwi CAF, sijui kama ilo unalifahamu
ReplyDeleteKupelekwa jina Caf siyo tatizo linapokuja swala la nan mmiliki?hata Chuji jinalake halijaenda Caf haiimaanishi si mali ya Yanga.Etoo wamefafanua kuwa Okwi hayupo kwao(kakimbia ndoa)hawaoni msingi wa kupeleka jina lake Caf.kama chuji aligoma kukaa benchi jina lake likakatwa Caf iweje Okwi aliyekimbia Tunis kwa miezi sita sasa jina lake liwepo?THINK BIG!
Deletewewe ndi mbulula kweli, kama Chuji jina lake halijaenda CAF kwanini waende nae Comoro, usiongee kwa kusoma magazeti ya udaku
DeleteSometimes nahisi huna jambo la kuandika, kipindi chenu cha sports extra kimejaa majungu kila siku mnamuongelea Okwi, mara yanga wameliwa mara ivi. Hivi michezo Tanzania its all about Okwi na Yanga. Wkt wa Maximo mlikuwa wa kwanza kuongea majungu, alipoondoka mkabadilika tena Oooh maximo alikuwa mzuri. Nyinyi wanafiki sana, kila kitu nyinyi ndo mnajua. Smtmz its gud kuwa msikiluzaj kuliko kuwa upande mmoja.
ReplyDelete..sasa mkuu hujajiuliza maswali muhimu..au umesahau...Jiulize CAF walipitishaje jina lake Yanga..system ya Caf ilionyesha status ya Okwi ni Ipi...Nani kaweka pingamizi kuzuia usajili wa Yanga..kwanini TFF wamempitisha..maana hawajatengua usajili ila wanajiridhisha...:
ReplyDeleteJamani tuheshimu mawazo ya kila mmoja, wengine wangependa kusikia kuwa yanga wanastahili kumutumia OKWI. wengine wanataka tuseme hakuna tatizo. km hakuna kwa nini TFF wamemzuia kucheza yanga? kwa nini CAF walimiidhinisha kuichezea yanga? kwa nini FIFA walimruhusu kucheza villa kwa muda maalumu? hapa kuna tatizo. Kama villa walimuuza mbona simba haikulipwa mgao wa mauzo kwa mjibu wa mikataba ya FIFA na simba na Etoile.
ReplyDeleteKwa uelewa wangu mdogo wa sheria ya mikataba km simba hawakulipwa yaani consideration the contract is void. nanukuu " any contract without consideration is void" je km ni void na mwenye mamlaka kumuuza OKWI? simba au Villa? km mkataba wa simba na etoile ulikosa nguvu za kisheria basi kwa kutotimiza matakwa mhimu ya mkataba mwenye OKWI narudi kuwa mchezaji wa simba na ndiyo wenye mamlaka ya kumuuza km FIFA itasema mkataba na etoile ilikufa. kwa kutumia sheria ya mikataba ya kimataifa e.g -(1) An agreement made without consideration is void unless–
(a) it is expressed in writing and registered under the law for the time
being in force for the registration of documents, and is made on
account of natural love and affection between parties standing in a
near relation to each other;
(b) it is a promise to compensate, wholly or in part, a person who has
already voluntarily done something for the promisor, or something
which the promisor was legally compellable to do; or
(c) it is a promise, made in writing and signed by the person to be
charged therewith, or by his agent generally or specially
authorised in that behalf, to pay wholly or in part a debt of which
the creditor might have enforced payment but for the law for the
limitation of suits.
hapo umechanganya madesa, kuna mikataba zaidi ya mmoja na wewe unalazimisha mkataba uwe mmoja. Kuna mkataba kati ya Simba na Etoile pia kuna Mkataba kati ya Okwi na Etoile, mkataba ambao FIFA imeuvunja kwa kukiuka makubaliano ni kati ya Okwi na Etoile ambao haumfanyi Okwi kurudi Simba maana hayo ni maamuzi binafsi bali unamfanya kuwa huru " free agent" na mkataba wa Simba na Etoile uko palepale. Simba hawatakiwi kudai asilimia ya mauzo kwa kuwa Etoile hawakumuuza Okwi bali ameondoka kama "free agent" na hata yanga wamemchukua kutoka villa kama free agent! fuatilieni vitu kabla ya kuandika
DeleteHaipendezi kumshamhulia muandishi au mtu kwa kile alichosema kwani kila mmoja ana haki ya kusema kile aonacho na kama kuna hoja au maelekezo tuelekezane vema muandishi hachezi soka wala waandishi hawauwi soka soka inauwawa na watu kama vionhozi wa yanga ambao wao haja yao ni kushindana kukomoana na kupindisha sheria kwa ubabe wao hili mbona halisemwi.yanga wa ekuwa na vurugu kila wakati wa usajili na wamekua wanafanya mambo yasio uungwana mengi na hata kuna wakati inatumika nguvu ya ziada hili halisemwi ila anatazamwa muandishi alieandika ukweli kuhusu okwy haipendezi nawakumbusha tu kuwa hao hao yanga kupitia bin kleb waoalowaho kutamka kuwa swala la okwy ni gumu na wana yanga wasahau kumpta okwy lakini ni hao hao waliokula matapishi na kuonekana leo wako sahihi
ReplyDeleteHata yanga hawajapeleka jina chuji je ww unalifaham na chuji ni mchezaji wa yanga kasmamishwa kwa utovu wa nizam
ReplyDeleteHivi kama kesi itaamuliwa na FIFA,hawa wapiga ramli wanatoka wapi?si tusubiri huo uamuzi wa FIFA kama kweli TFF imelipeleka huko.Kimsingi kama mfumo wa TMS ultumika kukamilisha uhamisho huu,ni wazi kwamba unakuwa monitored FIFA na hivyo taarifa zote za Okwi za kabla ya uhamisho zingejitokeza,hususan klabu yake inayomuuza,chama cha soka kinachostahili kutoa ITC n.k.
ReplyDeleteMbolembole Unajishushia hadhi kwa uandishi unaosukumwa na mapenzi yako. Jinsi ulivyoandika suala la Okwi ni wazi unajaribu kueleza kitu unachotamani kitokee. lakini suala la okwi halipo straight kama unavyolielezea nani alikwambia okwi aliidhinishwa kucheza kwa mkopo Villa? FIFA walimruhusu Okwi kucheza kwa kulinda kipajia chake walimuamuru acheze VILLA tu? kwa nini FIFA iliruhusu ITC ya okwi kwenda yanga? kuna maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kutoa majibu mepesi kama ulivyofanya.
ReplyDeletehongereni YANGA
ReplyDeleteWewe umesimuliwa tu unaesema jina halijapelekwa caf so yanga choo cha kike
ReplyDeleteWewe uliyeandika mada hii mara nyingin nataka comment but then naona ni upuuzi kufanya hivyo. Mara kwa mara una base on one side story...a good journalist mara nyingi anaongelee sehemu mbili kabla ya make any conclusion, by the way ulichoandika ni personal opinion yako so you have right to do that...but don't let the reader to believe that your artilce yako ni right, no, not at all. Nadhani nyinyi watu ndio mnaolimaliza soccer la Tanzania, mnaogopa kuongea ukweli mnaongelea ushabiki tu. Wewe na shaff nyinyi wote ni Simba nadhani mkiweka ushabiki pembeni mtalisaidia sana soccer la bongo, haya ni mawazo yangu.
ReplyDeleteMdau
Washington DC
Hongera ndugu kwa uandishi wako wa kina na kwa kuchanganua mambo hata mtoto mdogo au chizi anaweza kufanya ujinga kama Yanga waliofanya ila tatizo la viongozi wao ni elimu ndogo na ujinga wa kuikomoa Simba.
ReplyDeleteInaonekana haujui unachokiandika kaka, kuma haujui kitu ni bora kukaa kimya co lazima kuandika! Huu c uchambuzi bali ni ushabiki, na waandishi kama nyie ndio mmetufikisha hapa tulipo
ReplyDeleteSio lazima uandike article ili upate ukurasa ktk gazeti kaka. Ukikosa habari kausha jipange tena safari ijayo kwani unauliza maswali ya kitoto sana aisee ilkhali majibu unayo.
ReplyDeleteUkiwa mwanahabari na muandishi mzuri usiwe mvivu na mzembe wa kukusanya taarifa na si kutuletea vihabari vya kuunga unga toka kwenye magazeti pendwa.
Jipange na acha unazi/ushabiki ukiwa kama mwandishi bali pambana na pekenyua habari ili uje utujuze na kutushibisha vitu vya maana nasi vya kuungaunga kama hivi.
Uganda ni karibu sana ungeenda na kukutana na wahusika wangekupatia habari nzuri na unge-balance na huku ningekuona wewe ni mkali sana.
Jipange sana bro unajishushia heshima yako na tasnia nzima ya uandishi wa habari.
Jina la Okwi mpaka sasa Lipo na jezi namba 25 na Yupo kwa mashindano yote Etoile na kwenye soko wanamuuza Okwi pounds laki 125 sasa yanga wamemnunua villa dola elfu 20 eti mchezaji sio na alizuiwa kucheza CHAN yeye na Walusimbi hapa kuna uhuni ulifanywa na Saad Kawembo kushirikiana na villa na baadhi ya watu FUFA na yanga hao yanga walizoea kamati ya mgongolwa sasa hayupo
ReplyDeleteHawajapeleka jina CAF sababu hawajui alinlk ila ni mchezaji wao
ReplyDeleteYanga tatizo lao ni kukurupuka hawana lolote kazi kuangalia simba wanamchezaji gani mzuri tumchukue bila ya kukaa na kutafakari kwa umakini okwi ni mchezaji halali wa et. De sahel.
ReplyDeleteNILISHAWAAMBIA, HUYO SHAFFIH HAFAI KUWA MWANDISHI, HANA MAADILI HAYO. AGOMBEE NAFASI YA UONGOZI MSIMBAZI.
ReplyDeleteANATIA AIBU SAAAAANA NA KUISHUSHIA HADHI CLOUD.
Siyo kila mchezaji anayesajiliwa na timu lazima ajumuishwe kwenye kikosi cha timu hiyo kitakacho shiriki michuano ya vilabu balani Afrika.Vilabu makini huwa vinaacha nafasi za ziada ili zipate fursa yakuboresha vikosi vyao pale vinapopata nafasi ya kosonga mbele kwenye mashindano husika,hivyo kitendo cha etoile du sahel kutomjumuisha okwi kwenye usajili wa caf,haimaanishi kuwa okwi si mchezaji wao.Zaidi sana ninalionazigo likiiangukia yanga iwapo du sahel wakishikilia msimamo kuwa mchezaji wao alikuwa anarubuniwa na vilabu vingine na ndiyo maana hakuwa comitted kwa mwajili wake(etoile).Sheria za usajili zinazuia club kufanya mazungumzo ya usajili na mchezaji ambae mkataba wake ni zaidi ya miezi 6.Yanga walizungumza na wamiliki wa mchezaji ambao ni du sahel? Kwa nini itc ya okwi ilishughulikiwa na fufa badala ya chama cha soka cha tunisia ambacho etoile inayommiliki okwi ni mwanachama wao?Nawapongeza tff kwa kuling'amua hili mapema vinginevyo wangeingia kwenye matatizo ambayo fufa watakumbana nayo kwa kuidhinisha kuuzwa kwa mchezaji ambaye hakuwa chini ya mamlaka yao.
ReplyDeleteNadhani kutokupeleka jina CAF sio tatizo. Mbona Chelsea hawakupeleka jina la Essien UEFA na nimchezaji wao? CAF pia kitoa kibali sio solution ya tatizo au uhakika kua Okwi ana haki kuhamia Yanga. Hata mazembe walipewa Kibali na hao CAF na Simba walipokata rufaa waliwageuka na kuwaondoa kwenye mashindano. Nadhani pamoja na Kua TFF wamechelewa kuleta hii issue mezani ila wanaweza kua wamewasaidia Yanga. Wachezaji wengi hasa wa Uganda wanajua viongozi wa Vilabu vya TZ ni mambulula so wanajipigia hela tu. Kama kweli Okwi alipewa provisional license tu kutakua na shida. Ila pia baada ya kusoma habari mbili za mbombela kama cjakosea jina lake ni dhahiri anaandika Kinazi sana. Kwenye issue kama hizi tuache unazi tuandike mambo ya msingi kuwajenga vijana wetu. Mpira Tanzania umekua na unafiki sana kwa sababu ya unazi wa club. Kwa haki kabisa Ngasa angefungiwa mwaka huu ila ni mapenzi ya watu tu wanamtoa mchezaji kwenye club iliyomsajili kihalali anaambiwa awalipe. We need to set discipline ili tiendelee.
ReplyDeleteShaff wewe ni mtu wa analysis sana za soka cjui unachukuliaje mechi za Yanga kuwa na mapato makubwa kuliko timu zote za ligi kuu. Nchi za watu unaosemaga wameendelea hiyo ni spcial case. Lkn ikitokea Yanga wanademand kitu flan au wamekosea bcoz of tht mnakuwa wakwanza kukoment kama vile nyinyi ni wajuz sana wa uchambuzi. Jitahidin kuwa fair. Tangazo la simba kumpiga 5 yanga kwenye sports bar mmeliweka mwaka mzima. Ndo kianzio cha kipindi chenu.
ReplyDeleteNyie wote mliokoment hapo juu ni mbulula kweli kweli. Kwani mwandishi amekosea nini au ndio nyie mliosomea chini ya mti...?
ReplyDeleteKwan yanga mtapeleka majina ya wachezaji wenu wote? Unaambiwa mtoro watapeleka jina lake wazibe nafac za wasio watoro? 3:25 jibu swali mmemnunua wap? Wkt alkuwa villa kwa mkopo wa miez 6?
ReplyDeleteKutopeleka jina CAF haina maana sio mchezaji wao, Ni mipango ya timu kuangalia umuhimu wa mchezaji katika mashindano husika, labda wangelitoa kwenye ligi ya ndan hapo ingekuwa issue nyingine. Tukubali ukweli kwenye usajili wa Okwi kwenda yanga kuna utata, tuwe wavumilivu tuone waliompeleka kwa mkopo villa watasema mini?
ReplyDeleteKwani yanga wamelipeleka jina la chuji au si mchezaji wao?
ReplyDeleteAchana na huyu mtu hana facts zozote yani kwa sababu anaandika bure basi ameandika tu, halafu Shaffih makala kama hizi tupa kapuni hajatupa kipengele chochote cha FIFA kinachomfunga Okwi mara anasema Okwi alikwenda Villa kwa mkopo kutoka Etoile mara anasema alikwenda kwa kibali maalum kutoka FIFA sasa anaeleweka huyu mtu? Okwi asingeweza chezea CHAN hata kama Villa wangekua wamemnunua Okwi sababu kuna kipengele cha CAF kinachomtaka mchezaji awe amecheza nyumbani kwa kipindi kisichopungua miezi sita na wewe mwenyewe unasema Okwi amecheza Villa miezi miwili tu, haya mambo muwe mnawadanganya watu huko vijiweni.
ReplyDeleteLet's wait for the FIFA decision, do not make the premature judgement
ReplyDeleteMtahangaika bure tusubiri uamuzi.yaani hapa kila mtu ni mtaalam hiv nani anayefahamu ukweli?
ReplyDeleteNchi hii ina watu WA ajabu Sana!!!! Yani mtu akiwa na mawazo yanayotofautiana nawewe ndo anakua Mburula? Nadhan tatizo hapa ni usimba na uyanga! Ndo maana watu hawachangii hoja objectively Bali kumponda mtu utaona wasi kua hapa ni ubishani wa mashabiki wa simba na yanga...nanyie ndo mnaua soka la tz sio kingine.....mwandishi anaweza asiwe sahihi yes bas mkosoe kwa hoja sio matusi...alaf nyie mnaomsema Shaffih kwani yeye ndo kaandika hii makala? Hata hamjasoma vizuri mnaanza kumhukumu mtu hiyo Ni akili ndogo na mawazo mgando..Nivizuri tukajenga utamaduni wa kuheshim mawazo na mitizamo ambayo Ni tofauti na yetu tusiangalie Kila kitu kwa jicho la usimba na uyanga. Hata angeandika vile ambavo mbadhani Ni sahihi kua Okwi ni Mali ya Yanga bado watu wa simba ambao hawaamini hivyo wangemtukana pia..msipende kuwasikia tu wale wanaowsifu vinginevyo muwe mnasoma tu magazeti yenu ya Yanga Imara na lile la simba na if possible fungueni redio zenu muwe mnajisifia Kila siku.....Stupid!
ReplyDeleteHebu acheni usimba na uyanga wenu kitu kipo wazi kabisa okwi ni mtoro kazini na huyo BIN KELBU ni tapeli mkubwa hapo tatizo ni 10% tu hata huyo MAHARAGE nae kisha chukuwa10% yake tusipoze nguvu kwa swala hili lipo wazi yanga wameliwa
ReplyDeleteWabongo bwana, tunajua sana. Unakuta mtu yupo kijiweni anaelezea jambo kama vile movie lkn ukichunguza yy alisikia mjinga mwenzake akihadithia na yy akabeba kama vile anajua kila kitu. Mbolembole amejaribu kuandika anachodhani yy ni sahihi, so hakuna haja ya matusi na kuleta usimba na uyanga. Ni mawazo yke, tusuburi toka FIFA kwan wte hatujui mikataba ilikuwaje na hawa viongozi wabovu kama kina rage na kleb ndo wanaharibu soka letu. Tuzalishe kina Samata wengi.
ReplyDeleteDa! Nathan ujumbe umefika ila naomba tuwe tunabishana kwa hoja..mwandishi katoa kile anachokifahau..sa yule anayeona Yanga wako sahihi kua na Okwi aandike makala yake atupe vigezo vyake (fact)...cio naye atoe habari za mitaani hapana afanye uchunguzi wa kinaa atujuze...na yule anayesema Okwi ci mali ya Yanga afanye da same......sio ku2kanana...humu nakukashifianaa hapana 2bishane kwa hoja ili 2pate ukweli wa awali maana ukweli haliz upo fifa...
ReplyDeletehii makala haijaandikwa na Shaffih, cha kushangaza watu wanamuongelea yeye badala ya kutoa mjadala chanya..
ReplyDeleteOkwi RUKSA Yanga, wale VILAZA mliocomment hapo juu mmeliwa...........kamfolomondo nyie
ReplyDeleteuandishi umevamiwa nimemsikia Leo anawasemea fifa
ReplyDeletehay a mambo ya kisheria tuweke ushabiki kando,nimemsikia ndugu Yang Leo kawa msemaji wa fifa kwenye sports extra.
ReplyDeletewatu wanaongelea ushabiki badala ya hali halisi, jana nimemsikia mtu kwenye sports extra anasema " contractual obligations ni mkanganyiko wa mkataba" nikacheka sana!
ReplyDeleteunajua watu wanapenda kuchambua mambo mapema ili mwisho wa siku ajisifie kwamba "mi ndo wa kwanza kusema"bila kuwa na details za kutosha kwa kile anachokielezea. hili swala la Okwi, naamini mwandishi wa makala hii hajaona mkataba uliopo kati ya SC Villa na Etoile. huwezi ukakurupuka kusema kwamba Villa wamepata wapi jeuri ya kumuuza.
ReplyDeleteShirikisho la soka la Uganda nao ni watu makini pia. wasingeweza kutoa ITC ya okwi wakati wanajua Villa haina uwezo wa kumuuza okwi.
Ni vizuri waandishi wetu kutokuchambua kitu usichokijua kuliko kujidhalilisha. haya sasa FIFA nao wana makosa kusema kwamba kama taratibu zilifuatwa okwi acheze? mi naamini CAF, FIFA, Shirikisho la soka Uganda na TFF kuna watu makini sana na ndiyo maana usahjili wa Okwi ulipita.
ukikosa cha kuandika bora usiongee