UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA), unatarajiwa kufanyika Februari 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati ya
Utendaji ya TASWA kilichofanyika Dar es Salaam jana kujadili masuala
mbalimbali ya chama na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla.
Kikao kilikubaliana kuwa uchaguzi ufanyike kwa
katiba ya zamani, kwani mchakato wa katiba mpya unaweza kuchukua muda mrefu,
hivyo kusababisha viongozi waliopo madarakani kuendelea kukalia viti kinyume
cha katiba, jambo ambalo si sahihi.
Kutokana na hali hiyo viongozi wapya
watakaochaguliwa moja ya kazi yao kubwa itakuwa kuifanyia marekebisho makubwa
katiba ya chama ili iende na wakati.
BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA AMIR MHANDO KATIBU MKUU WA TASWA.
No comments:
Post a Comment