Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mtangazaji
wa michezo wa Radio Abood, Sultan Sikilo kilichotokea jana alfajiri (Januari 11
mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Sikilo
ambaye pia aliwahi kufanyia kazi Radio Times na Radio Kheri na hadi umauti
unamkuta alikuwa Mweka Hazina Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa habari za
Michezo Tanzania (TASWA) amezikwa jana jioni katika makaburi ya Kibada,
Kigamboni.
Msiba
huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati
tofauti Sikilo alifanya kazi na TFF kwa kuripoti shughuli zetu nyingi za mpira
wa miguu, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Sikilo, Radio Abood na TASWA na kuwataka
kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Pia
TFF imetoa ubani wa sh. 100,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
No comments:
Post a Comment