Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amezindua programu ya kutoa elimu ya kupambana na matumizi
ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru.
Programu
hiyo iliyozimduliwa jana (Januari 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam iko chini
ya taasisi ya Africa Inside Out inayoongozwa na Rebecca Young wakati washirika
(partners) ni TFF na kampuni ya Rhino Resources ya Marekani.
Rais
Malinzi amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamekuwa yakiongezeka, hivyo
kuwa kikwazo kwa maendeleo ya vijana ambapo ameipongeza Africa Inside Out kwa
programu hiyo kwa vile itazuia vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa
hizo.
“Moja
athari kubwa za matumizi ya dawa za kulevya ni kupata maambukizi ya virusi vya
Ukimwi kutokana na kuchangia sindano za kujidunga dawa hizo.
“TFF
tutatoa ushirikiano wa kutosha katika programu hii. Lakini pia tutaingiza Ishi
Huru katika programu zetu za mpira wa miguu kwa vijana. Tutahamasisha jamii
katika kupambana na dawa za kulevya,” amesema.
Katika
uzinduzi huo, pia Rais Malinzi alizundua semina ya waelimishaji na kuwaeleza
kuwa wamepata fursa hiyo kwa vile ni vijana wanaojituma, hivyo watafikisha
vizuri ujumbe wa Ishi Huru katika shule na vituo vya vijana nchini.
CAPTION: Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza kwenye
uzinduzi wa programu ya Ishi Huru jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment