Search This Blog

Monday, January 13, 2014

NA MSHINDI NI..............CRISTIANO RONALDO!,RONALDO NDIYE MSHINDI WA TUZO YA BALLON D'ORNa mshindi ni …. Cristiano Ronaldo. Usiku wa leo jijini Zurich, FIFA itamtangaza nyota huyo raia wa Ureno kuwa mwanasoka bora wa dunia kwa mwaka 2013 ambayo itakuwa tuzo yake ya pili.
Cristiano Ronaldo amepata kura nyingi zaidi ya wapinzani wake Franck Ribéry na Leo Messi, kwa kushinda tuzo hiyo Ronaldo atakuwa ameusitisha ufalme wa Messi aliyekuwa ameishinda tuzo hiyo kwa miaka 4 mfululizo.
Chachu ya ushindi huo wa Ronaldo ni mabao 69 aliyofunga mwaka 2013, ikiwa ni pamoja na kuumaliza mwaka vizuri.
Ronaldo mwenyewe anajua kuwa ni mshindi tangu juma lililopita baada ya kudhibitisha kushiriki kwenye sherehe za tuzo hizo, pamoja na kushiriki Ronaldo amewapa mialika ndugu na rafiki zake wa karibu,mpenzi wake mwanamitindo Irina Shayak wakala wake Jorge Mendes.
Pia wapo viongozi mbali mbali wa Real Madrid akiwepo raisi Florentino Pérez, Emilio Butragueño, Zinedine Zidane na Sergio Ramos, ambaye atatangazwa kuwa beki bora wa kati sambamba na Mbrazil Thiago Silva.

2 comments:

  1. namkubali sana CR7. Aifanya na anaendelea kufanya mambo makubwa sana, lakini najiuliza ni vigezo vipi walitumia kumpa hii tuzo na kumuacha Frank Ribbery. Nikiweka pembeni mapenzi binafsi niliyonayo kwa ronaldo naona ribbery alistahili kuchukua tuzo. Mwenye kujua ni kwa nini kapewa cr7 na sio ribbery naomba anielimishe kidogo........ .......

    ReplyDelete