Search This Blog

Thursday, January 2, 2014

JE KIPIGO CHA JANA CHA MAN UTD NI ISHARA TOSHA YA KUTOKUWA NA UBAVU WA KUTETEA UBINGWA WAO ?

Hapo jana Manchester Utd ilifungwa nyumbani mabao 2-1 na Totenham Hotspurs,kipigo ambacho kilikuwa ni cha pili mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani toka kwa Spurs.
Kipigo cha jana kwa Man Utd kilikuwa cha kwanza kwa bingwa mtetezi tangia mwaka 1989 kupoteza mchezo siku ya mwaka mpya na pia ilikuwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986 Manchester Utd kufungwa michezo minne kwenye uwanja wa Old Trafford kufikia siku ya mwaka mpya .
Siyo tu jana takwimu zilikuwa mbaya kwa  Man Utd tu pia ilikuwa ni mara ya kwanza kushuhudia timu zote zinazoshika nafasi nne za juu kuibuka na ushindi siku ya tarehe 1 january.
Baada ya kipigo cha jana,Man United sasa ipo nyuma kwa tofauti ya pointi 11 na vinara Arsenal na pointi 5 nyuma ya nafasi ya kufuzu Uefa Champions League.

Msimu mzima uliopita ambao Man Utd waliibuka mabingwa kwa kukusanya jumla ya pointi 89 walipoteza jumla ya pointi 25 tu,lakini mpaka kufika nusu ya msimu huu tayari wameshapoteza jumla ya pointi 26 hii inamaana wakishinda michezo yao yote iliyosalia watafikisha jumla ya pointi 88 tu.

Kibaya zaidi Manchester UTD haijawa na matokeo mazuri dhidi ya timu zilizo juu yake kwenye msimamo wa ligi kuu ya England, ukiangalia Msimamo uliotengenezwa kutokana na matokeo baina ya timu zinazoshika nafasi nane za juu utaona Manchester Utd inashika mkia ikimaanisha kutopata matokeo dhidi ya timu zinazoonekana kuwa bora msimu huu.

JE HII NI ISHARA TOSHA YA KWAMBA MAN UTD HAWANA UBAVU WA KUTETEA UBINGWA WAO ?

2 comments:

  1. mm naona wanaweza wakachukua ubingwa wamuombe fargason awasaidie bila hivo wapiganie wapate nafasi ya 4

    ReplyDelete