Search This Blog

Friday, January 3, 2014

HIGHLITES : AZAM FC ILIPOIFUNGA SPICE STARS MABAO 2 -0 KWENYE MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI.


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

MABINGWA watetezi mara mbili mfululizo wa kombe la Mapinduzi, Azam fc wameanza vyema michuano hiyo baada ya kuifunga Spice Stars mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi C jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mabao ya Azam fc yamefungwa katika dakika ya 71 kupitia kwa Mshambuliaji Mganda, Brian Umony kufuatia kuwatoka mabeki wa Spice  na kupiga mpira uliomshinda mlinda mlango, Mohamed Silima.

Pasi ya bao hilo litoka kwa kiungo mahiri wa Azam fc Salum Abubakar ‘Sure Bo”.
Bao la pili lilifungwana na Himid dakika ya 86 kwa shuti kali, baada ya kuuwahi mpira uliokuwa unaelekea mikononi mwa kipa Silima kufuatia shuti la Salum Abubakar.

Afisa habari wa Azam fc ameuambia mtandao huu kuwa  mchezo ulikuwa mgumu sana kwani wapinzani wao wameonekana kuwa imara.

“Tumeanza vizuri kwa ushindi, lakini inaonekana michuano ya mwaka huu ni migumu sana. Spice wameonesha upinzani  mkubwa sana kwetu, lakini hatuwezi kusema lolote kwani ni mapema sana”. Alisema Jafar.

Jafar aliongeza kuwa kocha wao Mcameroon, Joseph Marius Omog anakisuka kikosi chao, hivyo makosa yanayotokea yatafanyiwa  marekebisho na kuhakikisha wanatwaa ubingwa wao.

Aidha, Jafar kwa niaba ya viongozi wa Azam fc amewapongeza vijana wao kwa kujituma na kupata ushindi ambao haukuwa rahisi kabisa.

Kwa ushindi huo, Azam inaongoza Kundi C kwa pointi zake tatu, na kubaki au kushuka itategemea na matokeo ya mchezo wa pili usiku wa leo  leo Uwanja wa Amaan kati ya Ashanti United ya Dar es Salaam na Tusker FC ya Kenya.

Kueleka katika mchezo huo, wauza mitumba wa Ilala wamesema wapo tayari kuwamaliza wakenya.

Marijani rajab, afisa habari wa Ashanti ameuambia mtandao huu kuwa kocha mkuu wa kikosi chao, Abdalaah Kibaden Mputa amewapanga vijana wake kutokana na uzoefu wake katika michuano mikubwa barani Afrika.

Katika mchezo mwingine wa Kundi A, Uwanja wa Gombani, Pemba, URA  ya Uganda imetoka sare ya 2-2 na Chuoni ya Zanzibar.

Mabao ya URA yamefungwa na Owen Kasuule dakika ya 44 na 57, wakati ya Chuoni yalifungwa na Shaaban Moke dakika ya 21 na Mwinyi Mngwali dakika ya 45 


No comments:

Post a Comment