Search This Blog

Sunday, January 5, 2014

HATIMAYE LEWANDOSKI AJIUNGA NA BAYERN MUNICH KWA MKATABA WA MIAKA MITANO


Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski atajiunga na klabu ya Bayern Munich kwa uhamisho huru mwishoni wa mwa msimu huu, mabingwa wa Ujerumani wametangaza.
             
Mshambuliaji huyo wa Poland, ambaye aliisadia Dortmund kushinda makombe mawili mfululizo ya Bundesliga 2011 na 2012, amesaini mkataba wa miaka mitano. 
Lewandowski alitangaza nia yake ya kuondoka Westfalenstadion pindi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu, na akawa anahusishwa na kujiunga na wapinzani wao Bayern. 
Lewandoski, 25, alijaribu kulazimisha kuuzwa kipindi cha kiangazi kilichopita lakini Dortmund waligoma kumuuza na kusisitiza lazima amalize mkataba wake.
Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alitangaza dili la Lewandoski, akisema: "Tuna furaha uhamisho huu umekamilika kwa mafanikio.
"Robert Lewandowski ni mmoja ya washambuliaji bora ulimwenguni, atakiongezea ubora kikosi chetu cha FC Bayern."

No comments:

Post a Comment