Search This Blog

Sunday, January 5, 2014

BEKI DONALD MOSOTI ADAI ANA DENI SIMBA

LICHA ya kucheza katika kiwango kizuri tangu ametua katika kikosi cha Simba, beki wa kati Donald Mosoti Omwanwa amesema ana deni la kulipa kwa mashabiki wa timu hiyo.
Mosoti alijiunga na Simba Desemba mwaka jana akitokea Gor Mahia ya Kenya na ana mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa  Msimbazi.
Beki huyo aliuambia mtandao huu kwamba, anahisi ana kitu cha ziada anachopaswa kukitoa kwa timu yake hivyo ni kama ana deni la kulipa kwa klabu hiyo.
Simba ilitumia kiasi cha Zaidi ya dola 30,000 kumnasa beki huyo kutoka Gor baada ya Kocha Zdravko Logarusic kumuhitaji kikosini. Logarusic amewahi kufanya kazi na Mosoti akiwa Gor msimu uliopita.
“Najiona nina deni Simba, kwani bado sijawatumikia ipasavyo na bado nina mechi nyingi za kucheza hapa. Mashabiki najua kila mara wanataka vitu vingi kutoka kwangu ninajituma kuhakikisha Simba inafanya vizuri,” alisema Mosoti.
Tangu alipotua katika kikosi cha Simba mwezi uliopita, Mosoti amekuwa beki tegemeo wa katikati akicheza kwa kusaidiana na Joseph Owino ambaye awali alikuwa akicheza na Glbert Kaze.
Beki huyo ameichezea Simba mechi tatu hadi sasa kwani alicheza mechi ya kwanza dhidi ya Yanga Desemba 21 mwaka jana na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Mosoti aliichezea Simba dhidi ya AFC Leopards katika Kombe la Mapinduzi na kupata ushindi wa bao 1-0 kabla ya jana kutoka suluhu na KCC ya Uganda.

No comments:

Post a Comment