Search This Blog

Wednesday, January 8, 2014

GWIJI WA BRAZIL RONALDINHO ASAINI BESIKTAS.




Nyota wa zamani wa Barcelona Ronaldinho amejiunga na klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki kwa usajili huru.
Gaucho mwenye umri wa miaka 33 amesaini mkataba wa miaka 2 na nusu kujiunga na Besiktas inayoutumia uwanja wa BJK İnönü,taarifa hizi zimedhibitishwa na gazeti la ‘De Telegraaf‘ la nchini Uholanzi – inasemekana Ronaldinho atakuwa akilipwa kiasi cha kati ya Euro milioni 10 na 15 kwa mwaka.
Inasemekana sababu kubwa ya Ronnie kuhamia tena ulaya ni kujaribu kurejesha kiwango chake ili aweze kumshawishi kocha wa timu ya Taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari ili aweze kujumuisha jina lake kwenye kikosi cha Brazil kinachotaraji kushiriki fainali za kombe la dunia baadae mwaka huu.
Hivi karibuni gazeti la EL PAIS la nchini Uruguay lilimtangaza Gaucho kuwa mwanasoka bora wa bara la Amerika ya Kusini kwa mwaka 2013 baada ya kuiongoza timu yake ya Atletico Mineiro kutwaa kombe la Copa Libertadores kwa mwaka 2013 ikiwa ni pamoja na kufunnga jumla ya mabao 17 na kutoa pasi za mwisho 11 kwenye jumla ya michezo 36 aliyocheza.

No comments:

Post a Comment