Search This Blog

Friday, December 27, 2013

CLOUDS KUPAMBANA NA MAKIPA WA LIGI KUU KESHO

 Nahodha midifield kisheti,MBWIGA MBWIGUKE...Amerejea baada ya kuwakosa YANGA kwenye mchezo uliopita.
   Winga hatari Nuno Kabezi bado anasumbuliwa na goti lakini matumaini ya kucheza bado yapo
Mshambuliaji hatari Alex Luambano yupo tayari kuwafunga makipa.



TIMU ya soka la Clouds Media Group Limited inayomiliki vituo vya redio vya Clouds FM na Choice FM pamoja na Clouds TV, kesho Jumamosi jioni itajitupa kwenye Uwanja wa Kinesi kucheza na timu ya magolikipa wa timu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Timu ya Clouds Media Group Limited itajumuhisha wafanyakazi wa redio za Clouds FM na Choice FM pamoja na Clouds TV,
 
ambapo miongoni mwao wapo Shaffih Dauda, Alex Luambano, Mbwiga wa Mbwiguke, James Tupatupa, Chriss Kahongo, Ezra Kaaya, James Tupatupa, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ na wengineo.
Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo, Dauda amesema timu yao imejiandaa vilivyo kuzima ngebe za makipa hao wanaoongozwa na nahodha wao Shaaban Kado wa Coastal Union.
 
“Tumejiandaa vizuri kushinda mchezo huu na ni matumaini yetu kwamba tutaibuka na ushindi mnono, wachezaji wetu wote wako vizuri kupambana,” alisema Dauda ambaye hucheza nafasi ya ushambuliaji.
Kwa upande wa timu ya makipa, Kado amesifu uwezo wa makipa hao na kusema wamejipanga kuionyesha kazi Clouds Media Group.
“Kuna wachezaji wengi makipa ambao tuna uhakika watafanya vizuri na naomba watazamaji waje wengi kutazamamechi hii,” alisema Kado.
 
Miongoni mwa makipa watakaocheza mechi hiyo ni Kado, Hussein Sharrif ‘Casillas’, Juma Kaseja, Deo Munishi, Ali Mustapha ‘Barthez’, Amani Simba na wengineo wanaotamba ligi kuu. 

1 comment:

  1. Da!,yani ni bonge la mechi.shaffih dauda naomba unipigie hat-trick,ili mbwiga akuvulie kofia.

    ReplyDelete