Search This Blog

Sunday, November 10, 2013

UNAFIKI WA VIONGOZI SIMBA, UKWELI KUHUSU KASEJA.....

 KIPA Juma Kaseja ametua Yanga kwa mara nyingine baada ya Simba kuachana naye kabla ya kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Bara, sababu ikatajwa kuwa ameshuka kiwango.

Viongozi wengi wa Simba walipigana vikumbo kuhakikisha sababu za kumuacha Kaseja zinachukua nafasi kubwa kwa jamii kuliko mazuri aliyofanya kwa klabu hiyo kongwe nchini.

Walipoona sababu ya kuwa chini ya kiwango haiingii akilini mwa wadau wa soka hasa mashabiki wa timu hiyo, viongozi hao walibuni kauli nyingine waliyosema kwamba kipa huyo amekuwa na tabia ya kuuza mechi. Hapo walifanikiwa kwani baadhi ya watu hawakutazama aina ya timu waliyokuwa nayo na matokeo wanayopata.

Tazama mechi ya Simba na Yanga ya msimu uliopita, Simba haikuwa na kikosi bora hivyo waliambulia kipigo cha mabao 2-0 Kaseja akiwa langoni. Hakikutazamwa kikosi lakini ikaonekana Kaseja ndiye cha kipigo hicho huku ukweli kuhusu kikosi dhaifu ukikwepeshwa.

Wakati uongozi wa Simba ukipigana vikumbo kuhakikisha unaachana na Kaseja kwa kumuwekea sababu mbalimbali, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen mara kadhaa amekuwa akiwaaibisha viongozi hao kwani amekuwa akimuita Kaseja katika kikosi chake.


Mijadala ikaanzishwa katika mitandao ya kijamii na hata katika vyombo vya habari kwamba yupi mkweli kati ya Poulsen na viongozi wa Simba.


Kwa kutambua kwamba soka ni kazi yake, Kaseja akaanza kujifua ili kutunza kipaji chake na kweli, leo hii amepata mkataba wa kuitumikia Yanga kwa miaka miwili tena.POULSEN ALIWAAIBISHA VIONGOZI WANAFIKI
Sababu za kuachwa kwa Kaseja kuhusu uwezo na kuuza mechi zikachagizwa na kisingizio kipya cha kipa huyo kuwa 'babu' yaani mzee ambaye hawezi kuwa na faida katika timu.
Poulsen hakufanyia kazi mizengwe ya viongozi hao iliyosababisha kipa huyo kutupwa nje ya timu huku akiwa na uwezo wake. Pamoja na hali hiyo ya Kaseja kutokuwa na timu, bado Poulsen aliendelea kufanya kazi na kipa huyo na kupata mafanikio.

Na hata matatizo yalipotokea katika kikosi cha Taifa Stars hasa kutopata ushindi, yalikuwa ni matatizo ya jumla ambayo hayakumuhusu Kaseja peke yake. Pamoja na kuitwa kikosini

mara kadhaa akiwa na makipa namba moja wa klabu za Ligi Kuu, kama Ali Mustapha 'Barthez' wa Yanga, Mwadini Ally na Aishi Manula wa Azam, bado Kaseja alikuwa bora na kuwa kipa namba moja.KIONGOZI HUYU ADUI WA KASEJA
Hata siku moja Kaseja hakuwa anapendwa na viongozi wote wa Simba kutokana labda ya tabia yake ya kudai maslahi yake na wenzake wakati mwingine, hivyo alijikuta akiwa haelewani na viongozi kadhaa wa klabu hiyo.

Japokuwa Kaseja mwenyewe hakuwa tayari kumtaja kiongozi huyo, lakini anafahamika kwamba ni kiongozi huyo ni mjumbe wa kamati ya utendaji (jina tunalo ) ambaye anatajwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Kaseja anaondoka klabuni hapo vyovyote viwavyo.

Kiongozi huyo ndiye aliyeshiriki katika kuhakikisha Kaseja anaondoka na moja kati ya mikakati aliyoiweka ni kuhakikisha anasajiliwa kipa Wilbert Mweta akitokea Toto African ya Mwanza. Lengo la kiongozi huyo ilikuwa ni kuona Mweta anafanya vizuri ili Kaseja aweze kuondoka klabuni hapo.
Huo ulikuwa ni mkakati wa awali ambao Kaseja alikumbana nao na kushinda kwani Mweta hakuweza kuonyesha uwezo wa hali ya juu kumzidi kipa huyo 'mkongwe' katika soka la Tanzania.
Baada ya mkakati huo kushindikana, ndipo zilipoibuka sababu nyingine za Kaseja kushuka kiwango na pia kuwa ni mzee. Wakati viongozi wanasema Kaseja ameshuka kiwango, aliyekuwa kocha wa Simba, Milovan Cirkovic alikuwa akimtumia, hili lilikuwa tatizo kiuongozi.

MKAKATI WA PILI

Haraka viongozi wa klabu hiyo wakaanza mazungumzo na kipa Abel Dhaira wa Uganda huku wakijua mkataba wa Kaseja unaelekea ukingoni, huyo alisajiliwa na Simba huku akipewa maelekezo ya kuingiza baadhi ya vipengele katika mkataba ikiwemo kile kinachoeleza kuwa anapaswa kuwa kipa namba moja katika timu.
Pia Dhaira aliwekewa mazingira ya kuwa kipa anayelipwa zaidi katika klabu hiyo ili uongozi uone kwamba hakuna haja ya kuwa na mtu kama Kaseja wakati tayari ina kipa mwingine.
Hakika mkakati huu ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa na Kaseja akawa nje ya Simba hadi leo hii.


KASEJA ANAJUA ANACHOFANYA
 

Tofauti na wachezaji wengine, Kaseja mara nyingi amekuwa akipenda kufanya mazoezi binafsi kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo jambo linalomtofautisha na makipa wengine wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Huyu yupo mstari wa mbele kudai haki zake na za wachezaji wenzake pale inapobidi ndiyo maana anakuwa adui wa viongozi walioingia katika soka kwa ajili ya kunyonya wachezaji.
 
SIMBA WAUMBUKA 
Huku ikitegemea Dhaira atafuta aibu ya kutokuwa na Kaseja, ndani ya muda mfupi uwezo wa kipa huyo ulipungua na kuzua hofu ndani ya klabu hiyo kongwe nchini. Haraka benchi

la ufundi la Simba likamtupa benchi Dhaira na kumpa nafasi kipa chipukizi Abuu Hashimu.
Kutokana na mabadiliko hayo ya ghafla lango la Simba halikuwa makini hadi kuiacha timu hiyo ikishika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu.  IWEJE AUZE MECHI HALAFU WAMSAJILI.
 
Hata siku moja, Yanga hawawezi kuwa wajina kumsajili mchezaji iliyekuwa ikimtumia katika kununua mechi za Simba ili awe kipa wao namba moja. Hizi ni propaganda zilizopitiliza.
Japokuwa viongozi wa Simba hawaitaja klabu iliyokuwa ikinunua mechi za Simba kupitia kwa Kaseja, lakini wachambuzi wa mambo wanaamini klabu hiyo ni Yanga kwa asilimia 70 huku Azam ikipewa chache sana.

Leo hii Kaseja kasajiliwa na Yanga, ina maana Yanga itakuwa tayari kuwa na kipa muuza mechi ambaye walikuwa wanamtumia?  Kokote kule duniani huwa hakuna kitu kama hicho.


13 comments:

 1. Viongozi wa simba wanafiki kama na wewe ulivyo mnafiki
  Nilidhani unafiki wako huu ungekuwa na mashiko na kueleweka vema wakati ule kaseja ametoka kutemwa
  Lakini kwa sasa ulitakiwa usifu uongozi wa yanga kwa kuthamini ubora wa kipa Juma K Juma na kumrudisha dimbani kuliko kutaja walichokosea viongozi wa simba (kama ulitaja madhaifu hayo wakati huo huna haja ya kurudia)
  Acha unafiki wewe kwanza.....

  ReplyDelete
 2. Hapana Simba hawakumtaka kaseja. kwahiyo hizo habari ulizoandika ni za mtaani TUPE USHAIDI . kumbuka Kaseja ni Mchezaji si lazima acheze simba tu.

  ReplyDelete
 3. Jaman kulikoniiiiiiiii kila kukicha Kaseja Kaseja..........Kaseja ninaniiiiiiiii,,,,?..mbona sijaonaa mjadara pale Barthez alipoondoka Simba Kwenda Yanga.....au Yew Berko kutolewa mkopo wkt kiwango chake kilikuaaa cha juu sn kuliko Kaseja ktk msimu huu maana Kaseja alipokua Yanga alikua Kipa namba mbili lkn hakuna mtu aliyeamua kuandikaa makala wala nini,,,sasa uzushiii huu mnautoa wapiiii,,,?.Kaseja hakuachwa Simba hilo ndilo lakuzingatia nakuandikaaaaaa,Mkataba wa Kaseja na Simba uliishaa sa nafikiri ilikua ni heri kuwapongeza pande zote mbiliiii kwakumaliza mkatabaaa salama bilaaaa pande yeyote kuathirika kwa chochote sio kutulisha sumu kati ya wanachama,wapenzi wa simba na viongozi wao,,halafu kesho mtu huyu huyu atauliza kwanini soka la bongo linadidimiaaa,,,,waache Simba iendelee kua Simba na Kaseja awe Kaseja,,,Simba ni Taasisi na Kaseja ni mtu(mfanyakazi),,,,,,anapita hatujuiiiiii ya kesho......ebu tujadiliii mambo mengineeeeeeeee jamn

  ReplyDelete
 4. At times huwa hueleweki na inakuwa km unatumiwa. Hivi kweli unaweza andika Mweta alisajiliwa kwa sababu hizo ?? Simba ilikuwa na makipa wangapi, na klabu nyingi zinakuwa na min makipa wangapi ??

  I thought you are better than that !!

  ReplyDelete
 5. Wewe ni mtu wa ajabu sana mie sijui hata ambacho huwa unafikiria kuandika kama huwa unapata hata ushauri kwa waandishi wenzako, maana huwa unaandika ujinga kabisa hata hiyo taaluma ya uandishi sina uhakika km uliipata darasani au uliipata chini ya mwembe. Ushauri tu tena wa bure uwe uanafikiria kitu unachotaka kuandika na kukiweka hadharani, maana ulichoondika hapo juu ni utmbo na majungu tupu. Umeshindwa kueleza ujinga wako wa kulalamika ka toto dogo kuwa uliishia wapi safari yako ya kwenda uswissi kulalamika leo unakaa kufikiria kutuandikia utumbo hapa. Wewe simba una mchango gani pale unaishia kuponda viongozi! Kwani ni lazima Kaseja abaki simba!! Anzisha team yako umsajili awe wa maisha yako. Kaseja hakuzaliwa abakie simba tu

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mwandishi kafanya kazi yake na wewe toa mawazo kaka au kafanye wewe kazi ya uandishi utaandika mazuri kama vipi toa mawazo yako

   Delete
 6. uyo aliyetoa comment hapo juu aona hajielewi nini anachokifanya wala anachokiandika kweli atanzania tuna akili mgano hata hilo aliloeleza shaffii tena kwa kutazama igezo muhimu bado tuu kuna baadhi ya watu wanaona ni unafiki? we Tanzanians we ave a long way to go until we reach/achieve the success in football ni hayo tu naomba kutoa hojaaaaa!

  ReplyDelete
 7. SIMBA BILA YA KASEJA INAWEZEKANA. SIDHANI KAMA ANAKARIBIA HATA ROBO YA MWAMEJA LAKINI MWAMEJA ALIONDOKA NA SIMBA IKACHUKUA UBINGWA BILA YEYE MARA NYINGI TU. NA SIMBA ILISHAKOSA UBINGWA MARA NYINGI TU IKIWA NA KASEJA, MSIJARIBU KUMFANYA MUNGU MTU KWA MAPENZI YENU BINAFSI. AU SABABU WOTE MNAPANDA TRENI WAKATI MKIENDA KWENU? HIVI WACHEZAJI WANGAPI KASEJA ALIKUA HAONGEI NAO NA YEYE NDIE CAPTAIN NA NYIE WAANDISHI UCHWARA WOTE MLIKUA MNAJUA? MBONA HATA MARA MOJA HAMJAWAHI KUANDIKA? AU NDIO MNAKULA TEN PERCENT KILA ANAPOSAJILIWA? TUMECHOKA NA HADITHI ZISIZOKWISHA. KAMA NI MSEMA KWELI BASI ANZA KUANDIKA MADUDU YANAYOFANYWA NA MABOSI WAKO KATIKA KUWADHULUMU VIJANA WANAOJIAJIRI KUPITIA MUZIKI.

  ReplyDelete
 8. Leo Kaseja amekuwa lulu baada ya kusajiliwa na Yanga...? Shaffih si ndo nyie mlikuwa mnamasema Kaseja kachoka, kacheza mechi nyingi,, anapoteza umakini... Mkamsifia sana Bartez kwa kusajiliwa Yanga, kwamba Kaseja alikuwa anambania alivyokuwa Simba... Mpaka timu ya Taifa Kaseja alikuwa anazomewa.... Yanga hawakususia kuishangia timu ya Taifa??.... Sasa mtuambie Bartez kiwango kimeshuka au vipi na nini hatima yake???

  Hizi makala zenu mnaipamba YANGA ili mkachukua vi elfu 10, 10 kwa Manji... Hivi leo mnaweza kusema Kaseja ndo suluhisho la Mechi za Kimataifa za Yanga?? Acha unafikiti....

  ReplyDelete
 9. Kila mtu atoe mawazo yake na maoni yake kwa uelewa wake wala sio malumbano....mwandishi wa habari katoa anayoyajua kama mwandishi na ueledi wake basi wasmaji tutoe mawazo yetu kuanzia pale..heeeeee jamani....

  ReplyDelete
 10. Kila mchezaji enzi yake itakwisha tu, wala haina haja yq kuilaumu simba juu ya kumuacha kaseja na kuisifia yanga kwa kumsajili kaseja....it's about time, kila jambo lina wakati wake....enzi ya kaseja imekwisha simba na labda enzi ya yanga kwa kaseja imeanza tena...huu ndiyo mpira, mchezo wa kubadilishana wachezaji, soka ipo kama bahari vile mara inajaa huku na kubwa kwingine, wanahabari wetu wa tz mara nyingi mitazamo yenu inakuwa haina maana sana, sometimes mmekuwa kama kinyonga, jambo hilohilo leo unalisifia lakini kesho unakuja kubadilika na kuliponda.......hakuna mshindi juu ya kaseja...mshindi ni kaseja mwenyewe kwa kupata timu ya kucheza mpira..........msimalize maneno yanga na simba baba moja mama mmoja, tena mapacha wanaofanana sana..... wote vigeugeu, sasa yakija kumkuta kaseja ya yanga mtaandika makala nyingine?

  ReplyDelete
 11. Kitu kimoja nilichogundua mwandishi huyu anajitahidi kumpamba kaseja.Simba kama taasisi ina maamuzi yake yaheshimiwe.
  Nakumbuka sana mwandishi unavyohubiri nidhamu ni kila kitu.Vilevile unajua ya kwamba Maximo alimshutumu Kaseja kwa nidhamu.
  Kumbuka hata alisababisha Chuji atoke Simba.Taarifa ni nyingi tu zikimhusisha Kaseja kuwafanyia wenziwe fitna.
  Yote tuyaache.Waache Simba wafanye yao.
  Please wewe andika mengine sio kuwapakazia viongozi ea Simba ma kuwagombanisha na wanachama

  ReplyDelete
 12. This comment has been removed by a blog administrator.

  ReplyDelete