Search This Blog

Sunday, November 10, 2013

THE TANZANITE WAREJEA BAADA YA KUWAUA MSUMBIJI 5-1

 Mery Kanyaga, akimpongeza binti yake, Shelder Boniface ambaye ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, wakitokea Msumbiji katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Dunia za wanawake ambako Tanzanite iliichapa Msumbiji mabao 5-1 huku Shelda akitupia matatu kati ya hayo. (Picha Habri Mseto Blog)
 Mery Kanyaga, akiwa amepozi na binti yake, Shelder Boniface mara baada ya kuwasili akitokea Msumbiji na timu ya taifa ya wanawake ya Tanzanite. Shelder aliifungia timu yake mabao matatu.
 Nahodha wa The Tanzanite, Fatuma Issa akizungumza na waandishi wa habari.
 Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao baada ya kuwasili jijini Dar es Salam wakitokea Msumbiji.
Kocha Mkuu wa The Tanzanite, Rogasin Kaijage.
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ wakipanda basi baada ya kuwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji.
 Wachezaji The Tanzanite wakiwapungia mikono mashabi waliofika kuwapokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, wakitokea Msumbiji.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura akipeana mkono na wachezaji wa Tanzanite mara baada ya timu hiyo kuwasili jijini Dar es Salaam ikitokea Msumbiji. 
 Wachezaji wa timu ya taifa ya wananwake chini ya umri wa miaka 20 'Tanzanite' wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Msumbiji katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Dunia la wanawake dhidi ya Msumbiji, ambako Tanzania ilishinda 5-1.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ wakiwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Dunia za wanawake ambako Tanzanite iliichapa Msumbiji mabao 5-1. 

No comments:

Post a Comment